Hapo mtaani kwako wangapi mnatumia JF?

Tatizo la jamiiforums ni kama nyara, kila anayetumia mtandao huu hataki jamaa zake wajue utambulisho wake ili kila mmoja awe huru kwenye mijadala.
Ndugu zangu hawataki kutaja I'ds zao ili wawe huru.
Jf huwezi fungua mbele ya kadamnasi, as you said ni kama nyara, ukionekana nayo wanajua wewe ni mpinga Serikali
 
Mkuu kipi kinachokufanya ujifiche fiche wakati wewe mwenyewe umejipambanua kama mtetezi wa chama tawala na serikali yake.
Nadhani wale wanaokosoa chama tawala na serikali zake wana haki kujificha hasa kutokana na hali ya mambo inavyoenda kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kwa sasa.🙄🙄
Kwa aina ya michango yako kwenye jukwaa la siasa inafaa hata kuweka namba yako ya simu hadharani ili angalau ukumbukwe kupewa kijiko na uma ili nawe ukakae mezani utafune mema ya nchi.🤣🤣🤣🤣🤣
( mkuu huu ni utani tu 😂😂)
 
Haya matusi ya JF machadema wanatayamishia kwenye namba yangu ya simu nayajua haya majamaa kwa kutukana.
 
Sasa hapo si muambizane tu hizo Id zenu jamani, au ndo mnaogopa kujuana msije mkaanikana madudu yenu hapa jukwaani 🤣🤣
 
JF ina watumiaji wengi tu ambapo ni member (registered) na ambao sio member ramsi (guest user ) kitu pekee kinacho tofautisha na social platforms zingine ni kua watuamiji wa huu mtandao hatupendi kujulikana tuna utumia na hata kuweka wazi ID zetu.
Mm binafsi nime anza kutumia Toka 2010 nikajiunga rasmi 2013 baadae nikaja tambua Mzee wangu ni mtumiaji mzuri tu nae wa huu mtandao.
Miaka ya nyuma kidogo pia wakat nafanya field kwenye Moja ya ofis kubwa tu ya serikali pale mjini Posta mkabala na NIC Kuna boss Mmoja aliomba msaada kwenye desktop yake wakati nimeingia tu kwenye chrome nika kutana na Tab ya JF haikuishia hapo baadae nilipo ajiriwa pia Kuna maboss zangu nilikuta nao ni wasomaji wazuri tu wa huu mtandao ndipo nika notice kua watumiaji wapo lakini hua hawapendi kuweka wazi kua Wana utumia mtandao huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…