Harmonize, Huo ni Ushamba

SEASON 5

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
481
1,000
Huu wimbo mpya wa harmonize kama jinsi alivyouita mimi nimeupenda kwa u comedy wake lakini siuiti wimbo kwangu ni kichekesho na wala si wimbo lakini zaidi kitendo chakumchukua kijana anaefanana na diamond na kumuweka kwenye video Huo ni ushamba mkubwa kwenye hii video.

Wasanii idea za video na nyimbo wanazotunga huwa wanawaza wapi ndugu zanguni? mbona kama wote wapo mule mule kwenye bahari 1 ya mawazo mtu ninaemuona anaogelea kimawazo bahari tofauti na wenzake ni diamond,ila hizi idea za namna hii kweli unasema ni msanii kaimba hiki kituko?

Hamonize huo ni ushamba narudia tena kumuweka diamond feki kwenye wimbo wako kumekurudisha hatua 100 nyuma,matokeo yake hutoyaona sasa hivi subiri mwenzako atoe kitu ndio utajua hasira za mashabiki zake.

moja ya nyimbo mbovu kuwahi tungwa na huyu mmakonde ni hii HUO NI USHAMBA.
 
Back
Top Bottom