jamii01
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 1,974
- 1,400
Naweza kusema toka January hadi Dec.tutakapomaliza huu mwaka naweza kusema nimeshuhudia harusi za gharama nyingi zaidi tofauti na miaka iliyopita sijui kwa mwakani..hii inamaanisha nini?kwamba sasa hivi harusi si tena kanisani wala msikitini bali ukumbuni..kushindana na kuonyesheana nani zaidi ya mwingine,harusi ya nani ilikuwa bara zaidi ya mwingine..(kuonyeshana mimi ni bora zaidi yako)
Inaamanisha kijana asipokuwa na uwezo wa kutosha au ndugu zake au jamaa zake au rafiki zake basi kuoa kwake itakuwa ni shida na jambo litakalo msumbua sana..kwamba yeye hana uwezo wa kifedha au jamaa zake..hivyo kufanya harusi yake kuonekana dhaifu kulinganisha na wengine..
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa ndoa zilizofugwa kwa ufahari au au zilizotumia gharama kubwa mara nyingi kudumu kwake huwa ni ngumu sana..WEWE HUKO WAPI?
Naomba kuwatia moyo vijana wenzangu ndoa si ukumbini ndoa ni kanisani na pale tu mnabaki kuwa nyinyi wawili hapo ndipo tunapoita ndoa..mengineyo ni michangayo ya watu wa nje..kama watakavyoleta migogoro katika ndoa yenu pia.