TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,714
- 11,747
Mimi ni mvulana mwenye umri miaka 35. Nimewahi kuwa na rafiki yangu wa kike ambaye tulipependana nae kwa miaka mitatu hivi. Lakini kilichonishangaza kwa muda wote huo, huyo girlfriend wangu hakuwahi hata kuninunulia hata zawadi ndogo ya shukrani. Nimemnunulia vitu vingi na mara nyingi nimempleka lunch na hata dinner. Vile vile kwa muda wote huo amkuwa na tabia kuomba nimnunulie hiki na kile.
Nilipogundua kuwa ni mhitaji sana wa vitu vingi, nilimdanganya tu kama njia ya kumpima kuwa mimi ni mgonjwa na kazi sina. Yeye anaishi Dar na mimi nipo Mwanza. Kilichonishangaza ni kuwa tangu nimpe habari hii, hata siku moja hakuwasiliana nami tena. Ndiyo ikawa mwisho wa mawasiliano yetu. Hata ile kunijulia hali hamna. Wakati nilipokuwa namtimizia haja zake alikuwa akinipa maneno matamu kuwa atanipenda hata mpaka ahera! Je, huu ni ule msemo wa kiswahili usemao; hapendwi mtu ila pochi? Naombeni mnisaidie.
Source: http://www.darhotwire.com/maisha/mh_other.php?id=4432