Wasomi wa sasa huku kwetu (baadhi), hawaamini mambo haya, yaani wanaona kama ni mambo ya kutungwa tu. Ila namna Mungu, alivyo mwema, huwa anajidhihirisha kwao kupitia kuyaruhusu hayo madude yawatese, ndipo hukiri wenyewe baadae, tena kwa machozi haswa. 1Wakorintho 5:1-5
1Timotheo 18-20
Hayo yanatokea sana, tena sana tu, hutaki kuamini sawa, ila yapo na yanaendelea kuwatesa wengi.
Pole kwa huyo dada rafikiyo, ila kwa kuwa chanzo cha tatizo kishajulikana, anaweza kabisa kupata watoto, kwa kuanza kwanza kuyakana na kuyaangamiza yote hayo, pamoja na hao watoto, na itabaki kuwa historia tu.
Kutokuzaa ama kutokushika mimba, ama kutokuolewa, ama nuksi, kuna wakati ni Mungu, mwenyewe anazuia ili utukufu wake udhihirike, na utakapodhihirika atapata mtoto ama watoto.
Tobiti 6:14-18, 7:15-16
Kuna wakati mwanadamu mwenzio anaamua tu akufunge, hasa kwa kutumia nguvu za giza, yakiwemo hayo majini, ila akifunguliwa atapata tu watoto.
Mungu, ni mwema, anasamehe anajali, anahurumia, na haijalishi ni yapi uliyafanya huko nyuma kabla, ila ukirudi kwake Mungu, kikamilifu na kiuaminifu, atakujalia yote hayo.
Ahsante!