Hapo mtaani kwako wangapi mnatumia JF?

Hapo mtaani kwako wangapi mnatumia JF?

Habarini wakuu:

vp hapo.kwenu ni wangapi mnaotumia mtandao wa jf au ndo wewe peke yako.? ushawahi kushawishi mtu ajiunge jf.?
Since nipo Chuo mpaka sahivi nipo mtaani Zaidi ya miaka mitatu sijawahi Kuona ama kusikia anyetumia JF.....

Ni wazi ukiachana na JF kuwa platform ya watu Makini but pia ni sehemu ya watu walitembea age kidogo
 
Wachache mno, kila niliyemuambia hata haijui, anasema anaisikia tu !

Good enough kuna mshikaji wangu mmoja yupo humu ila wote tunaishi kama digidigi....Hatujawahi kuambizana IDs zetu.... ila tunaambizana yanayojiri humu, au anaweza kukuambia kuna habari flan ipo jukwaa flan ebu ukipata muda ipitie n.k
 
Tatizo la jamiiforums ni kama nyara, kila anayetumia mtandao huu hataki jamaa zake wajue utambulisho wake ili kila mmoja awe huru kwenye mijadala.
Ndugu zangu hawataki kutaja I'ds zao ili wawe huru.
 
Id ya mkeo?
Mbona inajulikana vizuri tu.

Sema nyie akina "Joined 2026" hamuwezi kuelewa!

Screenshot_20260802_170940.jpg
 
Yani mm hapa mtaani ukitaja Jamii Forums watakuuliza ndo taasisi gani hiyo? Ipo chini ya wizara gani?😂
Marafiki zangu wengi(kama sio wote) ni Tiktok,IG,Snapchat.
Sema siwalaumu since we are all Teenagers ndo wakati wao huu.
Mm JF,Reddit,X ndo mitandao yangu. Wananiona wa ajabu kweli yan😂
 
Back
Top Bottom