Kisa cha kweli: Labda tunaweza kujifunza kitu kuhusu mapenzi kupitia story ya maisha yangu

Mar 25, 2023
73
246
Mimi sio mwandishi mzuri hivyo tutavumiliana kidogo.

Mimi ni kati ya wale vijana wachache ambao tumepata bahati ya kuwa na pesa tukiwa na umri mdogo, nikisema umri mdogo sijui mnanielewa? By 22 nilikuwa na nyumba 5 na gari za kutembelea mbili ukitoa vitu vingine ambavyo sio muhimu kusema.

Kabla hamjaanza kusema hii ni chai labda kidogo niwape chanzo cha mimi kuwa na access ya hizi mali. Kabla ya kufa, baba yangu alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mkulima.

Baada ya kufariki mali ziligawanywa nusu kwa nusu kati yangu na aliyekuwa mke wa mzee kwa wakati huo, ingawa ulikuwa ni ugomvi mkubwa sana hadi tukafikia mgawanyo huo (story ya siku nyingine ).

Kwa mzee wangu nilizaliwa peke yangu na mama yangu alifariki baada ya kunizaa mimi, nimelelewa sana na mzee, nilipofika darasa la saba mzee akaamua kuvuta jiko ingawa muda wote hawakufanikiwa kupata mtoto.

pia baada ya kuingia sekondari nilipelekwa boarding hivyo hatukuwa na ukaribu sana na huyo mama mdogo.

Baada ya mgao nilipewa nyumba 5 ambazo 2 zilikuwa Dar na 3 mkoa tuliokuepo (mkoa sitotaja mzee wangu alikuwa maarufu kidogo), mashamba , Rav 4 Kili time na pesa ambazo tuligawana baada ya kuuza baadhi ya vitu.

Baada ya kumaliza Diploma katika Chuo kimoja Jiji la Makala, ndugu zangu ndio wakanipa full access ya vitu vyote, sikuwa na chochote cha kunirudisha mkoani kwangu hivyo nikaamua kuanza maisha Dar.

Nyumba zilikuwa zimepangishwa hivyo niliamua kupanga na pia sikutaka kukaa kwenye nyumba kubwa peke yangu, nilitafuta apartment karibu na town sababu nilikuwa na lengo la kufungua biashara hivyo sikutaka kukaa mbali sana na town. Pia nilinunua Toyota Ist ilikua nisaidia mizunguko ya town, Rav 4 Kili time niliipiga bei maana ilikuwa inafanya nimkumbuke sana mzee kila nikiiangalia.

Baada ya miezi minne ya kupambana kutafuta fremu nikfanikiwa kupata fremu Kariakoo, nikafungua duka la computer's na vifaa vyake. Nilikuwa na uzoefu na biashara hii, pia nilipata msaada kutoka kwa uncle wangu ambae alikuwa akiifanya hii biashara.

Bidhaa nyingi tuliagiza Dubai na China, mara nyingi Uncle alienda kufunga mzigo Dubai hasa hizi computer refurbished na vifaa vingine, kwa hiyo nikawa naunganisha mzigo kwake baadae nikawa naenda pia.

Kwa ufupi baada ya kama miaka 3 hivi nikiwa Dar nilifanikiwa kusettle, nilikuwa na biashara iliyosimama vizuri, nilipata pesa za kodi, mashamba nilikuwa nikikodisha sababu sikuwa interested sana na kilimo, nikanunua gari nyingine Crown athlete.

Pamoja na yote hayo bado nilikuwa naishi kwenye apartment, nilikuwa sio mtu wa bata sana starehe yangu kubwa ilikuwa kucheza game, movies na gambe ingawa nilipenda sana kunywa nyumbani, nikitoka ni mara moja moja sana.

Kipindi hiki chote pamoja na kula mbususu kadhaa ila nilikuwa na demu mmoja tu, tulianza kudate tukiwa diploma akafanikiwa kupata kazi, hivyo mara nyingi alikuwa akija home na kurudi kwao. Alikuwa mwanamke mmoja smart sana, very caring, mpishi mmoja hatari sana, ingawa hakubarikiwa sana sura ila shepu ilikuwa ni shida. Nilimpenda sana pia alinikaba kila kona hata kucheat ikawa kidogo mtihani labda kula kimasihara zilipojitokeza.

