NAFIKIRI itakuwa kama hivi:
1. Kumbi zote za sherehe zisajiliwe.
2. Wamiliki wa kumbi sharti mwanzo mwezi wawasilishe TRA list ya sherehe zote zinazotarajiwa kufanyika ndani ya mwezi huo.
3. Sherehe yoyote itakayofanyika kwenye ukumbi usiozidi sh. 700,000/= hakuna kodi.
4. Ukumbi wa sh. 700,001/= au zaidi kodi 100% ya bei ya ukumbi au 18% ya budget ya sherehe, whichever is higher.
5. Maafisa wa TRA kutinga ukumbini kabla ya sherehe kuanza na waandaji waonyeshe vifuatavyo kwa uhakiki:
a. EFD ya ukumbi
b. EFD ya Caterer
c. EFD ya Vinywaji
d. EFD ya MC
e. EFD ya Mpambaji
f. EFD ya mpiga picha
g. EFD ya gari za kukodi
i. EFD ya saloon
n.k
Mnaonaje hapo? Bila shaka meanza kupapenda
Mfano:
Bajeti sh. 20,000,000/=
Ukumbi sh. 2,500,000/=
Kodi:
(a) 18% = 3,600,000/= au ukijitahidi kudanganya kuhusu bajeti, unaenda kwenye (b)
(b) 100% ya Hall = 2,500,000/= au ukijifunza kuacha makuu, utafuta ukumbi wa 1,500,000/=, unahamia (c)
(c) 100% ya Hall = 1,500,000/=
Teh tehe, serkali haijatoka kapa