Hasira za mtoto

Hasira za mtoto

Slim
Wangu nae alikuwa na hasira hasira pia tabia ya kukunja uso muda mwingi. Kilichomuondolea hiyo hali ni kucheza nae sana pia kumsukuma yeye acheze mwenyewe. "uko wapi mpira? Kacheze mpira. Piga makofi, imba, cheza mziki" ni maneno madogo madogo yanayoweza kumtoa mtoto kwenye hali hiyo. Akifanya kakitu kadogo msifie, kama mko wawili watatu
muongeleeni akiwa anafanya kitu mf. "Brenda amekunywa maji? Anapenda maji ehh? Asiee anapenda sana." Ongeeni huku mmefurahi, sifa kwa wingi na makofi vitamfanya achangamke kwa furaha.

Swala la kufinya watu wengine na kujigonga unapaswa umkemee bila kujali kilio chake kwa muda mfupi. Mgombeze ajue kabisa sio tabia nzuri (wangu kaacha kabisa maana alianza tabia ya kujigonga na kupiga) ili aache. Akimfinya mtu mwingine na yeye afinywe kidogo (namaanisha kidogo jamani sio mumtoe ngozi au abaki na alama) kusudi ajue inauma akifanya hivyo na yeye akifanyiwa hivyo anaumia kwahiyo baada ya muda ataacha kusudi na yeye asifanyiwe hivyo.

Uzuri ni kwamba watoto ni wepesi sana kusahau na wanabemblezeka kirahisi sana ikiwa upendo unaomuonyesha anauona kweli. Sio unambembeleza huku una hasira nae/uso umeukunja n.k maana hata kama hakuangalii anahisi. Kwahiyo dawa ni kwamba ukitaka afanya kitu mwambie taratibu kwanza akiakaidi ndio uwe mkali. Na ukiwa mkali let say umemuondoa kweye tv,umemnyang'anya kitu cha hatari badili mawazo yake kwa kumuongelesha, kumchezesha, kumtekenya na vitu kama hivyo ili asipate nafasi ya kupandisha hasira. Yani control hasira zake.

Wangu mimi hata akianguka naweza kumnyamazisha kabla hata sijamuinua. Nimemfundisha kukumbatia na kubusu kwahiyo kwa namdaka pale pale akianza kulia na "jamani, mtoto ameumia. Njoo nikumbatie/njoo nikukumbatie" basi atajitutumua ainuke mwenyewe afuate hug/kiss. Akinikumbatia hasira/maumivu yake yanayeyuka fasta. Hata nikishamgombeza amuacha imuingie kidogo alafu hug a kiss vinafuata. Hii imemsaidia sana kiaso kwamba hata akiwa aamchokoza mtoto mwingine (ana kamkono kepesi ) nikimwambia "acha kumpiga mwezio, haya mchum/mkumbatie haraka" anatekeleza na uchokozi unaishia hapo.

Jamani watoto rahaa. . .
Ngoja niishie hapo maana naweza kuandika mpaka kesho.
Sizinga hehehehe umpige mtoto wa miezi mitano hayo mabao yote jamani kwenye mashavu yapi? Huyo ni wa kubembeleza tu. Bana

Lizzy ubarikiwe sana!
 
Acha🙂iyo kitu mitishamba ipo kwa ajili gani ukiwa na jibu maombi umejikwaa maombo rwakatate. Kakobe.mzee wa upako.kwajima mmetuaribia vizazi da

Unatakiwa unatafuta tiba kwanza alafu mungu nisaidie

aliekuharibia kizazi nani? unajua maana ya imani?
 
Wana - JF, habari za asubuhi?

Naomba msaada wenu, nina mtoto wa kike, 18 months age, ana afya nzuri! shida yangu ni 1 tu, katika umri huu, anaonekana atakuja kuwa na hasira sana, dalili zinaonyesha atakuwa mtata sana, pia ana elements za utundu lakini hii sioni shida, najua ni stage tu ya makuzi.

Ila hili la hasira jamani, mpaka naogopa!

Wataalamu wa psychology, wazazi wenzangu na yeyote mwenye ushauri namna gani naweza kumsaidia binti yangu kupunguza kama sio kuondoa kabisa hasira!

slim5 ....Inaniwia vigumu kidogo kukuelewa, ni dalili zipi anazonyesha mtoto wako wa miezi 18 kuwa atakuja kuwa na hasira? Labda tuanzie hapo.....
 
Last edited by a moderator:
Kama sikosei wataalamu wanaiita hiyo hali kwa lugha ya kikoloni "TANTRUMS". Ni kawaida kwa mtoto wa umri huo kuwa na hii hali ingekuwa shida kama asingekuwa na hiyo hali kwani anaweza kuwa zoba.
 
Sizinga hehehehe umpige mtoto wa miezi mitano hayo mabao yote jamani kwenye mashavu yapi? Huyo ni wa kubembeleza tu. Bana
Usijali Lizzy nshakuelewa, nahisi nilikosea sana madame!! Huku Unga Ltd vumbi sana aisee
 
Last edited by a moderator:
Mwanangu cjamchunguza sana coz bado mdogo miez m3 lakin cjajua kama ana hasira ama vp btw napenda sana watoto jaman nafeel happy kuwa na watoto 2furah pamoja
 
Mwanangu cjamchunguza sana coz bado mdogo miez m3 lakin cjajua kama ana hasira ama vp btw napenda sana watoto jaman nafeel happy kuwa na watoto 2furah pamoja.
 
Back
Top Bottom