Mzee wangu alinifundisha vitu vingi kuhusu biashara pamoja na pesa, pia ukaribu wangu na uncle ulichangia sana kunifanya niwe na matumizi mazuri ya pesa pamoja na kuwekeza.

Hadi kipindi hiki mambo yalikuwa yananiendea vizuri pesa nilikuwa naiona, pia nilikuwa na mpango wa kumvisha pete Lisa ambaye alikuwa mpenzi wangu kwa kipindi hicho.

Ilikuwa ni Ijumaa baada ya kucheza sana game na masela wangu home, mida ya saa tatu nikapokea sms kutoka kwa Lisa, anataka nimfate anakuja kulala kwangu, ikabidi niwapeleke masela home halafu nikampitia Lisa maeneo ya kwao. Alikuwa na nyege sana siku hiyo tulivyofika home hatukuwa na mambo mengi moja kwa moja tulianza show, baada ya round ya pili kuisha tukiwa tunajiandaa kwenda kuoga simu yangu ikaita sababu ilikuwa usiku sana, Lisa akawahi kuchukua simu lengo kujua nani anapiga.

Baada ya kuangali simu na kuona namba ngeni akaniangalia kwa jicho kali akapokea na kuweka loud speaker na kunipa simu huku akisikiliza kwa makini.....

Itaendelea....
 
Na huu mfungo sijui nitapata wapi bagia
JamiiForums-265074307.jpg
 
Hiyo Aya ya mwisho nimekerwa na mambo mawili. Kwanza ni hiyo tabia ya demu wako kuchukua simu na kuipokea as if ni yake. Hii tabia huwa naona ni kukosa adabu kuliko pitiliza. Hata kama ni mwanaume wako usithubutu kuipokea simu yangu pengine ni mtu ananidai au nimedanganya kuwa sipo karibu na simu wewe unapokea hiyo sio adabu hata kidogo Pumbavu zako shemeji lisa.

Pili ni hii tabia ya kuja na story nusu nusu badala ya kuandika kitu cha kueleweka. Ukapost chote unaandika nusu nusu halafu unasema itaendelea unatukera tunaosoma na mimi nikishaona neno itaendelea huwa naishia hapo hapo.

Kwahiyo naomba nikufahamishe ndugu mleta uzi kuwa umenikera sana matako yako mbwa wewe na Hadithi yako zitasoma tena.
 
Watu mna makasiriko...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂 Daaahh!!!
 
Mimi sio mwandishi mzuri hivyo tutavumiliana kidogo.

Mimi ni kati ya wale vijana wachache ambao tumepata bahati ya kuwa na pesa tukiwa na umri mdogo, nikisema umri mdogo sijui mnanielewa? By 22 nilikuwa na nyumba 5 na gari za kutembelea mbili ukitoa vitu vingine ambavyo sio muhimu kusema.

Kabla hamjaanza kusema hii ni chai labda kidogo niwape chanzo cha mimi kuwa na access ya hizi mali. Kabla ya kufa, baba yangu alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mkulima.

Baada ya kufariki mali ziligawanywa nusu kwa nusu kati yangu na aliyekuwa mke wa mzee kwa wakati huo, ingawa ulikuwa ni ugomvi mkubwa sana hadi tukafikia mgawanyo huo (story ya siku nyingine ).

Kwa mzee wangu nilizaliwa peke yangu na mama yangu alifariki baada ya kunizaa mimi, nimelelewa sana na mzee, nilipofika darasa la saba mzee akaamua kuvuta jiko ingawa muda wote hawakufanikiwa kupata mtoto.

pia baada ya kuingia sekondari nilipelekwa boarding hivyo hatukuwa na ukaribu sana na huyo mama mdogo.

