Dhambi ni mtazamo.

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Kama kichwa cha habari kinavyosema, binafsi naona suala la dhambi ni mtazamo na sio kitu universal standard. Dhambi ni uasi na uasi ni kwenda tofauti na sheria.Na kinyume cha uasi ni UTII.

Embu tuangalie mfano wa kabila la banyankole nchini 🇺🇬 Uganda.
Banyankole wanakitu kinaitwa (potency test) kwa maana ya majaribio ya uwezo wa mwanaume kusimamisha uume.

Hili linafanyika vipi?
Nchini Uganda kuna kabila la banyankole, Mara nyingi ndoa huonekana kama mzigo usiofikirika haswa kwa mashangazi wa bibi harusi, kwenye kabila hili nchini Uganda shangazi wa bibi harusi anatakiwa kufanya majaribio na bwana harusi ili kupima uwezo wake kwa kufanya nae mapenzi.

Shangazi ndio huridhia, pia shangazi anapaswa kucheki bikira ya bibi harusi. Hii kwao ni jambo la heshima,kwenda kinyume na jambo hili ni dhambi kwao.

Dini zinatazama vipi kuhusu hili? Kwenye upande wa dini ndoa ni baina ya watu wawili (wakristo) na Mke zaidi ya mmoja(waislamu) kwa maana shangazi hatakiwi hapa kufanya mapenzi na bwana harusi na pia atakiwi kwenda kupima bikira ya bibi harusi.

Isipokuwa tu kuna baadhi ya dhambi ni standard universal kama usiue.

Nikienda umasaani kabla ya kumuamkia mzee masaai warriors wanatemea mate mikono Yao kabla ya kusalimiana na wazee hio ni heshima. Atakutafsiri vipi raisi au bosi wako uteme mate mkononi halafu umpe mkono? Ataona huu ni uasi na ni dharau.

Una mtazamo gani kuhusu hili?
 
Kweli kabisa dhambi ni mtazamo Tu, wa jamii husika kutokana na tamaduni zao.

Mfano Roman Catholic Church wanakataza ndoa za wake wengi wanasema ni unyanyasaji wa kijinsia Kwa mwanamke,

Lakini wanakubali ndoa za jinsia moja.
Huku Afrika 👆 wakisema ni kinyuma na maadili za Ki Afrika
 
Dhambi ni mtazamo wa watu wa jamii fulani ,hapo bado zunguka sana utashangaa mengi sana .

Kikubwa kila mtu ana lake ukienda India kule baadhi ya makabila na mila hawali ng'ombe kwao ni haramu kabisa ..

Kila mtu aishi chini ya mfumo wake anaoamini.
 
Wakuu habari za uzima?

Kama kichwa cha habari kinavyosema, binafsi naona suala la dhambi ni mtazamo na sio kitu universal standard. Dhambi ni uasi na uasi ni kwenda tofauti na sheria.Na kinyume cha uasi ni UTII.

Embu tuangalie mfano wa kabila la banyankole nchini Uganda.
Banyankole wanakitu kinaitwa (potency test) kwa maana ya majaribio ya uwezo wa mwanaume kusimamisha uume.

Hili linafanyika vipi?
Nchini Uganda kuna kabila la banyankole, Mara nyingi ndoa huonekana kama mzigo usiofikirika haswa kwa mashangazi wa bibi harusi, kwenye kabila hili nchini Uganda shangazi wa bibi harusi anatakiwa kufanya majaribio na bwana harusi ili kupima uwezo wake kwa kufanya nae mapenzi.

Shangazi ndio huridhia, pia shangazi anapaswa kucheki bikira ya bibi harusi. Hii kwao ni jambo la heshima,kwenda kinyume na jambo hili ni dhambi kwao.

Dini zinatazama vipi kuhusu hili? Kwenye upande wa dini ndoa ni baina ya watu wawili (wakristo) na Mke zaidi ya mmoja(waislamu) kwa maana shangazi hatakiwi hapa kufanya mapenzi na bwana harusi na pia atakiwi kwenda kupima bikira ya bibi harusi.

