Hivi karibuni kumezuka tabia ya watu wanaojiita 'content creators' kusafiri kwenda kwenye jamii za Waadzabe na kuwapiga picha na kuchukua video ambazo nyingi za hizo video ni za kuwadhalilisha na kuwaonyesha kama watu ambao hawana ustaarabu na vikaragosi.
Juzi kuna watu waliwatembelea na kuwapatia bangi na kuwarekodi wakivuta bangi. Wengine wanatoka nchi za nje na kufanya uhuni huu.
Serikali inatakiwa kuchukua hatua kali na kukomesha tabia kama hizi za kuwadhalilisha watanzania. Usasa wa watanzania na watu wengine duniani umewafanya kuamini kuwa watu kama Waadazabe ni watu walipitwa na wakati ambao hawahitaji kuheshimiwa.
Napendekeza serikali ichukue hatua zifuatazo kuhakikisha kuwalinda Waadizabe na makabila mengine ya asili:
1. Kabila la Sentilese huko India ambalo linafanana na Waadizabe lilitungiwa sheria maalum ya kuwalinda na hakuna anayeruhusiwa kuyatembelea bila kibali maalumu.
Walifanya hivyo kuhakikisha mila zao zinalindwa na watu wa magharibi hawatumii fursa ya kuyaona makabila haya kuweka propaganda zao.