Baada ya mgao nilipewa nyumba 5 ambazo 2 zilikuwa Dar na 3 mkoa tuliokuepo (mkoa sitotaja mzee wangu alikuwa maarufu kidogo), mashamba , Rav 4 Kili time na pesa ambazo tuligawana baada ya kuuza baadhi ya vitu.

Baada ya kumaliza Diploma katika Chuo kimoja Jiji la Makala, ndugu zangu ndio wakanipa full access ya vitu vyote, sikuwa na chochote cha kunirudisha mkoani kwangu hivyo nikaamua kuanza maisha Dar.

Nyumba zilikuwa zimepangishwa hivyo niliamua kupanga na pia sikutaka kukaa kwenye nyumba kubwa peke yangu, nilitafuta apartment karibu na town sababu nilikuwa na lengo la kufungua biashara hivyo sikutaka kukaa mbali sana na town. Pia nilinunua Toyota Ist ilikua nisaidia mizunguko ya town, Rav 4 Kili time niliipiga bei maana ilikuwa inafanya nimkumbuke sana mzee kila nikiiangalia.

Baada ya miezi minne ya kupambana kutafuta fremu nikfanikiwa kupata fremu Kariakoo, nikafungua duka la computer's na vifaa vyake. Nilikuwa na uzoefu na biashara hii, pia nilipata msaada kutoka kwa uncle wangu ambae alikuwa akiifanya hii biashara.

Bidhaa nyingi tuliagiza Dubai na China, mara nyingi Uncle alienda kufunga mzigo Dubai hasa hizi computer refurbished na vifaa vingine, kwa hiyo nikawa naunganisha mzigo kwake baadae nikawa naenda pia.

Kwa ufupi baada ya kama miaka 3 hivi nikiwa Dar nilifanikiwa kusettle, nilikuwa na biashara iliyosimama vizuri, nilipata pesa za kodi, mashamba nilikuwa nikikodisha sababu sikuwa interested sana na kilimo, nikanunua gari nyingine Crown athlete.

Pamoja na yote hayo bado nilikuwa naishi kwenye apartment, nilikuwa sio mtu wa bata sana starehe yangu kubwa ilikuwa kucheza game, movies na gambe ingawa nilipenda sana kunywa nyumbani, nikitoka ni mara moja moja sana.

Kipindi hiki chote pamoja na kula mbususu kadhaa ila nilikuwa na demu mmoja tu, tulianza kudate tukiwa diploma akafanikiwa kupata kazi, hivyo mara nyingi alikuwa akija home na kurudi kwao. Alikuwa mwanamke mmoja smart sana, very caring, mpishi mmoja hatari sana, ingawa hakubarikiwa sana sura ila shepu ilikuwa ni shida. Nilimpenda sana pia alinikaba kila kona hata kucheat ikawa kidogo mtihani labda kula kimasihara zilipojitokeza.

Mzee wangu alinifundisha vitu vingi kuhusu biashara pamoja na pesa, pia ukaribu wangu na uncle ulichangia sana kunifanya niwe na matumizi mazuri ya pesa pamoja na kuwekeza.

Hadi kipindi hiki mambo yalikuwa yananiendea vizuri pesa nilikuwa naiona, pia nilikuwa na mpango wa kumvisha pete Lisa ambaye alikuwa mpenzi wangu kwa kipindi hicho.

Ilikuwa ni Ijumaa baada ya kucheza sana game na masela wangu home, mida ya saa tatu nikapokea sms kutoka kwa Lisa, anataka nimfate anakuja kulala kwangu, ikabidi niwapeleke masela home halafu nikampitia Lisa maeneo ya kwao. Alikuwa na nyege sana siku hiyo tulivyofika home hatukuwa na mambo mengi moja kwa moja tulianza show, baada ya round ya pili kuisha tukiwa tunajiandaa kwenda kuoga simu yangu ikaita sababu ilikuwa usiku sana, Lisa akawahi kuchukua simu lengo kujua nani anapiga.

Baada ya kuangali simu na kuona namba ngeni akaniangalia kwa jicho kali akapokea na kuweka loud speaker na kunipa simu huku akisikiliza kwa makini.....

