Jumamosi hii nimehudhuria ibada ya ndoa iliyokuwa inafungwa katika kanisa moja hapa Jijini Dar-Es-Salaamu.
Ibada ilienda na ukafika wakati bwana arusi akaambiwa na kasisi kufunua kipande cha shela kinachofunika uso wa bi arusi, kama ishara ya maharusi kuunganishwa rasmi.
Mara baada ya Bi Arusi kufunuliwa uso na kuangaliana uso kwa uso kwa mwenzi wake (Bwana arusi), kilichofuata ni bibie huyo kububujikwa na machozi kwa, maana ya kulia, yasiyokifani kwa takribani dk 5.
Badae ibada ikaendelea.
Akiendelea na mahubiri Kasisi alikiita kitendo kile cha kutokwa na machozi cha bi arusi, kama ishara ya usafi, uadilifu, malezi na makuzi mema, ambayo binti amekua nayo katika kipindi cha maisha yake.
Aidha aliendelea kuwa enzi hizi ndoa nyingi ni kama maonesho au fashion ndio maana imekuwa kawaida kuona ndoa inafungwa na bibi arusi ni mjamzito, bibi arusi kuingia madhabahuni na nguo za aibu akiwa nusu uchi, ndoa nyingi kutodumu maana upendo wa Ki-Mungu haupo tena bali upendo wa vitu na unafki na kadhalika.
Nadhani lipo zuri la kutafakari hapo!