Hili ni jambo la kiimani zaidi, hivyo kila mtu na aminicho..
Kwangu iko hivi, kwa mungu kuna neema tofauti, yaani neema za dunia(naita neema ndogo ndogo) mfano kupata mali, kupumua, uzima wa afya, watoto n.k n.k, kuna neema kubwa hii ndio kuingia peponi, hii ndio neema kubwa kabisa.
Mungu kila kitu katuumbia ni mtihani, mali watoto, na mazaga zaga yoote ni mtihani,hata ufukara ni mtihani pia,mpaka tamaa za kimwili ni mtihani, vyoote hivyo katupa halafu katuwekea namna ya kuviendea, mathalani, kukwichi kwichi, ametuamuru tuoe na tusizini, tukizii tumefeli, mali katupa katuelekeza jinsi ya kuzitumia(mf. Kusaidia yatima, maskini,wajane, wapita njia n.k)
Kama kila jambo ni mtihani, basi kwenye kila mtihani kuna kufaulu na kufeli, je nikifeli inakuwaje na nikifaulu inakuwaje, ndio hapo kaumba moto na pepo wanaofeli wataingia motoni na wanaofaulu pepono ambayo hii ndio neema kubwa kabisa kuliko neema zoote.
Anaepewa mali na kunyimwa mali wote ni wapo katika mawili afaulu(ashukuru) ama afeli(akufuru).
Tajiri anaetumia mali zake kiuadilifu vile mungu inampendeza huyo kafaulu, vingimevyo kafeli akifeli motoni akifauulu nfio anapata neema kubwa kabisa ya pepo, hivyo hivyo maskini, akiridhika na umaskini wake akaona mungu ndio mpaji akitaka kumpa atampa, na akaacha kukufuru kuwa mungu anamuonea, akatenda mambo mola anayapenda(akafaulu) nasi nae atapata meema kubwa kabisa ya pepo
Mungu sijaona sehemu kasema niabuduni niwape mali, ila kasema nitaweneemesha na neema za mungu ni kama nilizoorodhesha na anatoa kadri apendavyo, kuwa mzima wa afya tu ni neema kubwa mnooo, kuna wachamungu wanapewa mali, kuna wachamungu masikini, kuna mabaradhuli wanapewa mali na kuna mabaradhuli maskini... Shida ni sisi wanadamu kuona neema ni mali tu, la hasha hilo si kweli.. neema ni nyingi.
Malipo ya mungu ni makubwa mnoo, watu hatuelewi kuna vitu vinatusumbua, mfano umenikuta njiani naumwa, ukanichukua ukanipelela hospitali, unauwezo wa kunighamikia, ukafanya hivyo, siku ya siku tukakosana nikakutukana, we fala tu, huna lolote kimeemda kimerudi!? Je malipo yako kwa mungu hayapo!? Au kwa wema ulionitendea nami nikakutendea wema je, mungu hakulipi tena, la hasha malipo ya mungu costant, mtu atalipwa kwa kile alichotenda, umenitendea wema nimekufanyia ubaya, wema wako utalipwa,umenitendea wema nikakutendea wema, bado wema wako utalipwa tu.
Ndio ufukara na utajiri.. uwe maskini uwe tajiri, kizuri ni kufayanya mema tu. Kila mtu ataulizwa neema aliyopewa aliitumia vipi!? Kimbembe kitakuwepo hapo kudadeki.
Ni jambo refu kidogo, niishie hapa.