Hapo "chacha" na sio sasa.

Hapo "chacha" na sio sasa.

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,250
chui.jpeg
 
Wazungu na imani zao za kijinga jamaa lazima atakuwa kashiba..mimi ningekuwa nalia sa hiyo maana najua kifo kiko mbele..
 
Hapo badae hata izo camera zao wanaweza kuziona nzito!!!
 
Wazungu na imani zao za kijinga jamaa lazima atakuwa kashiba..mimi ningekuwa nalia sa hiyo maana najua kifo kiko mbele..
ukilia ndio wanakuja, si unaona wazungu wametulia utadhani wanyama wenzao
 
Wazungu na imani zao za kijinga jamaa lazima atakuwa kashiba..mimi ningekuwa nalia sa hiyo maana najua kifo kiko mbele..

Duma hana madhara sana kwa wanadamu, ukilinganisha na chui. Huyu ni mpole kiaina
 
Hawa wamezoea kuona watu kila siku kwenye maisha yao,kwahiyo wanajua hakna hatari hapa. Wanyama wa kwenye hifadhi za taifa wengi wakiona haya magari wataendelea na shuguli zao tu,kwasababu wanayaona kilasiku. Ndo maana unashauliwa, kwamba si vizuri kuingia mbugani na gari tofauti,kwa mfano yenye rangi nyeupe,kwani kwao ni kitu kigeni sana wanaweza kushituka.
 
Ok mimi nilijua kama chui..maana huyo hana urafiki na mtu me naogopa ata mbwa..
 
Huyo ni cheetah.. yuko friendly na sio mkorofi... angekuwa chui hapo ingekuwa ni hadithi nyingine kabisa...
 
We sema hana madhara! Kutana nae ujinyeee,,, mnyama yeyote anaekula nyama ni hatari,,,,! hizo n picha za kutengezwa
 
We sema hana madhara! Kutana nae ujinyeee,,, mnyama yeyote anaekula nyama ni hatari,,,,! hizo n picha za kutengezwa

Picha zote huwa ni za kutengeneza japo kwa njia tofauti. But that one is real... sioni cha ajabu..
 
Duma huwa hana time sana na binadamu...
 
Wote ni HATARI. Huyo Chui alikuwa anawindwa na akabanwa, akawa mkali kama kawaida ya paka akikosa pa kutokea.

Hao juu watakuwa wamefungwa na binadamu tangu utotoni na wanakuwa wameshalishwa tayari, hawana madhara hapo.

Muone huyu Mdada na Simba wake, hata hana wasiwasi. Ila wanaume, msiangalie sana kitu kisichowahusu..... hihihiii

 
Last edited by a moderator:
Mi nimeshindwa kutofautisha duma na chui mbona kama wako sawa?
 
We sema hana madhara! Kutana nae ujinyeee,,, mnyama yeyote anaekula nyama ni hatari,,,,! hizo n picha za kutengezwa

Hapana,sio picha za kutengeneza,mbona zipo hata documentary za wafanyakazi wa mbugani zinaonyesha wako karibu sana na chetah.Mara nyingi wanapanda juu ya magari hivi.
Friend of my friend alikuwa anaishi na Chetah nyumbani. Alizoeana na watu sana na muda wote alikuwa anapenda kucheza kama mbwa.Nilipomwona kwa mara ya kwanza nilishtuka sana,lakini baadae nikagundua ni rafiki tu.
 
Mi nimeshindwa kutofautisha duma na chui mbona kama wako sawa?
Duma ni warefu wembamba, nguvu chache,kilo ndogo tofauti na chui ambao wana kilo nyingi, mwili mkubwa kiasi na nguvu za kutosha.
 
Back
Top Bottom