Hapana, hapana UKAWA mnaipeleka nchi pabaya

Hapana, hapana UKAWA mnaipeleka nchi pabaya

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Mimi ni Mtanzania nasema basi inatosha ghiriba za UKAWA kutaka kuingia Ikulu kwa gharama zozote zile. Maneno yaliyotokewa leo na "Mchungaji Gwajima" na yale ya "padri" Dr Slaa, wote wana CHADEMA, si ya kupuuza kwa jinsi yanavyogusa usalama wa Taifa hili.

Chonde chonde tuyafakari kwa kina, kwani siyo tu kwamba wanajibizana tu hawa wawili bali yaenda mbali zaidi na kugusa hata imani zetu.
 
Mimi ni Mtanzania nasema basi inatosha ghiriba za UKAWA kutaka kuingia Ikulu kwa gharama zozote zile. Maneno yaliyotokewa leo na "Mchungaji Gwajima" na yale ya "padri" Dr Slaa, wote wana CHADEMA, si ya kupuuza kwa jinsi yanavyogusa usalama wa Taifa hili. Chonde chonde tuyafakari kwa kina, kwani siyo tu kwamba wanajibizana tu hawa wawili bali yaenda mbali zaidi na kugusa hata imani zetu.

Kwa nini Slaa analindwa na usalama wa Taifa?CCM wabaya kweli mlimhonga Slaa na kutumia Usalama alafu mnadhani ndiyo mnastahili kuongoza nchi,CCM ni hatari sana kwa amani ya nchi hii.

Katafakari sasa kwanza ndio uje useme UKAWA blaa blaa blaa blaa
 
Kwa nini Slaa analindwa na usalama wa Taifa?CCM wabaya kweli mlimhonga Slaa na kutumia Usalama alafu mnadhani ndiyo mnastahili kuongoza nchi,CCM ni hatari sana kwa amani ya nchi hii.

Mbona Lowassa na Sumaye wanalindwa na usalama wa taifa?hata wewe ukitishiwa amani utalindwa na usalama wa taifa na hata polisi.
 
Issue sio CHADEMA wala UKAWA. Ukweli ni kuwa CCM inatumia Vyombo vya Serikali Kisiasa, na madhara yake ni hayo. Wataipasua hii nchi hao watu. Inaonyesha wazi CCM mwaka huu imepasuka na itatumia the last possible resource kubaki madarakani.
 
Mbona Lowassa na Sumaye wanalindwa na usalama wa taifa?hata wewe ukitishiwa amani utalindwa na usalama wa taifa na hata polisi.

Umesahau ni mawaziri wakuu wastaafu? Au hujui.
 
Issue sio CHADEMA wala UKAWA. Ukweli ni kuwa CCM inatumia Vyombo vya Serikali Kisiasa, na madhara yake ni hayo. Wataipasua hii nchi hao watu. Inaonyesha wazi CCM mwaka huu imepasuka na itatumia the last possible resource kubaki madarakani.
Weka ushahidi! Tafadhari, Usiseme Gwajima kasema!
 
Dr. Slaa amekiri kuwa mchungaji Gwajima ni rafiki yake,mchungaji Gwajia hali kadhalika. Inapotokea marafiki wakaanza kuumbuana mbele za watu, ujue watu hawa wote wawili wana tatizo. Mchungaji, mara nyingi husikia siri nyingi za watu hasa waumini wake. Ikitokea mchungaji anasema juu ya muumini wake aliyemsaidia kibinadamu au kiroho mbele za hadhara ujue mchungaji huyu anapungukiwa na taaluma ya kichungaji na hafai kuchunga kondoo wa Mungu.

Biblia takatifu inasema vita vyetu si vya mwili na nyama bali vya roho. Mchungaji Gwajima anayasema haya ili kulipiza kisasi kwa yale aliyoyasema Dr. Slaa kuhusu yeye, lakini Biblia takatifu inasema' kisasi ni cha Bwana'.
Ukitafakari kwa makini kiini cha kufarakana kwa marafiki hawa tena wote wa UKAWA, ni ujio wa Edward Ngoyai Lowasa.

