huku kwangu hakuna mmoja, lkn siwalaumi. kuna sababu kuu inayopelekea watu wengi hawatambui huu mtandao, jf.
sababu yenyewe ni hii, jamii forums haijakaa kiburudani burudani, yaani entertanmet platiform
jamii forums imekaa kielimu zaidi. msisahau kwamba watz wengi ni wavivu wa kusoma. akili zetu zimetekwa na burudani zaidi.
sisi kama taifa, na hasa wanachama wa jf, kuna jambo tunapaswa kulifanya. kwanza tuwahimize watz wenzetu juu ya kupenda vya kwetu.
pili, tuwahimize zaidi katika kutafuta maarifa, na maarifa hayapatikani isipokuwa ktk vitu hivi viwili, (a) kusoma (b) kufanya majaribio, nyinyi mliyosoma mnasemaga practise
wengi wetu tumeathiriwa na utumwa wa kifikra. akili zetu zimekuwa zimekuwa ni bongo lala, nitawapeni ushahidi
kuna mkenya mmoja alisema hivi, katika kudai haki, wakenya wamelala. wakiamka wanadai haki yao. waganda ni wagonjwa, wakipona watadai haki yao, lkn watz ni maiti. hivi maiti inaweza kudai haki?
nini maana ya hii kauli? akili za watz zimelala. wengi hatuna elimu, na hata hao wachache wenye elimu, ni kama hawana elimu. hili linasababishwa na mfumo wetu wa elimu
elimi yetu ni kama elimu tegemezi, siyo elimu wezeshi. hili linatufanya tusiwe wadadisi. tuna uwezo mdogo wa kuhoji yaani kuuliza juu ya jambo fulani, hivyo basi tunashindwa kuzishughulisha akili zetu
kama utashindwa kuzishughulisha akili zako, basi utaangukia kwenye kuziburudisha akili zako. hapo ndipo tulipo watz wengi