It is 1st June....
Special day for
ICHANA
Its her birthday
ICHANA sina maneno mengi ya kuandika juu yako ila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kwako. Mshukuru MUNGU wako maana ni kwa rehema na neema zake tu ndio maana leo unasherehekea siku hii muhimu kwako. Jaribu kufikiria ni ndugu na marafiki wangapi umewapoteza mpaka kufikia leo. Tafakari piga magoti mshukuru MUNGU na la muhimu jitahidi kutenda yaliyo mema zaidi na zaidi.
ICHANA washukuru sana wazazi wako kwa malezi waliyokupa hadi leo. Kumbuka kuna watoto wengi wanakosa malezi ya wazazi wao na kuishia kuharibikiwa maisha yao lakini wewe umepata rehema ya kukua mikononi mwa wazazi.
ICHANA sema pia asante kwa ndugu na marafiki zako kwa sapoti wanayokupa kila siku maishani, kumbuka hii ni dunia na kamwe huwezi kuishi peke yako hata uwe maskini au tajiri kiasi gani.
Mwisho
ICHANA tunajifunza kupitia makosa yetu maishani, na wewe jifunze katika makosa yako ili sasa unapoanza mwaka mwingine upige hatua mpya ukiwa na matumaini na furaha kuu maishani mwako.
Kumbuka maneno yako haya "
Nitaimba kwa sauti kuu ya kumshukuru MUNGU".
Jamani tumtakie heri ya kuzaliwa mwenzetu ICHANA
Copy to: sungura1980, miss neddy, Kaizer, DEMBA, christine ibrahimu, miss chagga, The Boss, Invisible, Mtambuzi, watu8, Miss Bantu, lara1, ladyfurahia, amu, Kunta Kinte, Dinazarde, Asprin, Mashaxizo, Rocky, Mndengereko, utafiti, uran, Mentor, Nyani Ngabu, evelyne Salt, Mamndenyi na wengineo wooote