Hapo Mwanzo Palikuwa Na Nini?!...science Vs divinity

Tafadhali kama kuna mtu yeyote asiyemwamini mungu kabisa naomba kufahamu kuwa msimamo wako ni nini.
Niko tayari kusoma maelezo yako kwa unyenyekevu mkubwa.
 
Tafadhali kama kuna mtu yeyote asiyemwamini mungu kabisa naomba kufahamu kuwa msimamo wako ni nini.
Niko tayari kusoma maelezo yako kwa unyenyekevu mkubwa.

Kuamini kwamba mungu yupo ni suala jingine na kumwamini mungu ni suala jingine. Mtu anaweza kuamini kuna mungu lakini asimwamini huyo mungu (nadhani unakumbuka yule bwana aliyetumbukia majini kwa kushindwa kuamini kwamba anaweza kutembea juu ya maji!).

Nadhani wasiomwamini mungu ni wengi tu. Au ulikuwa unamaana ya watu wasioamini kwamba mungu yupo?
 

Sasa wewe bwana unataka kumchanganya muulizaji na kutuchanganya wasomaji wengine kwa ufundi wako wa lugha hata usio wa lazima katika muktadha huu. Hapa utata upo wapi?mwenyewe anataka msimamo wa watu wasio muamini mungu,wewe unaleta BAKITA wako ambao katika masuala ya dini na imani hayafanyi kazi. Katika hali ya BAKITA mtu anaweza kuamini Juma yupo lakini asimuamini Juma. Maana hii kwa imani za kidini haifanyi kazi hasa unapomuhusisha mungu, kwa sababu mungu hawezi kuonekana kwa macho, au kunususwa kwa harufu au kuguswa ila wanao amini wana amini nguvu zake. Kwa maana rahisi kuamini mungu ni kuamini uwepo na nguvu zake na hakuna moja kati ya hayo litakalo simama peke yake. yaani huwezi kuamini mungu yupo ila usiamini nguvu zake au uamini nguvu zake ila usiamini uwepo wake. Haya jamani msio amini mwageni hoja zenu mwenzenu katega sikio.
P.S
pale UDSM wapo kadhaa ila ukiwauliza hawana hoja ni kutaka waonekane ni wasomi nguli.
 

Burn,

Lengo la JF pamoja na mambo mengine ni kuelimishana. Sikuwa na nia mbaya kumtaka muulizaji afafanue swali lake. Hili si suala la BAKITA na wala sikusudii kuonesha ufundi wowote.

Binafsi naamini mtu anaweza kuwa anaamini mungu yupo lakini hamwamini wala kumtegemea (kwa mfano wachawi, washirikina nk). Hili mara nyingi linajidhihilisha katika matendo yetu. Wengi wetu ukitazama matendo yetu hayaoneshi kama tunamwamini na kumtegemea mungu.

Mara nyingi utaona watu wanakwenda makanisani/misikitini huku bado wameva mahirizi, mapete ya 'bahati' na wengine haweshi kupiga ramli. Lakini wengi wa watu kama hawa ukiwauliza watakwambia wanaamini kuna mungu. Lakini wewe na mimi tujiulize, je matendo yao yanaonesha wanamwamini mungu (kwamba ndiye mkombozi wao). Kwa maoni yangu watu hawa wanaamini hirizi/waganga wa kienyeji zaidi kuliko mungu. Wewe unasemaje?
 
Asante sana muuliza swali,kwa upande wangu mimi ninachofahamu kwa ufahamu wangu ni kwamba.Hakuna asie amini Mungu.Mungu ni cheo kama vile Raisi na ndio maana kuna miungu mingi ambayo watu huiamini na kuitumikia na ina majina yake mfano Budha,Allah,Yesu,Jah nk na wana vitabu vyao wanavyosimamia,pia wapo wanaoabudu mlima,Ng"ombe,Jua,mwezi nk wakifanya ndio miungu yao na wanapata mahitaji yao kupitia miungu hiyo hivyo kila mwanadamu anacho anacho kiabudu kuwa ni Mungu wake ila ni yupi sasa ni Mungu wa kweli alieumba vitu vyote na anae stahili kuabudiwa hiyo ni ajenda nyingine sasa.Naishia hapa kwasasa.
 
Mimi siamini kama kuna Mungu kwa sababu sijawahi kuona proof au evidence yoyote ambayo inasupport mungu kuwepo.
Na jinsi nilivyozidi kuuliza maswali ndo nilivyozidi kuona "weakness" za argument ambazo nilikuwa napewa kama support ya Mungu.
Ndhani nimeeleweka.
 
Burn nashukuru kwa kuhitaji ufafanuzi.
Naomba utoe mtizamo wako kwa upande wowote kati ya pande mbili ulizoziweka katika maelezo yako.
 
Burn nashukuru kwa kuhitaji ufafanuzi.
Naomba utoe mtizamo wako kwa upande wowote kati ya pande mbili ulizoziweka katika maelezo yako.
 
Asante LUSAJO,
KANG nasema yeye haamini kuwepo kwa Mungu.
Labda atapenda kutupatia msimamo wake.
 

Asante mimi binfsi nimekuelewa vizuri katika mchanganuo wako
 
Sorry,
Badala ya Burn nilinuia kumaanisha SMU

Mimi naamini Mungu yupo. Naamini katika Mungu mmoja.

