Hashiki mimba maskini!, kumbe kazaa na jini!

Kwani kaombewa ili jini ajihalalishe au aondoe tatizo hadi kufikia wewe kutaka kujua hatma ya ndoa yao?

Mumewe asimpende kwa sababu zipi tuanzie kwako?

Akijua lengo la kuombewa atajisikia faraja.

Kuna majini na uchawi hata vitabu vya dini vinasema.

Unachagua njia gani ya kupambana navyo. Kwa ushirikina au kwa kumuomba Mungu.

Mara zote Mungu ni muweza wa kila jambo hata kama atachelewa.

Wameenda kanisani wameombewa, basi kwa Nguvu za Mungu na imani yao kwa Mungu tatizo litaisha.

Suala la ndoa itakuwaje havihusiani na hili kwa sababu hajafumaniwa au hajapenda kupatwa na hali hiyo
 
Hakuna jini, shetani, malaika wala mungu.

Ni hadithi zisizo uthibitisho wala mantiki.
 
Umeeleweka vema kwa wale wajuvi wa mambo
na midhali amejikabidhisha kwa mola wake mwambie adumu katika maombi mwenyezimungu atamsaidia
JINNI ni kiumbe mwenye daraja la chini sana kwa mwanadamu ukimpatia na kumjuria
 
Dada huyu ni mchepuko wa Jamaa kwahiyo anapima urefu wa maji kwa miguu, usije ukawa umemtupia jini mwenzako ili uwawekee vikwazo ili uolewe wewe, kama hupendwi kwa hiari ya moyo yote uyafanyayo utawachelewesha tu lakini watavukaaa.
 
Wenye tabu ni hao wenye kuamini katika mambo ya usasili.
Mkuu haya madude yapo mkuu niamini

mimi yashanichagiza sana na nishafanya nayo kazi mkuu na mpaka maskani kwao nishatimba na hata watu wengi walioletewa maudhi nao nishatibu
Kama unataka uyahakikishe naweza nikakuelekeza namna ya kufanya na ukameet nao hata hapo ulipo au kama upo sehemu inapokutanishaa maji ya mto na bahari ikifika alhamisi usiku saa 6 nenda hapo arafu utakachoshuudia ni pm uniambie nini umeona
 
Mkuu haya madude yapo mkuu niamini

mimi yashanichagiza sana na nishafanya nayo kazi mkuu na mpaka maskani kwao nishatimba na hata watu wengi walioletewa maudhi nao nishatibu
Kama unataka uyahakikishe naweza nikakuelekeza namna ya kufanya na ukameet nao hata hapo ulipo au kama upo sehemu inapokutanishaa maji ya mto na bahari ikifika alhamisi usiku saa 6 nenda hapo arafu utakachoshuudia ni pm uniambie nini umeona

Hamna kitu.

Hayapo hayo.

Kama yapo nionyeshe yalipo.
 
*Kaombewa ili ajue tatizo,na liondoke pia.

*mumewe hataki aombewe,yeye kalazimisha,afu inajulikana kuwa ana watoto na jini!
Na mumewe hupo mbali naye kwa sasa,ila anajua tu kuwa mkewe anaombewa.
Huyu dada ni rafiki yangu sana.ila alipoolewa mawasiliano na mazoea tulikata.
Na yeye ndio kanipa hiyo stori.
Na akaniuliza kama ningekua mimi ndio mwanaume, ningekubali kuendelea kuishi na mtu aliyezaa na jini?

Sikumkatisha tamaa,nikampa moyo.akafarijika.na nina imani ndoa yao itasimama daima!
tu,leo ndio nimeamini kuwa haya mambo yapo!
Ni kumuomba tu mungu atuepushe nayo!
Luv
 
Hakuna majini wala mashetani.

Kama unaamini hayo mambo au kama ndo umeanza kuamini nakushauri uende ukapimwe akili.

Huenda umeanza kuwehuka!
Hata Mimi nilikua siamini kama wewe,ila acha nirudi kwa Mungu mbiombio,kuna mengi hatuyaoni ila yapo aisee.
Anasema alikua anaota tu ndoto anafanya mapenzi,ooh mara ana watoto.lakini yeye alichukulia ni ndodo za kawaida!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom