Kwanza, ni 'umebadilika' siyo 'umebadirika'.
Pili, wala sijabadilika kabisa.
Bado ni yule yule wa siku zote.
Labda wewe ndiye uliye badilika.
Jiangalie.
Dictatorial tendencies zake nimeshaziongelea sana humu.
Wewe ulikuwa wapi wakati nayazungumzia hayo?
Namtetea kuhusu jambo gani? Hebu kuwa mahsusi.
Mbona hilo ndilo ninalolifanya humu....
Magufuli juzi tu hapa nimetoka kumpinga kuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni.
Hata kuhusu Lissu kukamatwa na kuwekwa ndani nalo nimelipinga.
Sidhani kabisa kama Lissu alistahili kuwekwa ndani.
Lakini napinga madai yake kuwa rais anaendesha nchi kwa misingi ya upendeleo wa kikabila na kikanda.
Hebu ona hizi mada nilizowahi kuzianzisha juu ya Magufuli.....
Magufuli is the real deal
Nataka rais Magufuli ashindwe
Mliompigia debe Magufuli nawauliza swali...
Mwaka mmoja umetueleza mengi
Majuto ya mnunuzi?
Kaisoma na kuielewa katiba kweli?
Naibu Spika Tulia Ackson Mwansasu anapwaya, hafai
Rais Magufuli na maana ya neno 'catalyst'
Rais Magufuli na Libya
Haya, hebu nambie sasa....mimi ni mtetezi wa Magufuli muda wote?
Unataka niwe 'neutral' au 'balanced' kivipi zaidi ya nilivyo sasa?
Nakala iwafikie na
QUIGLEY na
valuablecock