Isipokuwa tu kuna baadhi ya dhambi ni standard universal kama usiue.

Nikienda umasaani kabla ya kumuamkia mzee masaai warriors wanatemea mate mikono Yao kabla ya kusalimiana na wazee hio ni heshima. Atakutafsiri vipi raisi au bosi wako uteme mate mkononi halafu umpe mkono? Ataona huu ni uasi na ni dharau.

Una mtazamo gani kuhusu hili?

Ndugu, kila mfumo wa maisha huongozwa na utaratibu wake na sio mtazamo kama unavyotanabaisha. Ukishaita “Dhambi” moja kwa moja unaingia katika dini na maana ya Dhambi katika dini ni uasi wa Mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu.

Dhambi sio mtazamo kwasababu ili ujue hii ni dhambi na hii sio dhambi, lazima urejee kwenye vitabu vitakatifu kupata muongozo. Haijalishi kabila gani linafanya nini as long as Maandiko yameshasema ni dhambi, hiyo ni Dhambi katika mfumo wa maisha ya kidini

Lakini tukirudi kwenye mfumo wa maisha ya kawaida tuna “Morals” kuna “good morals” na kuna “bad morals” Hapa ndipo jamii zinaweza kutofautiana kulingana na taratibu za tamaduni zao. Mathalani, kuna makabila ndugu wanaweza kujamiiana lakini kuna makabila ndugu hawapaswi kujamiiana.

Hivyo, Dhambi sio mtazamo. Ni suala la kuyajua maandiko matakatifu ili kubaini lipi ni dhambi na lipi sio dhambi. Na kama mtu sio muumini wa dini basi hawezi kuzungumza lolote kuhusu dhambi. Lakini hilo halimfanyi akwepe hukumu ya dhambi.
 
Dhambi ni mtazamo wa watu wa jamii fulani ,hapo bado zunguka sana utashangaa mengi sana .

Kikubwa kila mtu ana lake ukienda India kule baadhi ya makabila na mila hawali ng'ombe kwao ni haramu kabisa ..

Kila mtu aishi chini ya mfumo wake anaoamini.

Dhambi sio mtazamo. Mtazamo upo kwenye taratibu za kijamii ila Dhambi ni Dhambi katika mfumo wa kidini. Biblia ikisema usiue, Muumini yoyote wa Kikristo awapo popote pale hapaswi kuua. Huwezi ukawa mkristo kisha ukasema kwa mtazamo wangu kuua sio dhambi.

HAKUNA MTAZAMO BINAFSI KATIKA DHAMBI.
 
Ndugu, kila mfumo wa maisha huongozwa na utaratibu wake na sio mtazamo kama unavyotanabaisha. Ukishaita “Dhambi” moja kwa moja unaingia katika dini na maana ya Dhambi katika dini ni uasi wa Mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu.

Dhambi sio mtazamo kwasababu ili ujue hii ni dhambi na hii sio dhambi, lazima urejee kwenye vitabu vitakatifu kupata muongozo. Haijalishi kabila gani linafanya nini as long as Maandiko yameshasema ni dhambi, hiyo ni Dhambi katika mfumo wa maisha ya kidini

Lakini tukirudi kwenye mfumo wa maisha ya kawaida tuna “Morals” kuna “good morals” na kuna “bad morals” Hapa ndipo jamii zinaweza kutofautiana kulingana na taratibu za tamaduni zao. Mathalani, kuna makabila ndugu wanaweza kujamiiana lakini kuna makabila ndugu hawapaswi kujamiiana.

Hivyo, Dhambi sio mtazamo. Ni suala la kuyajua maandiko matakatifu ili kubaini lipi ni dhambi na lipi sio dhambi. Na kama mtu sio muumini wa dini basi hawezi kuzungumza lolote kuhusu dhambi. Lakini hilo halimfanyi akwepe hukumu ya dhambi.
Umenena vyema sana.

