Katika siasa, hasa hapa Tanzania, mwanasiasa anahitaji kuwa anazungumziwa ktk vyombo vya habari vingi iwenavyo. Kitu muhimu ni kwamba mwanasiasa huyo awe anazungumzia matatizo ya wananchi na apendekeze utatuzi unaokubalika.
Kwa upande wa CHADEMA, ni dhahiri kwamba sehemu nyingi nchini Tanzania, ktk miezi ya karibuni, wanakubalika sana. Ndiyo sababu hata WanaCCM wengi wanajivua magamba na kuomba kadi za CHADEMA. "Peoples Power" na "Hakuna Kulala. Mpaka Kieleweke!" vimekuwa ni kauli mbiu za kitaifa sasa.
Kwa hiyo sioni tatizo hilo unalolizungumzia. On the contrary, Watanzania wengi wanawajua na kuwapenda wanaCDM waliotajwa: kwa umakini wao, uzalendo wao, na jinsi wanavyojieleza ktk kutatua matatizo ya nchi yetu.
Sisemi hapa kwamba tatizo la Dr Slaa na Mama Kamili sio la maana. Hata Mh. Mnyika pia ana jambo la kujieleza. Lakini kwa ujumla, hawa ni wanasiasa safi, na Watanzania wengi wana matumaini kutokana na jinsi wote hawa pamoja na kundi lote la viongozi wa CDM wanavyojituma kuleta suluhu ktk matatizo ya nchi yetu.
Kwa hiyo sioni "Hard times for CHADEMA". On the contrary nasema Uzi ni huo huo kwa uongozi wa CDM!!!