Harusi sasa hivi Tanzania kama hujajipanga ni balaaa...

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,969
1,392
Naweza kusema toka January hadi Dec.tutakapomaliza huu mwaka naweza kusema nimeshuhudia harusi za gharama nyingi zaidi tofauti na miaka iliyopita sijui kwa mwakani..hii inamaanisha nini?kwamba sasa hivi harusi si tena kanisani wala msikitini bali ukumbuni..kushindana na kuonyesheana nani zaidi ya mwingine,harusi ya nani ilikuwa bara zaidi ya mwingine..(kuonyeshana mimi ni bora zaidi yako)

Inaamanisha kijana asipokuwa na uwezo wa kutosha au ndugu zake au jamaa zake au rafiki zake basi kuoa kwake itakuwa ni shida na jambo litakalo msumbua sana..kwamba yeye hana uwezo wa kifedha au jamaa zake..hivyo kufanya harusi yake kuonekana dhaifu kulinganisha na wengine..

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa ndoa zilizofugwa kwa ufahari au au zilizotumia gharama kubwa mara nyingi kudumu kwake huwa ni ngumu sana..WEWE HUKO WAPI?

Naomba kuwatia moyo vijana wenzangu ndoa si ukumbini ndoa ni kanisani na pale tu mnabaki kuwa nyinyi wawili hapo ndipo tunapoita ndoa..mengineyo ni michangayo ya watu wa nje..kama watakavyoleta migogoro katika ndoa yenu pia.
 
na hilo ndo linalofanya tuchelewe kuoa maana na hawa mabinti bila harusi nao wanakuwa wanazingua

mara ooh mi kwetu wamesema lazima harusi

hivi si inawezekana kwenda kwa mchungaji mkamalizia mambo ofisini maisha yakaendelea jamani!
 
jamii01 binafsi sina tatizo sana na mtu kufanya harusi ya gharama kubwa, ila kinachonikera ni kuifanya harusi kubwa kwa kutegemea michango ya watu huku ukiwawekea kima cha chini cha kutoa ambacho ni kukubwa ukilinganisha na idadi ya kadi za send off na harusi zilizo mezani kwako.

Nashauri watu wafanye sherehe hizo kwa kuangalia uwezo walionao siyo kushindana kwa kutegemea michango ya watu. Mwishowe michango inaposhindwa kufika bajeti mtu anaingia kwenda kukopa bank kwa ajili ya hurusi ....

Na baada ya hurusi badala ya kuishi maisha ya furaha wanaingia kwenye zoezi la kulipa madeni. Nifikiri tuache kuiga iga na kushindana bila sababu za msingi. Wachangishe watu watoe walichonacho na kufanya sherehe iliyo ndani ya uwezo wako.
 
Harusi yako mwenyewe kuifanikisha tuifanikishe siye...
Huwa wananikera sana watu wanaokaribia kuoa, huwa wanang'ang'ania kama kigando cha mav.i ambacho hakijatawazwa vizuri...
Wengi washazoea vibaya kwa kujishaua eti utasikia "wewe kama ndugu wa karibu unapleji shilingi ngapi?" ukiuliza kwani kima cha chini kiasi gani? unaambiwa laki 2...khaaa kwani kuna mtu anapelewa INDIA kutolewa bone marrow!!
 
Ndoa ni kiapo ambacho wenzi wamekula ili kutimiza ndoto zao, ila huweza kutodumu kutokana na mambo yafuatayo:,
1.Uaminifu kupungua au kuisha kabisa.
2.Umaskini.
3.Kuto toshelezana.
4.Ktokua na upendo wa ndugu kutoka pande zote.
5.Kauli zisizomfaa mmoja kati yao wanandoa .
6.Kutotimiza ahadi mlizo ahaidiana.
 
watu wanapenda waonekane kwenye kipindi cha bango, harusi zao ziwe gumzo mtaani by any means
 
mmh, kazi ipo
ukute wengine wanapitisha michango na mtu keshazaa, na wanaishi pamoja.
Mie huwa sichangi ng'o
 
Harusi yako mwenyewe kuifanikisha tuifanikishe siye...
Huwa wananikera sana watu wanaokaribia kuoa, huwa wanang'ang'ania kama kigando cha mav.i ambacho hakijatawazwa vizuri...
Wengi washazoea vibaya kwa kujishaua eti utasikia "wewe kama ndugu wa karibu unapleji shilingi ngapi?" ukiuliza kwani kima cha chini kiasi gani? unaambiwa laki 2...khaaa kwani kuna mtu anapelewa INDIA kutolewa bone marrow!!

umeoa kaka, najitolea kua mwenyekiti wa kamati if bado maana haitakua pasua kichwa kima cha chini
 
dada eleweni watu wenu,si mnasema mna uhuru,sasa iweje wazazi wako wawe mwiba eti bila ndoa tena ya gharama hauolewi?
 
