Hasheem Thabeet afanya kufuru, amwaga mamilioni disco! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasheem Thabeet afanya kufuru, amwaga mamilioni disco!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Fareed, May 30, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi nikiwa kama mdau wa viwanja vya starehe vya usiku, nimekuwa nikikutana na supastaa wa Tanzania, Hasheem Thabeet, ambaye anacheza mpira wa kikapu wa kulipwa huko Marekani.
  Wadau wa Arusha wanasema wiki iliyopita Thabeet alikuwa huko siku ya Alhamisi kwenye club inayoitwa Vai Vai. Hapo alionekana akiambatana na crew (wapambe) kibao na kununua vinywaji huku akiwa amezungukwa na vimwana kibao.

  Kali kuliko yote ilitokea hivi karibuni siku ya jumapili ambapo mwanamuziki wa Bongo fleva, Dully Sykes, alikuwa anafanya show Bilicanas jijini Dar.
  Wakati Dully anaimba wimbo wake maarufu wa "Bongo Fleva Naipenda" jukwaani, Thabeet alienda na kumpa bulungutu kubwa la pesa ambalo ni kati ya shilingi laki 5 mpaka sh milioni 1. Baada ya hapo Dully alipata kiwewe cha ghafla na kuacha kupiga shoo kwa muda huku akimwaga misifa kwa Thabeet.

  Thabeet hakuishia hapo, alipanda juu pale Bils na kumwaga mamilioni ya noti chini kwa watu walio kwenye dance floor. Ilibidi watu waache kucheza disco na kuanza kugombania kuokota noti alizokuwa akimwaga. It was raining money...
  Pia alizunguka kwenye meza za watu na kuanza kugawa ofa za vinywaji. Wapambe wake wanasema siku hiyo Thabeet alienda Bureau de change na kubadili dola elfu 15 (sawa na shilingi 22.5 milioni). Mpambe huyo alisikika akisema usiku huo mmoja Thabeet aligawa shilingi milioni 10 hapo Bils.

  Ukiacha Bils, Thabeet pia amekuwa akitembelea viwanja vingine vya dar karibu kila usiku ikiwemo Nyumbani Lounge kwa Lady JD na Mafian kwa Kimbau. Huko amekuwa na tabia ya kuingia nyuma ya counter na ku-serve vinywaji kwa wateja bure yeye mwenyewe na bili yote hulipa yeye. Alionekana akifanya kufuru hizo huku akiwa ameambatana na girlfriend wake, Jokate.

  Pia Thabeet anajulikana kupendelea kwenda Nairobi na wapambe wake na kufanya starehe kubwa. Supastaa huyu akiwa Dar hufikia Kempinski Hotel na kuwaambia wasichana warembo waende kulala naye kwenye hoteli hiyo. Tangu ashushwe daraja kutoka NBA kwenda ligi ya chini, Thabeet amekuwa akionekana mara kwa mara Dar utafikiri hana kazi ya kufanya kule Marekani.
  Wadau wanasema kushushwa kwake daraja kunatokana na kushuka kiwango kwa kukosa discipline (nidhamu) ya mazoezi na work ethic.

  Afisa mmoja wa Benki iliyopo Dar amesema kuwa Thabeet kwa wiki anapokea zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka Marekani na huenda pesa hizo ndiyo zinamchanganya. Ikumbukwe pia kuna siku Thabeet alimpiga mtama mwanamuziki TID nje ya ukumbi wa disco.

  Sijui kwa mwenendo huu kijana huyu atadumu mpaka lini kama professional baller huko Marekani. Namuonea huruma kijana huyu, sijui pesa zake anaziwekeza kwenye miradi ya kumsaidia baadaye au la? Maana kashashushwa daraja. Akishindwa huko pia akafukuzwa hali itakuwa mbaya sana kwake.

  Mama yake, ndugu zake na marafiki zake wanahitaji kumpatia ushauri wa nasaha.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,446
  Likes Received: 19,814
  Trophy Points: 280
  maisha mafupi haya pga pesa kijana:)
  wenye vimdomo najua watakuja kuponda hapa wakati wanavuta bangi badala ya kutafuta timu hasa football
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi ningemshauri Hasheem arudi Texas na kufanya mazoezi ya summer ya kati ya Yao, Olujuwon au Mutambo badala ya kutanua bongo kwa sasa. Ukweli ni kwamba kiwango chake kimeshuka kiasi kwamba timu ya Rockets inafikiria kununua contract yake. Hii ni kwamba wanamlipa pesa ya kumtoa kwenye timu. Hii sio nzuri kwani timu nyingine hazitaweza kumsajili mchezaji wa hivyo. Mimi ninajua Hasheem anao uweza wa kupandisha kiwango chake lakini ni mvivu na anapenda sifa badala ya game. Anaweza kupata pesa nyingi kwa miaka iliyobakia kwenye mkataba lakini ni lazima uelewe kwamba wewe bado ni mdogo na hiyo pesa bila kuwekeza vizuri na makodi ya marekani na ma agent utaishiwa mika 10 ijayo na huwezi kufanya kazi. Achana na marafiki ambao hawakuambii ukweli na tafuta vijana waliotulia kama kaka zako hapa Texas wakushauri bila kujali unawapa nini.
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  I do this when i get ma money doe......
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  If you ain't got no money then you have done somethin wrong
   
 6. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waswahili bwana duuuh, wameshaanza na umbea wao. Kwani akigawa hela wewe inakuuma nini???? au kwa sabaru wewe hazijakufikia.
   
