Happy Birthday Raia Mwema

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Siku kama ya leo, Jumatano ya Oktoba 30, 2007, gazeti la Raia Mwema lilianzishwa na kuingia sokoni, leo ni siku maalumu kwao na kwetu wana JF maana wamekua na mchango mkubwa katika mijadala yetu humu ndani. Nawapongeza na kuwatakia kila la kheir katika mapambano ya demokrasia ya kweli Tanzania. Ikiwa ni miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, Raia Mwema litusaidie kupata uhuru wa kweli wa kifikra kwa Watanzania wote.
 
Tunaomba tamko kuhusu tetesi kwamba mmenunuliwa na Magamba.Siku hizi hata mauzo yamepungua.Kuna mtani wangu humu jamvini siku moja aliwalinganisha na Jambo Leo.Kama mna masikio na msikie!
 
Raia Mwema wako mbioni kuwapita Mwanahalisi. Na kama Jenerali Ulimwengu atakuwa macho basi sina shaka atafanikiwa kuwa na sauti ya kuaminika kwenye hii media industry yetu. Tayari alishaonja 'maujanja' ya mjini kupitia kwa swaiba wake wa zamani Salva hivyo nategemea atakuwa makini. Mwanahilisi inabadilisha 'tune' siku hizi na kuna ka-harufu ka-kimtandao.
 
Tunaomba tamko kuhusu tetesi kwamba mmenunuliwa na Magamba.Siku hizi hata mauzo yamepungua.Kuna mtani wangu humu jamvini siku moja aliwalinganisha na Jambo Leo.Kama mna masikio na msikie!

Ada ya mja hunena, Muungwana ni Vitendo.
 
Mbona mnasherekea birthday mkiwa hampo hewani kwenye website? Au ndo maana ya birthday?
Tupe pumzi jamani au tuchange malipo ya webmaster?
 
Nani mhariri mkuu au linamilikiwa na nani? Wengine tuko Alaska.
 
Mbona mnasherekea birthday mkiwa hampo hewani kwenye website? Au ndo maana ya birthday?
Tupe pumzi jamani au tuchange malipo ya webmaster?

Hahaa!! Kweli hawapo hewani ila kwa kweli inasikitikisha sana, mara ya mwisho kwenye twitter ilielezwa kwamba kuna tatizo la kiufundi, naamini wiki iinayoanza kesho mambo yatakua hewani yakiwa bora zaidi
 
Back
Top Bottom