Itaendelea....
Duuuh jmn hadii tuanze kusubili muendelezo tena
 
Kutokana na majukumu nakosa muda wa kuandika yote , hivyo nitaendelea kuandika kwa vipande.

SEHEMU YA PILI.

"
0ya Bob ? umenitenga sana mwanangu." baada ya kusikia maneno hayo Lisa akaniacha chumbani na kuelekea sebuleni, kabla sijajibu chochote jamaa akaendelea kuongea. " Mimi Kida hii namba yangu mpya mwanangu."

Hapo ndo nikajua naongea na nani maana muda wote huo nilikuwa sijajua.

" Kida vipi mwanangu ?. hii namba nilikuwa sina "

" Save hiyo kaka ndo natumia , Bado upo Dar ?. kesho naingia huko kaka"

" Ndio nipo kaka nitaenda wapi." Baada ya mimi kusema hivyo Kida akacheka .

" Tutaongea kesho nikifika huko kaka muda huu nipo kwenye kelele"

" Poa poa kaka" Baada ya hapo nikakata simu .

Kitendo cha Lisa kupokea simu kilinipa sana hasira! nikaona huyu sasa ameanza kunizoea vibaya , baada ya kukata nilitoka chumbani na kuelekea sebuleni , nikamkuta amekaa kwenye sofa nikasimama pembeni yake.

" Kwa hiyo wewe ulivyopokea simu ulitegemea kusikia sauti ya nani ?" alivyoona nimemuuliza hivyo huku nikiwa serious sana akasimama nakunikumbatia huku akiweka kichwa chake kifuani kwangu , nikamtoa mikono nikamkalisha kwenye sofa huku nikikaa karibu yake.

" Bob nisamehe unajua nakupenda sana , nilivyoona ile namba haina jina nikadhani atakuwa mwanamke mwingine , plz nisamehe."

Wadau huyu demu nilikuwa nampenda sana hivyo baada ya kuniomba msamaha nikaona sio issue acha yapite tu . Baada ya kuongea kwa muda pale kwenye sofa nikamuacha akiendelea kucheki Tv nikaelekea chumbani kulala maana nilikuwa na usingizi tayari.

Asubuhi ilivyofika niliamshwa na kelele za muziki sebuleni , Lisa alipenda sana kupiga muziki akiwa anafanya usafi. Mara nyingi Jumamosi nilipendelea kushinda nyumbani, dukani nilikuwa nikienda jioni kufunga hesabu tu.

Baada ya kuamka nilienda kujiweka sawa na kuelekea sebuleni ambapo tayari Lisa alikuwa ameanda chai lakini alikuwa nje anamalizia usafi. Baada ya chai tulitoka na kuelekea sokoni kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali kwenye mida ya saa tano nikiwa narudi home kutokea sokoni , nikapokea simu kutoka kwa Kida.

" Bob nipo tayari mjini jioni nitakucheki basi tuonane "

" Poa kaka utanicheki." baada ya kukata simu Lisa ndo akaanza kuniuliza kuhusu Kida maana asilimia kubwa ya marafiki zangu anawafahamu kasoro Kida.

Subiri niwaeleze kidogo kuhusu Kida. Nilisoma nae olevel tulikuwa marafiki wakubwa sana huko nyuma , Kwao ni Arusha baada ya kumaliza o level akuendelea na shule akaingia kupiga kazi kwenye kampuni ya utalii ya Mzee wake, hivyo mara nyingi akija Dar lazima anicheki tangia kipindi nipo Chuo.

Ni mtu wa bata sana , mara nyingi akiwa Dar anakuwa na kaka zake ambao wanapesa sana, ingawa hadi leo sijawah kujua wanafanya mishe gani maana unaweza usiwaone mjini hata miezi 2 lakini wakirudi , wanarudi na magari mapya , wanawake na bata kwa sana then wanapotea tena.