Bada ya kanisani sambaa mbele mimi huwa nashangaa sana mtu anatumia mil35 just for a single day kesho yake anaenda kulala nymba ya kupanga!!
 
Harusi zinaonekana ni gharama kwa sababu watu wanazifanya hizi kwakuangalia watu wengine!

Unakuta watu wana ng'ang'ania harusi za gharama wakati huwezo hakuna!

Inashangaza kuona watu wanafanya harusi za gharama alaf baada ya harusi maisha ya tabu na shida!

Mi naona ni vyema kufanya kitu ndani ya uwezo wako kuliko kusumbua na kukimbizana na watu!
 
Harusi yako mwenyewe kuifanikisha tuifanikishe siye...
Huwa wananikera sana watu wanaokaribia kuoa, huwa wanang'ang'ania kama kigando cha mav.i ambacho hakijatawazwa vizuri...
Wengi washazoea vibaya kwa kujishaua eti utasikia "wewe kama ndugu wa karibu unapleji shilingi ngapi?" ukiuliza kwani kima cha chini kiasi gani? unaambiwa laki 2...khaaa kwani kuna mtu anapelewa INDIA kutolewa bone marrow!!

..ulichosema kweli kabisa, unakuta sendoff/harusi budget milioni 15-20 halafu.zote zinategemea mifuko.ya watu....walahiiiii inakera kweli...wanadai kama walikukopesha wakati ni hiari kuchangia
 
Harusi zinaonekana ni gharama kwa sababu watu wanazifanya hizi kwakuangalia watu wengine!

Unakuta watu wana ng'ang'ania harusi za gharama wakati huwezo hakuna!

Inashangaza kuona watu wanafanya harusi za gharama alaf baada ya harusi maisha ya tabu na shida!

Mi naona ni vyema kufanya kitu ndani ya uwezo wako kuliko kusumbua na kukimbizana na watu!
Harusi yangu ilikuwa mimi mume na judge baada ya hapo fireworks na wine .tukawatumia barua wazazi tumeoana.mama angu na ukatibu wote jasho lilimtoka.oh kwa nini umefanya hivyo oh ningekufanyia harusi ili watu wanione akanipa zawadi ya mjumba basi .I believe wedding is a waste of money pesa zote nipe mkononi nikafanye shopping
 
umeoa kaka, najitolea kua mwenyekiti wa kamati if bado maana haitakua pasua kichwa kima cha chini

hahaha hata usipate shida, harusi yangu itakua very casual lakini watu watafurahi...kwangu harusi ni shughuli ya kifamilia zaidi
 
..ulichosema kweli kabisa, unakuta sendoff/harusi budget milioni 15-20 halafu.zote zinategemea mifuko.ya watu....walahiiiii inakera kweli...wanadai kama walikukopesha wakati ni hiari kuchangia

BT, mie miezi hii mitatu ya kufunga mwaka nimechangia harusi mpaka nimekoma...halafu watu wengine wakikuoma waendesha gari, wavaa vizuri basi unaletewa pleji kabisa hehehe...
 
Ina maana hata wewe haukufanya bonge la harusi!

Lakini tatizo letu wabongo tunapenda harusi za gharama na huwezo hakuna, yani mtu ana tegemea michango hili avunje rekodi baada ya hapo hata pa kulala ni shida!

Harusi za kuangalia watu watasemaje zina waumiza wengi sana!

Harusi yangu ilikuwa mimi mume na judge baada ya hapo fireworks na wine .tukawatumia barua wazazi tumeoana.mama angu na ukatibu wote jasho lilimtoka.oh kwa nini umefanya hivyo oh ningekufanyia harusi ili watu wanione akanipa zawadi ya mjumba basi .I believe wedding is a waste of money pesa zote nipe mkononi nikafanye shopping
 
Huu ni ugonjwa wa watanzania wengi, kupenda sifa na kujionesha wakati huwezo hakuna! Yan baada ya harusi unashangaa watu wanaishi kwa tabu!

Baada ya kuchangia elimu tunachangia starehe!

..ulichosema kweli kabisa, unakuta sendoff/harusi budget milioni 15-20 halafu.zote zinategemea mifuko.ya watu....walahiiiii inakera kweli...wanadai kama walikukopesha wakati ni hiari kuchangia
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom