Kweli ndugu yangu nimeona na nimestaajabu sana kuona wanakuchafua. Sema ndio hivyo huenda wamekalili
Hata kipindi kile nimeandika barua ya wazi kukuhusu. Walihisi kama ni wewe umejiandikia. Ila kumbe ni mimi mwenyewe niliamua kuwa muwazi na kukuandikia ujumbe ule.
Sisi acha tuwaache waamini wanavyoamini ila ni ukweli usiofichika kuwa wewe ni miongoni mwa wale members maarufu na wanaokubalika na watu humu ndani.
Kuna watu wanachukia misimamo yako na jinsi unavyojenga hoja na kuwapopoa ila wanafurahia hoja zako na wanapenda kukuona humu ndani kila siku.
Mkuu usiwajali. Ila nikuombe tu wakiingia anga zako wapopoe bila kusita


. Huwezi kutenganisha upopoaji na jina lako. Mtu akiiona ID yako tu cha kwanza lazima asome comment yako kwa makini ili kujua style ya upopoaji uliyokuja nayo siku hiyo.
Humu ndani kuna baadhi ya watu wamejijengea identity zao na umaarufu wao...Maswala ya ulozi na uganga tunamuachia MSHANA JR....Maswala ya siasa tunamuachia JOHNTHEBAPTIST....Maswala ya Udaku ilikuwa Identity ya WARUMI (R.I.P).....wewe identity yako ni kusimamia unachokiamini na kupopoa mapopoma wote...
Kiufupi mkuu wanakuchukia wakikuona ila wanakumiss usipoonekana....huo ndio ukweli.
Sema mkuu wangu kidogo jaribu kupunguza kuwapopoa wale wanaokuja na hoja kupinga hoja zako. Maana yake kuna muda hutaki kabisa kupingwa



.
Basi mkuu....usinipopoe