Hata wakiristo wanapokufa haitakiwi kucheleweshwa

Hata wakiristo wanapokufa haitakiwi kucheleweshwa

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,553
Reaction score
14,861
Katika Matendo ya Mitume:

“Anania, akaposikia maneno haya, akaanguka, akafa... vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamtoa nje, wakamzika.”
(Matendo 5:5–6)



Na baadaye mke wake Safira:

“Wakamtoa, wakamzika karibu na mumewe.”
(Matendo 5:10)



Hii inaonyesha kuwa maziko yalifanyika mara moja baada ya kifo.


---

Hitimisho la Kibiblia

Ingawa Biblia haisemi moja kwa moja "mtu akifa azikwe haraka" kama amri, maandiko yanaonyesha kwamba katika tamaduni za kibiblia:

Maziko yalifanywa haraka, mara nyingi ndani ya siku hiyohiyo.

Ilikuwa ni ishara ya heshima kwa mwili wa marehemu na pia kutii sheria za kidini
 
On coming 101 days.
Hence proven. Ongeza kifungu cha biblia mkuu maana hapo anania alianguka tu, je, labda alikuwa anaumwa mpox au ebola hiyo kuzuia kuenea kwa ugonjwa wakaona wazike haraka same kwa mkewe safira.
 
Sioni mantiki ya kumuanika mtu na kuzurura nae kama mwenge. Mtu akifa apelekwe kwao akazikwe
 
Kila watu na utamaduni wao,hilo la kuchelewesha naliona zaidi kwa wachaga,msiba unageuka sherehe, lakini kwetu japo ni wakristo asilimia 100,ukifa hupaswi kukaa zaidi ya siku mbili labda kama mtu anasafirishwa toka mkoa A to B
 
Back
Top Bottom