Kwenye mida ya tisa mchana nikatoka na Lisa baada ya kula msosi wa mchana , nikaingia dukani Kariakoo then nikamrudisha kwao Kisha kurudi nyumbani.

Hadi naingia home ilikuwa mida ya saa kumi na mbili kasolo , nimefika home naingia ndani naona simu inaita kucheki ni Kida nikapokea.

"Oya ukwapi kaka nije nikufuate ndo mida hii." Kutokana na sauti yake nikagundua tayari alikuwa amewaka.

" Nipo home kaka bado unapakumbuka uliponileta siku ile."

" Sio sana kaka maana ni muda kidogo."

Tukakubaliana tukutane kwenye Barabara ya moja ambayo haipo mbali sana na ninapokaa.

Baada ya dakika chache nikawa nimejiandaa nakuanza kusogea mdogo mdogo kwa mguu maana sio mbali sana na home, nikiwa njiani nikawa naongea na Lisa mdogo mdogo nikielekea road.

Kufika road nikampigia simu Kida akaniambia tayari ameshafika muda tu , akanielekeza nisogee kwa mbele kidogo. kusogea mbele nikaiona discovery 4 nyeusi imepaki lakini ilikuwa imezibwa na daladala hivyo Kwa nyuma ni ngumu kidogo kuiona.

Kama nilivyowaambia kaka zake wakirudi mjini lazima wanunue magari mapya , plate namba ya hii gari ilionyesha ni mpya. Nilifika nikafungua mlango wa mbele na kuingia .

" Daaahh!! kitambo sana kaka siku hizi umevimba kaka unapiga gym nini ?." Kida aliongea huku akinipa mkono.

kwenye gari alikuwa peke yake.

" Amna kaka kidogo tunagusa gusa tukiwa free" wakati naongea akawa ameshachukua Heineken kiti cha nyuma na kunikabidhi .

" Itabidi na mimi nianze maana hichi kitambi kinakuja kwa kasi" Huku akichukua chupa ya black en White na kuongezea kwenye kikombe chake.

Tulikaa kama dakika 20 tukiongea mambo mbali mbali. Baada ya hapo ndo akaniambia bro wake mmoja amemvisha pete mpenzi wake hivyo kuna party wameandaa ko tunaenda huko. Kwa kuwa alikuwa ameanza kunywa tangia mchana hivyo akaniomba niendeshe gari.

Nikashuka nikahamia upande wa dereva na yeye upande wangu. kabla hatujaondoka akapigiwa simu na huyo shemeji yake tuwapitie rafiki zake maeneo ya Mwenge tunavyorudi.

Tukaanza safari huku tukikumbuka matukio mbali mbali ya kipindi hicho tukiwa shule, baada kama ya dakika 30 tukawa tumefika Mwenge nikapaki gari huku Kida akipiga simu kujua tunaowapitia wapo wapi. Baada ya dakika kadhaa Toyota harrier ikasimama mbele yetu wakashuka wanawake wa tatu .

Walikuwa wamependeza sana hadi nikajishtukia maana nilikuwa nimevaa simple sana , nikawaza huko ninakoenda kutakuwa kwa moto , wanawake wale walivyokuwa wamependeza lazima ujiulize mara mbili mbili.

Kida akashuka akaenda kuongea nao then wakaja wote na kuingia kwenye gari , wakanipa salamu then tukaanza safari kuelekea huko kwenye hiyo party , muda wote huo nilikuwa sijaongea chochote zaidi ya kupokea salamu yao, muda mwingi Kida ndo alikuwa akiongea nao, Mimi macho yangu yote yakiwa barabarani.

Mmoja wao akamuuliza Kida mbona ndugu yako dereva yupo kimya sana au anaumwa , Kida akaniangalia alafu akaanza kucheka na mimi nikajikuta nacheka!, Nikamjibu hapana nikiwa naendesha napenda kufocus ndo maana nipo kimya , akadakia rafiki yake ndo utaki hata kuchangia mada nikatabasamu huku nikiangalia angalia mbele .