 7. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wabongo mlivyo wanafiki, aki lost hapa mtaanza kuponda sasa hivi anatumia mnasema acheni atumie si za kwake? Najua mshikaji bado ni kijana mdogo sana na hiyo cash ina mzuzua na ukizangatia kwa mtanzania kwa umri kama wake kuwa na fedha nyingi kiasi kile ni nadra sana au naweza kusema yeye ndio wa kwanza..
  Jamani mshaurini vizuri sio kumpa sifa za kijinga na mtanzania mwenzetu
   
 8. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  he's making it rain...
  professional bongo? hamna kitu hapo,
   
 9. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hachukui raundi huyu jamaa,
  misifa ishaanza kumlevya na kumzuzua...
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Sitataka Hasheem Thabeet aishie pale watanzania wengi wanapoishia wakipata hela. Ila kama wadau wengine wanavyosema inabidi atulie afanye mazoezi ili apande kiwango. Tatizo la kuridhika ni ugonjwa unaowapata watanzania wengi na ndo maana umaskini unaongezeka.
  Tulidhani tumepata balozi atakayeiondolea Tanzania aibu katika medani ya michezo ya kimataifa na kuinua bendera yetu juu lakini kwa habari hizi kama ni za kweli basi tumekwisha. Thabeet please geuka hao wapambe wanakuharibia, tulia tafutu meneja mzuri na nenda kwa washauri wakusaidie ili future yako isije kuwa na majuto. Umepewa nafasi na kipawa na Mungu basi usi abuse hiyo fursa mTZ mwenzetu jaribu kuzinduka na kuwa tofauti. Hebu angalia Tyson mahela aliyopata na kwa kuwa alikosa nidhamu ya matumizi basi akafilisika. Elewa hutakwepa kuingia katika mkumbo huo kama hutatafuta watu wenye akili wakupe ushauri pia upunguze kushinda kwenye vilabu vya kipuuzi.
  Kutoa milion 10 kuwagaiwia watu ni kujichora na kujidhalilisha na ni ushahidi kwamba bado uwezo wako wa kudhibiti nguvu ya hela bado ni mdogo. Kwa upande mwingine unatangazia umma kwamba pamoja na kukaa US kwa muda mrefu bado ulimbukeni haujakutoka na kwamba unapelekeshwa na wahuni.

  Piga U-TURN kubwa urudishe heshima bwana mdogo kabla haijawa too late.
  Tunakuombea na tunakutakia mafanikio mema na utuwakilishe vema. Tutajisikia vibaya sana kama utaacha kupokea ushauri mzuri halafu leo na kesho ukarudi bongo ukafilisika baada ya miaka mitano. jifunze kwa akina Mutambo ambao wamejenga vitua vikubwa vya afya huko kwao na kuacha legacy kubwa hata kama leo atastaafu.

  Angalia usiache legacy ya kuzunguka kumbi za starehe NO BODY WILL EVER REMEMBER YOU FOR THAT ila ukafanya kitu tangible cha kimaendeleo basi wewe utakuwa unatumiwa kama mfano wa kuigwa.

  Raise up, make up your mind, think about the future and move forward kiutu uzima acha utoto.
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hasheem mshamba Tanzania ina maeneo kibao kwaajili ya uwekezaji sikuakifilisika atakumbuka misifa ya kijinga.Mwambieni aje Arusha akutane na mifano kibao ya machalii waliokamata fedha za mawe [Tanzanite] wakachezea sasa wamefulia vibaya.
   
 12. njiro

  njiro Senior Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 106
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Guns and Butter. Butter ni matanuzi na Guns ni shughuli inayoingiza pesa. Its better aka-invest for the future. Walikuwepo wanamichezo ambao walikuwa maarufu+hela kushinda hata huyu bwana mdogo leo hii wapo chokest. Ainvest
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Maadam haitokei kwa ndugu yako wewe unaona hiyo ni sawa siyo? hivi angekuwa kaka yako au mdogo wako anagawa fedha bila mpangilio wakati fedha siyo majani useme zitachipua tena ungethubutu kutoa hii comment?
   
 14. L

  Lughe Senior Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  anyway it's your perception ,ila nampa big up jamaa for sharing povertyin Tanzanian na kuzungusha round bar however
  stil can hang out there in Texas or wherever!
  no place for leisure in Bongo.very low class.wasn't even in a list in the leisure centres around the globe.
  somehow Nairobi.
  kwa njaa za njaa bongo caused by f****gv leders u can say kufuru ....na hapa ndiyo muwashangae hao mafisadi wa bongo nini wanafaidi ?

  by the way for advice $100 plus allowance and other opportunities he can invest in
  basketball academy in TZ and stil he do any kind of leisure.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ni hela zake na ana haki na uhuru wa kuzitumia anavyopenda yeye.
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Si basha wako u've to defend him hoe
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  :A S 103:mmmh
   
 18. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,140
  Likes Received: 3,329
  Trophy Points: 280
  Weezy na drake walimwaga $ 250000/= club juz kat,.almost Tshs million 300/=..sio mbaya kwa huyu ngongoti wetu akishow love..kwa kumwaga $ 10k.
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  hapa dogo akiingia na jokate kudadadeki....
  [​IMG]

  shori jokate hapo anauwazia mkwanja tu....
  [​IMG]

  lol kudadadeki later kidogo hasheem na shori wake jokate wakasepa....viti vyao vikiwa na watu wengine....
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  huyu dogo anacheza sana, nadhani huyo Jokate ana mmislid na hiyo mbunye yake lkn bahati haiji mara mbili
   
Loading...