Hata vitabu vya risiti hakuna, tunaelekea wapi?

Hata vitabu vya risiti hakuna, tunaelekea wapi?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
Nikiwa nimepotelewa mali zangu, nikaenda kuripoti polisi, nikapewa utaratibu wote lakini ilipofika wakati wa kuonana na mhasibu wa kituoni - nakutana na janga hili ... "Vitabu vya risiti vimeisha - nenda kituo kingine jirani"
Hivi tunaelekea wapi? Si hilo tu naskia hata hati za kusafiria ni kitendawili ... karatasi za kuduruza nyaraka bungeni kitendawili ... mbona mwelekeo hauonekani jamani?
 
Hiyo ndiyo safari ya kuelekea kwenye Tanzania ya viwanda Ili tuwe na uwezo wa kujichapishia risti wenyewe.
 
SUBIRINI KWANZA SERIKALI IMEWEKEZA NGUVU NYINGI KUJENGA VIWANDA KWANZA..

OVA
 
juzi pale kituo cha polisi niliambiwa kitabu hakuna nilishangaa sana,yaani tumeshindwa hata vitabu?binafsi naona watanzia wote tumepitîwa na tetemeko tupewe misaada tu,hii aibu.
 
Kukosa vitabu vya risiti kituoni ni uzembe tu wa huyo mhasibu wa hapo kituoni. Atumbuliwe tu.

Hebu eleza ni kituo kipi.
 
Nikiwa nimepotelewa mali zangu, nikaenda kuripoti polisi, nikapewa utaratibu wote lakini ilipofika wakati wa kuonana na mhasibu wa kituoni - nakutana na janga hili ... "Vitabu vya risiti vimeisha - nenda kituo kingine jirani"
Hivi tunaelekea wapi? Si hilo tu naskia hata hati za kusafiria ni kitendawili ... karatasi za kuduruza nyaraka bungeni kitendawili ... mbona mwelekeo hauonekani jamani?
Umbea tu huo.
 
Tanzania imepotea
Na walioipoteza ni CCM na serikali yake. ...
Nakumbuka enzi za miaka ya 80's kuna jamaa alikuwa na uwezo wa kutengeneza mizani, ila serikali ilikuwa ikimsumbua sana. Huyo angeandaliwa vyema - kiwanda cha mizani kingekuwepo tu.
Haya watu tuliokulia vijijini tulikuwa tunatengeneza baiskeli za miti ... serikali ingetuwezesha kwa sasa viwanda vya baiskeli vingekuwa vingi tu.
Kuna watu walijaribu hata kutengeneza siraha za moto (magobole) - hao walisumbuliwa sana ...
Hivi taifa la viwanda bila maandalizi ulishaliona wapi?
Akimaliza awamu yake (10yrs) anayekuja anakuja na mambo mengine tofauti kabisa! Dira ya CCM ni kuhakikisha Tanzania haina mwelekeo.
Viwanda vya kuprinti viko kibao na havina kazi ... leo hii serikali haina vitabu vya risiti? Na mianya hiyo ndo hutumika kwa wajanja kutengeneza vitabu feki kupiga hela!
 
Umbea upi kijana? Sikuambiwa ni mimi mwenyewe ndo nilikutana na maneno hayo kituo cha polisi jijini Mwanza, nikaambiwa niende kituo cha Kirumba.
Fafanua vizuri sana taarifa yako ili ifanyiwe kazi kwakua haijitoshelezi.
 
Back
Top Bottom