Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye 'headline' mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa hastaili kuwa mwanamuziki.
Alianza kama utani hivi kwa kufananishwa na mkali wa lebo ya WCB then mdogo mdogo anaanza kupenya kwenye masikio ya wapenda burudani.
Hapa Tunamzungumzia HarmoRapa Jamaa anatabiriwa kufanya makubwa kwenye mziki wa bongo fleva Time hii hapa. Single yake ya kwanza usigawe pasi ndiyo iliyomuweka kwenye ramani na kuanza kujulikana japo haikufanya vizuri sokoni.
This Time around HarmoRapa amekuja na another hit in Town goes by the name “Kiboko ya Mabishoo” wengi walidhani kama ni Jokes lakini Jamaa amekuwa serious sasa baada ya kusaini deal na kampuni kubwa ya upigaji picha na teknolojia bongo Slides Visual chini ya Mx Carter.
Jamaa kwa kasi hii anatabiriwa kusumbua kwenye game wasanii waliopo hawatakiwi kubweteka na kasi hii ya ukuaji wa ajabu na wanatakiwa wamuangalie zaidi sababu yupo chini ya menejimenti nzuri inayofanya promotion ya uhakika kuendana na soko la sasa.
kupitia mitandao ya kijamii Facebook, Twitter na Instagram jina la Harmorappa limezungumzwa Mara nyingi na Story zake zikifuatiliwa kwa wingi na wapenzi wa burudani Bongo.