Swahiba na rafiki wangu wa ukweli
Roulette,
Najua nimechelewa kukutakia heri ya siku yako ya kuzaliwa.
Najua unajua kuwa halikuwa kusudio langu
Najua wajua kuwa nakupenda na kukuheshimu sana
Najua unafahamu kuwa we ni mtu muhimu sana ktk maisha yangu
Najua unajijua we ni mkarimu, mpole na mwenye moyo wa utu
Najua unajua kuwa maombi yangu kwa Mungu huwa yanasikilizwa
Ndio maana namwomba Mwenyezi Mungu mwenye rehema
Akujalie afya njema,
Akuepushe na mikosi, balaa na bahati mbaya
Akupe bahati nzuri daima
Akuepushe na hatari zote
Akuongezee siku za kuishi kwako huku akikuepusha na dhambi
Akupe umri uwaone wajukuu wa wajukuu zako ili siku atakapokuita kwake mbinguni wajukuu zako wasilie bali wamshukuru Mungu kwa kuwapa bibi mwema.
Hongera na heri ya siku yako ya kuzaliwa mpendwa
Roulette
Ni mimi ODM wako nimekuombea
Itikia AMINA