Hata kama ni kuwajali machinga, kinachoendelea pale ubungo ni aibu

Moneyowner

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,423
1,251
Tukirejea kauli ya mkuu wa nchi kuwa hawa watu wasisumbuliwe, lakini kuna baadhi ya maeneo mtu mwenye akili timamu ukipita lazima upate kichefuchefu.

kwa watumiaji wa mandela road mradi wa flyover {ubungo interchange} unaendelea lakini machinga nao wamo wanajibanabana mara leo yuko hapa kesho kule wengine hadi wamesukumiziwa kwenye ukuta wa tanesco ambako ni hatari tupu..

sasa mi najiuliza hatuwezi tukapisha mradi mkubwa kama huu, naona kama tunawabugudhi wajenzi na ni aibu kubwa mno kushindwa kuacha eneo free ili mkandarasi afanye kazi yake kwa uhuru.

Hata watu wa osha sijui wako wapi pale ni site watu wanatakiwa wawe na safety gears .sasa machinga wanafanya kazi gani eneo la site bali na kuhatarisha maisha yao, kwa kweli ni aibu mno walitakiwa wapishe kwa nguvu yoyote.nguo zenyewe zinazouzwa zimechafuka vumbi mpaka basi.

najiuliza mpaka nashindwa kuelewa na wala sina kinyongo nao lakini walipaswa kupisha ujenzi,

Ova..
 
Machinga hao hao wanalipa
Nyumba,wanalisha familia,pia wao

wenyewe wanamahitaj yao
Sasa lazma mtu upambane uwezavyo
Mkono uende kinywan
 
Basi sawa acha wapambane, wala siona kiunyongo nao. ila lazima tujue kuna haja hawa watu wapewe maeneo salama zaidi.
Ttz mamlaka huzka ndo haztak
Kuwapa kiwanja wengekua wamewapa ucnge
Waona hapo mahali wako
 
Tukirejea kauli ya mkuu wa nchi kuwa hawa watu wasisumbuliwe, lakini kuna baadhi ya maeneo mtu mwenye akili timamu ukipita lazima upate kichefuchefu.

kwa watumiaji wa mandela road mradi wa flyover {ubungo interchange} unaendelea lakini machinga nao wamo wanajibanabana mara leo yuko hapa kesho kule wengine hadi wamesukumiziwa kwenye ukuta wa tanesco ambako ni hatari tupu..

sasa mi najiuliza hatuwezi tukapisha mradi mkubwa kama huu, naona kama tunawabugudhi wajenzi na ni aibu kubwa mno kushindwa kuacha eneo free ili mkandarasi afanye kazi yake kwa uhuru.

Hata watu wa osha sijui wako wapi pale ni site watu wanatakiwa wawe na safety gears .sasa machinga wanafanya kazi gani eneo la site bali na kuhatarisha maisha yao, kwa kweli ni aibu mno walitakiwa wapishe kwa nguvu yoyote.nguo zenyewe zinazouzwa zimechafuka vumbi mpaka basi.

najiuliza mpaka nashindwa kuelewa na wala sina kinyongo nao lakini walipaswa kupisha ujenzi,

Ova..

Kwanza wee ni chama gani aisee... ?
 
Je hayo ni ya muhimu zaidi ya usalama wao?
Lkn kama mamlaka husika
Zmekataa kuwatengea sehem ya
Kufanyia shuhuli zao wafanye nn??

Kumbuka hata wao hawako hapo
Kwa kupenda kwao na wala hawafrahii
Kuwa hapo kwa sababu wanAjua madhara ya
Hapo walipo,

Lakin Sasa wataenda wap?
Wako hapo kwakua hawana otherwise
Pakwenda hakuna mamlaka znawadharau

Mungu wao tu ndo anasmama na wao
Mahali walipo
 
Hata kama mkuu tujifunze kuwa na taratibu
Ndyo mkuu utaratibu unafaa kuwa
Lakin mfano ndyo ww

Embu niambie n wap utaenda
Kufanyia hyo biashara yako
Na Kila unapoenda utafkuzwa
Unajikuta wacha ujibane hapo hapo
Maana unataka kula n.k

Kwann mea wa ubungo
Aswapatie eneo wakafanyia shuhuli zao
Kama n ushuru c hata wao watalipa
 
Machinga hao hao wanalipa
Nyumba,wanalisha familia,pia wao

wenyewe wanamahitaj yao
Sasa lazma mtu upambane uwezavyo
Mkono uende kinywan
Mkuu kumbuka kua SAFETY FIRST,
Sasa kama hao machinga wanaingia eneo la site bila kua na safety gears huoni kua ni hatari kwa maisha yao? kama ikitokea ajali eneo hilo la site, si ajabu hata wewe utakuja hapa na kuanza kuilaumu mamlaka husika!
Hakuna kitu chenya thamani ya juu kuliko uhai wa mtu.
 
Lkn kama mamlaka husika
Zmekataa kuwatengea sehem ya
Kufanyia shuhuli zao wafanye nn??

Kumbuka hata wao hawako hapo
Kwa kupenda kwao na wala hawafrahii
Kuwa hapo kwa sababu wanAjua madhara ya
Hapo walipo,

Lakin Sasa wataenda wap?
Wako hapo kwakua hawana otherwise
Pakwenda hakuna mamlaka znawadharau

Mungu wao tu ndo anasmama na wao
Mahali walipo
Umemwelewe kweli mtoa mada ndugu? Kwa nini unakimbilia ku comment kitu usichokielewa? Mtoa mada amewalaumu machinga au mamlaka husika?
 
Back
Top Bottom