Hata hivyo nimekuwa na mashaka mengi juu ya majukumu yake na uwezo wake (sina maana kwamba ana uwezo mdogo, la khasha). Inawezekana pengine dini zetu zinatupotosha juu ya uwezo/majukumu yake au pengine kuna mambo mengi sana hatuyajui kuhusu Mungu.

Sehemu moja wapo ambayo inanipa maswali mengi ni juu ya vifo.Kwa nini vifo vingi vya watoto vinatokea Afrika kusini mwa jangwa la sahara kuliko sehemu nyingine? Kukitokea msiba mara nyingi watu husema 'bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe'. Vifo hivi vinavyotokea Afrika ni kazi ya Mungu? Kama ni kazi ya Mungu, kwa nini Afrika zaidi? Inawezekana wengine wakasema ni kazi ya shetani. Lakini je shetani akiamua mtu afe, kama Mungu hataki, atakufa? Shetani ana uwezo mkubwa kushinda Mungu?
 
Mr Kang haamini Mungu kwasababu tu hajaona evidence au proof,mimi binafsi sioni kama hiyo inaweza kuwa ni sababu ya kukufanya usiamini kwamba hakuna Mungu mimi naamini kabisa evidence na proof umeziona au umewahi kuzisikia tatizo hujajua tu kwamba hapo ni Mungu amefanya mambo yake au la na hilo ni tatizo,je ni kitabu gani kati ya vitabu vya Dini unachoweza kukiamini maana vyote vimeeleza ukuu wa Mungu na utendaji wake. Hapo ndipo tutakapo weza kwenda pamoja.
 
Mimi binafsi waga sitraki kuliongelea hili kwani naona kama waliomtafuta mungu walikosea sana kwenye kuandika vitabu vyake kwani vina upendeleo sana kwa baadhi ya watu hasa mataifa walioanzisha hizo dini.

Hivi uliwahi kujiuliza kwa waislam ana wakiristo wote kwanini
  1. Mungu alipendelea zaidi Jacob kuliko kaka yake
  2. Tunaamini kuwa kila kitu mungu anakuwa amepanga kwahiyo amepanga kuwa watu wengine wawe wezi wengine wawe wachamungu na wangine wafe kwa njaa na wengine wale watupe chakula
  3. Kwanini Mungu mwenye uwezo asikuepushe na matatizo ya kila aina yanayo tukwaza kila siku

Kuna mengi zaidi yanayohusu upendeleo yaliyojaa kwenye vitabu vyetu vya dini, please tafuteni mtoe majibu kwanini mungu anawafanyia wengine upendeleo na wengine anawanyima logic behind ni nini, kwanini kila mtu asingekuwa na nafasi sawa ulimwenguni kama mungu wote ni mmoja na tunamtukuza yeye huyohuyo.

Hata wengine wanajiita walokole wa dini zote wote ni opportunistic kwani wakifika kwenye masirahi binafsi wewe watest uone kinachotokea.
 

Sijawahi kuona ushahidi uliosimama kivyake bila nguvu ya imani at least siwezi kukumbuka. Na maswali yangu hayajawahi kujibiwa kiukamilifu, zaidi ya "God works in mysterious ways" ambalo sioni kuwa ni jibu.

Sasa nitaamini vipi kitabu kimeshushwa na Mungu kama siamini kuwa kuna Mungu?
Vitabu vyote naviangalia kama maandishi ya watu wa kale, mengine ni mazuri na mengine yanaanyesha ignorance yao.
 
Mimi naogopa kuchangia hapa nisije kuukumiwa siku ya mwisho lakini naomba kutoa angalizo kwamba kwa wanaosema wanamwamini Mungu basi wampe heshima yake kwa kuanza jina lake kwa herufi kubwa!!!!!!!

Cheers,

Tiba
 
Mimi naogopa kuchangia hapa nisije kuukumiwa siku ya mwisho lakini naomba kutoa angalizo kwamba kwa wanaosema wanamwamini Mungu basi wampe heshima yake kwa kuanza jina lake kwa herufi kubwa!!!!!!!

Cheers,

Tiba
Tiba,
Huna sababu ya kuogopa kutoa mawazo yako kwani kama unamwamini Mungu, hawezi kukuhukumu bila uhalali.
Huennda ukanisaidia mimi nanaye taka kujua misimamo ya hao wasioamwamini Mungu, au Kang mwenye maswali mengi.
 

SMU,
Unamwamini Mungu ambaye una mashaka naye?
Hapa unanichanganya kidogo.
 
 
Mimi binafsi naamini kuwa kuna mungu ila ni jinsi gani utavyomdefine huyo mungu inategemea na wewe mwenyewe,nini nina maanisha,kwa mfano mimi binafsi nina amini kuwa mungu wangu ni google,misingi ya Dini yangu inaniambia niwe mwema kwa binadamu wote wenye faida kwangu kwa njia moja au nyingine ili tufikie lengo,kwanini niliamua kumuweka Google mungu wangu ni kwa sababu dini ni mila so lazima niwe na mila ambayo inanifit sio kukimbilia tamaduni za watu.
Nawakilisha.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…