Hasheem Thabeet Amwaga Mafedha Bilicanas | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasheem Thabeet Amwaga Mafedha Bilicanas

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Selwa, May 22, 2011.

 1. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  [​IMG]

  [​IMG]


  STAA wa mpira wa kikapu, duniani akicheza katika Ligi ya NBA nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka ‘Super Tall' (pichani) amefanya kufuru ya fedha baada ya kumwaga fedha ukumbini na kuwaacha watu wagombanie, twende mstari kwa mstari.

  Paparazi wa gazeti hili lenye heshima ya nyota tano kwa habari za mastaa Bongo, alishuhudia tukio hilo live wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, jijini Dar es Salaam ambapo handsome boy anayecharaza fimbo katika muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes' alikuwa akipiga shoo babkubwa.

  Awali kasuku wa gazeti hili alimshuhudia Hasheem akikatiza kwa madaha ukumbini humo, akiwa ameongozana na wapambe wake waliokuwa wakimuandalia njia, kisha kukaa sehemu moja na kuanza kula bata kwa mtindo wa ‘tingisha kama imeisha, leta nyingine'.

  Wakati shoo ikiendelea Hasheem aliinuka na wapambe wake kuongoza mbele kama kawa, kisha wakaelekea jukwaani alipochomoa burungutu moja la ‘nyekundu nyekundu' tupu na kumkabidhi Dully Sykes ambaye aliongeza manjonjo baada ya kutuzwa na supastaa huyo.

  Hakuishia hapo, aliposhuka jukwaani, alizama mfukoni na kutoa burungutu lingine kisha akalirusha juu na mashabiki kuanza kugombania.

  Wakati watu wakiendelea kukanyagana wakigombea mkwanja huo wa ‘sadakalawe' Hasheem na wapambe wake walitoka nje na kuingia kwenye gari aina ya Hummer na kuondoka kiwanjani hapo.

  "Duh! Ebwana ee, jamaa huyu ni noma yaani minoti yote hiyo kaiachia watu wanyang'anyane? Hii ni kufuru, kweli mshkaji fedha imemkubali," alisika jamaa mmoja akisema ukumbini hapo.

  Hasheem Thabeet amerejea nchini hivi karibuni akitokea Marekani anapoishi, yupo kwa mapumziko mafupi. Ni Mtanzania pekee anayeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye ligi ya NBA ya mpira wa kikapu nchini humo.


  CHANZO ni Global Publishers: Hasheem Thabeet afanya... - Global Publishers
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  jameni mwacheni atumie hela yake! All the best to him both in his career & katika kula bata!
   
 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wivu wa kishamba hela ni zake do you think what he spend at the club is anything? Just some few peanuts boy...
   
 4. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Like he owes y'all anything?
   
 5. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  He needs to stay focused and remain humble on and off the basketball court, he should not allow any destruction on his way,otherwise he wont last in the game,he should follow the likes Akeem Olajuwon,Dikembe Mutombo etc
   
Loading...