Tulikuwa tumesha karibia kufika kwa mbali nikaona kuna magari mengi yamepaki nje. kufika pale nikapaki pembeni nyuma ya gari nyingine maana parking ya ndani ilikuwa imejaa. wakashuka wale wadada tukabaki na Kida ndani ya gari. Baada ya sekunde chache akarudi mmoja na kuja upande wangu , nikashusha kioo , akaninong'oneza " ukiingia ndani nitafute" nikamjibu fresh akaondoka na kuwafuata wenzie. Kida akaanza kunitania huku tukiendelea kushusha gambe kwenye gari .

Baada ya dakika 15 tukaamua kuingia ndani watu walikuwa wengi sana , wadada wazuri walikuwa kila kona utakayotupa macho , tukaenda moja kwa moja sehemu waliokuepo kaka zake Kida , nikawapa salamu pamoja na kumpongeza aliekuwa anamvisha pete mchumba wake.

Hadi hapo ilikuwa imeshafika saa mbili , tulikaa na kaka zake Kida Kwa muda mrefu kidogo tukipiga story na kunywa huku muziki ukipingwa.

Nilivyochoka kukaa nikaamua kusimama na kwenda kunyoosha miguu kidogo nje . nikasogea hadi sehemu moja kulikuwa na garden ya maua , nikaegemea ukuta lengo nitoe simu nimcheki Lisa , Ghafra akaja yule msichana aliesema nimtafute nikiingia ndani bila kusema chochote akanishika mkono na kuanza kunivuta moja kwa moja hadi kwenye meza yao .

Walikuwa wamekaa kama watano hivi na zote zilikuwa pisi kali , wakaniambia wanataka niwape company kwenye meza yao pia wakati wa kuondoka niwapeleke nyumbani ,bado nikasema poa maana funguo za gari nilikuwa nazo mimi nikapewa kiti na kukaa tukaendelea kupiga story huku tukishusha gambe , hapo inaenda saa nne kasoro.

Tukiwa tumekaa pale alikuja dada mmoja akaanza kuongea na yule ambae alinishika mkono nakunivuta pale. kiukweli nipingwa na butwaa hadi nafika umri ule sidhani kama nilikuwa nimewahi kuona mwanamke mzuri kiasi kile, alikuwa na shepu nzuri , sura, mweupe wazungu wanasemaga " A complete package".

Nilibaki nikimuangalia muda wote akiongea na mwenzie , ghafla mwezie akanionyeshea kidole mimi , akatoka akaja hadi karibu yangu akaniambia " Am Nancy my friend amesema utawapeleka home , nilikuwa naomba unipe lift na Mimi pia". muda wote anaongea nilikuwa kama nimepigwa shoti nikaishia kutikisa kichwa tu , huku nikimuangalia akiondoka .

Nilibaki kimya kwa muda kidogo nikitafakari uzuri wa yule mwanamke , nikabidi nizuge naenda chooni , lengo kumtafuta Kida anipe information kuhusu Nancy maana hadi muda huo nilikuwa sielewi chochote.

Nikamkuta Kida Bado anapiga story na kaka zake , nikamshika bega na kumsogeza pembeni nakuanza kumueleza nilichokiona. Baada ya kunisikiliza Kida akacheka sana . Huku akionyesha kumfahamu Nancy.

Tuliongea Kwa dakika kadhaa hapo ndo nikapata kuelewa kumbe wale wanawake wote wamesoma na huyo shemeji yake Kida , alienishika mkono alikuwa anaitwa Cathe . Cathe na Nancy wote walikuwa wanakaa Mbeya na walikuja kwa ajiri ya hiyo sherehe ya rafiki yao.

Hapo ndo nikapata mwanga kidogo sababu muda wote naongea nao sikuwaza hata kuwauliza majina yao, Mimi tabia yangu nisipomuelewa sana mwanamke huwa sitaki kumjua .

Kwa maelezo ya Kida ilionyesha anamfahamu Nancy lakini sio sana anajua detail ndogo ndogo tu , Lakini kwa sababu nitawapeleka home nikaona hiyo nafasi ndo nitaitumia kuchukua hata namba yake.

