Kwa niaba ya wapwa na mabinamu zangu, na
Kwa niaba ya mababu wenzangu wote, na
Kwa niaba ya wajukuu zangu wote, watukutu, mtiifu, spesho,mwema, wapya na wakongwe, na
Kwa niaba ya hommies zangu wote
Kwa niaba ya wanachama wote na uongozi wa ISC,na
Kwa niaba ya wanywaji na wachangiaji wakuu wa pato la Serikali ya JMT, na
Kwa niaba ya mashabiki, wanachama, wapenzi na wachezaji wa Simba SC na Liverpool FC, na
Kwaniaba ya MODS wenzangu wa majukwaa yote, na
Kwaniaba ya mashemeji zangu wote, wakiongozwa na my darling shemeji, na
Kwa niaba ya soulmate wangu...
Mimi ODM kwa mamlaka niliyopewa na kujipa mwenyewe...... Nakutaarifu kuwa watu wote hao hapo juu wanakutakia Heri ya Siku yako ya kuzaliwa.
Kumbuka: Kadiri mwaka unavyoongezeka ndivyo unavyopiga hatua moja kulisogelea kaburi. Mkumbuke Mungu wako na Mshukuru kwa mema yote aliyokutendea.......... Tazama, leo umetimiza miaka hii, wakati kuna uliowatangulia kuliona jua hivi sasa wamefunikwa na tani takribani saba ya dongo zito, katili na lisilo na huruma.
Nakuombea uishi miaka mingi zaidi, uzae watoto wengi waizunguke meza yako wakati wa chakula. Wale wasishibe ili upate maarifa ya kuhangaika kwa ajili yao zaidi na zaidi kama ambavyo wazazi wako walikuhangaikia.
Ukikutana na mama yako, naomba umpigie makofi matatu kwa niaba yangu.
Ubarikiwe sana.