Ila umetazama upande wa divine law.

Na sin inaweza zungumziwa hata upande wa philosophy.

Point inabaki pale pale itabaki kuwa ni mtazamo.
Sababu hakuna universal standard moja. Ipo sin in context of religion ipo sin in context of philosophy.
 
Ni kama msafwa kunywa pombe ni jambo jema na utamaduni unaopendwa. Ukienda na dini zako eti unawakataza waswafwa wasinywe pombe hutapata muumini hata mmoja.
Mswafwa na Mbena pombe kwao ni ibada sasa wewe ibada zako za kizungu ukitaka wazitimize kwa 100% unafeli hivyo wahubirie tu wanayoweza kuacha mfano usiibe.
Ni kama kwetu kigoma UCHAWI ni kama utamaduni unaopendwa na kuambatana na dini za leo. Eti umwambie mtu wa Kigoma UCHAWI ni dhambi watakuona kama unaumwa akili uliechanganyikiwa.
Pamoja na kupokea hizo dini mwafrika hajakubali kuuacha utamaduni wake kwa 100% japi kuna waafrika wvibaraka wa wageni wanajaribu kutaka tutekekeze dini kama hao wageni..
 
Dhambi sio mtazamo. Mtazamo upo kwenye taratibu za kijamii ila Dhambi ni Dhambi katika mfumo wa kidini. Biblia ikisema usiue, Muumini yoyote wa Kikristo awapo popote pale hapaswi kuua. Huwezi ukawa mkristo kisha ukasema kwa mtazamo wangu kuua sio dhambi.

HAKUNA MTAZAMO BINAFSI KATIKA DHAMBI.

Kwenye biblia zipo adhabu za uzinzi kwamba wapigwe mawe mpaka kufa, maana hio ni dhambi.

Narudi kwako ni nani alishawahi kuhukumiwa mahakamani kwa dhambi ya uzinzi hapa Tanzania?
 
Ndugu, kila mfumo wa maisha huongozwa na utaratibu wake na sio mtazamo kama unavyotanabaisha. Ukishaita “Dhambi” moja kwa moja unaingia katika dini na maana ya Dhambi katika dini ni uasi wa Mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu.

Dhambi sio mtazamo kwasababu ili ujue hii ni dhambi na hii sio dhambi, lazima urejee kwenye vitabu vitakatifu kupata muongozo. Haijalishi kabila gani linafanya nini as long as Maandiko yameshasema ni dhambi, hiyo ni Dhambi katika mfumo wa maisha ya kidini

Lakini tukirudi kwenye mfumo wa maisha ya kawaida tuna “Morals” kuna “good morals” na kuna “bad morals” Hapa ndipo jamii zinaweza kutofautiana kulingana na taratibu za tamaduni zao. Mathalani, kuna makabila ndugu wanaweza kujamiiana lakini kuna makabila ndugu hawapaswi kujamiiana.

Hivyo, Dhambi sio mtazamo. Ni suala la kuyajua maandiko matakatifu ili kubaini lipi ni dhambi na lipi sio dhambi. Na kama mtu sio muumini wa dini basi hawezi kuzungumza lolote kuhusu dhambi. Lakini hilo halimfanyi akwepe hukumu ya dhambi.
Vitabu vitakatifu ni vitabu gani na utakatifu wake umehalalishwa vip?
 
Dhambi ni mtazamo Kuna vitu sehemu Moja sio kosa sehemu nyingine ni kosa.....mm mpaka nakufa huwezi niambia kulala na mdada ni dhambi kikubwa nisiwe nimemshurutisha, nimemlaghai kivyovyote au nimetumia advantage ya changamoto yake kumdinya!
😂😂Wanadai bila kwenda kanisani kuvaa suti na shera hio ni dhambi
 
Back
Top Bottom