Tukiwa bado tunaongea simu yangu ikaanza kuita kuangalia alikuwa Lisa hapo tayari ilikuwa saa tano . Nikasogea pembeni kidogo iliniweze kuongea nae alikuwa tayari ameingia kulala hivyo tulitakiana usiku mwema nikakata simu, kurudi nilipomuacha Kida nikawakuta Cathe na Nancy wapo pale , kufika pale macho yangu yote namuangalia Nancy tu.

" Bob tumeshachoka tunataka kuondoka " Cathe aliongea kwa kudeka huku akiniangalia .

"Sawa subiri niwapeleke chap" nikasema huku nikiwaza Kida ndo aliemwambia Cathe jina langu au .

Kida akasema niwapeleke nitamkuta maana tulikuwa tumepanga kutafuta kiwanja cha kwenda baada ya kutoka pale.

Tukaondoka mbele akitangulia Cathe , Nancy huku mimi nikiwa nyuma, muda wote nilikuwa nashanga jinsi Nancy alivyoumbika , akilini nikitafakari jinsi gani nitaanzisha maongezi nae.

Tulipotoka nje kabisa tukielekea nilipopaki gari , kulikuwa na wadau kama watu wamekaa juu ya gari yao wanakunywa . Mmoja wao akamwita Nancy akaenda bila hata kusita , kuona hivyo nikahisi watakuwa wanajuana hivyo nikaendelea kuelekea gari.

Nikafungua tukaingia na Cathe huku tukimsubiri Nancy, baada ya kuona ukimya kati yangu na Cathe umezidi nikaanzisha story, baada ya kuongea kwa dakika kadhaa nikamuomba namba yake, akilini nawaza nikishindwa kuchukua namba kwa Nancy nimuombe Cathe.

Nilivyoona Nancy anachukua muda kuja nikaamua kuwasha gari na taa ilikumuharakisha, nilivyowasha taa kwa mbali nikaona kama kuna malumbano kati ya Nancy na wale jamaa.

Kuona vile tukashuka na Cathe kwenda kuangalia shida ilikuwa nini , kufika pale jamaa amemshikilia mkono Nancy hataki kumuachia anadai ameshakula pesa zake nyingi siku hiyo hivyo hawezi kumrusu aondoke peke yake kizembe , jamaa alikuwa ameshalewa wenzake walikuwa kimya tu , hawaongei chochote muda wote huo.

Akilini nikawaza hapa ndo pakujichukulia point kwa huyu demu , moja Kwa moja nilimfuata yule jamaa na kutoa mkono wa Nancy , nilivyotoa mkono nilishtukia jamaa karusha ngumi nikaikwepa , kuona hivyo nikaona hapa nimesha yakanyaga , akarusha ngumi ya pili nikaikwepa ila nikaona isiwe kesi acha na mimi nirushe , alikuwa amelewa hivyo ilikuwa rahisi kuona movement zake.

Akiwa anajiandaa kurusha ngumi nyingine , nikamuwahi nikampiga ngumi ya uso , akadondoka chini , hapo rafiki zake na baadhi ya watu waliokuwa nje wakaja kutuachanisha. Baada ya kujibizana nikaona isiwe kesi nikamshika mkono Nancy nakuanza kwenda nae kwenye gari huku Cathe akifuata kwa nyuma.

Nikafungua mlango wa mbele akaingia Nancy , Cathe akapanda nyuma , kipindi naelekea kufungua mlango upande wa pili nilisikia kelele , kuangalia hivi chupa imerushwa inakuja upande wangu nikajiziba uso na mikono chupa ikapasukia mikononi mwangu , watu wakamshika tena jamaa kuona hivyo nikawahi kuingia kwenye gari nakuondoka , watu wakiwa wamemshika yule jamaa asirushe chupa nyingine.

Baada ya kukata kona kama mbili huku kwenye gari ukimya ukiwa umetawala sana, nyuma nikaona gari inatufuata kwa kasi sana.

NITAENDELEA WADAU......

Similar Discussions

Back
Top Bottom