Siyo hawa wawili tu bali kuna makundi mengine mengi ndani ya ukawa yanatofautiana. Kwa watu wanaoona mbali wao wawili si maadui bali adui yao ni Lowasa kwa kuwa amekuja kuwafarakanisha. Hapa ndipo palipohitaji busara ya hali ya juu kutambua ni nani hasa adui yao badala ya kusema sijui Josephine sijui Dr. Slaa, sijui Gwajima.

Kama Gwajima kweli ni mchungaji wa kiroho, Roho wa bwana angemfunulia kabla hata kumkaribisha Lowasa. Angemuonya kiroho kuwa huyu anayekuja, haji kwa mema, anakuja kuwafarakanisha mtu na rafiki yake, mtu na mkewe nk nk. Gwajima anasema kazi ya mchungaji ni kuwapatanisha waliofarakana lakini anasahau kuwa hata yeye anafarakana. Mfarakani atawapatanishaje wafarakani.

Lugha wanayoongea wagomvi ndiyo hiyohiyo anayeongea mpatanishi, atafanikiwaje kuwapatanisha wengine? Mchungaji mwema ni yule anayeleta maneno matamu mahali penye maneno makali, analeta amani mahali penye vita. Katu hawezi kua mchungaji kuchochea moto wa mafarakano

Gwajima anasema walinzi wa Dr. Slaa ni walinzi wake, mpishi wa Dr. Slaa ni wa kwake. Kwa namna ya kujisifu, lakini Biblia takatifu inasema unapotoa kwa mkono wa kulia, mkono wa kushoto usijue. Ni mchungaji gani asiyeijua hata biblia kitabu kitakatifu anachotumia kuwafundishia waumini wake?

NEC ya CCM katika maamuzi yake Dodoma ilikata jina la Lowasa asigombee uraisi kwa tiketi CCM kwa sababu iliona ni mchafu. Ukawa, wakasema wao watamsafisha. Matokeo yake uchafu wa Lowasa umeanza kuwatafuna wana UKAWA tena kuanzia kwa viongozi wao wa kidini.

Harufu mbaya ya Lowasa imemrukia Gwajima, Dr. Slaa, Mbowe Tundu Lisu na itaendelea na wengine mpaka itakapowatafuna wote. Wanasaikolojia wanasema Akheri ukakaa kimya, watu watadhani unazo busara hata kama huna, kuliko kusema neno lisilofaa ukajianika ulivo mtupu kichwani.

Kirusi cha Lowasa anachoishi nacho kwa matumaini amekihamishia UKAWA
 
Narudia tena, kama hatua hazichukuliwi mapema mimi na wewe unayenitukana hatutapata nafasi tena kama hii kutukanana. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba vijana wanajengewa imani kwamba matatizo ya kiuchumi yaliyopo ni CCM, na ikiondolewa madarakani basi ni neema. Huu ni upumbavu mtupu na ufinyu wa kujenga hoja. Fikiri, chukua hatua. Nitukane unavyoweza kwa jinsi unavyoshabikia fikra hasi za kuchonganisha jamii ya Kitanzania iliyoishi kwa amani muda wote huu. Kama unaamini ni ugomvi kati ya Slaa na Gwajima, niseme umepotoka. Kama unadhani tatitzo ni CCM kama chama, hoji uadilifu wa viongozi waliotoka CCM.

Mkuu...matatizo mengi kwenye NCH hii yamesababishwa na CCM vinginevyo uniambie matatizo yakijamii tuliyonayo hayahuisiani na Utawala huu....wengine sisi tunataka CCM ikaekando kwenye huu uchaguzi wakajipange upya next election tutaweza kuwarudisha Tambueni jambo 1 hakuna MTU yyt mwenye akili timamu anaedhani SERIKALI itamletea Hela nyumbani kwake NO kinachotakiwa iweke uwanja sawa ili kila MTU apambane
 
Kabla ya Kufanyika Uchaguzi inatakiwa Mipaka yote ya Nchi ifungwe na Viongozi wakuu wote wa kisiasa Hati zao za kusafiria zikusanywe ili kama kikinuka wote tuwe humu humu ndani sio kukimbilia Nairobi kwenye Press conference kutangaza Mapambano kama 2001 pale Maalim Seif akiwa DSM huku akisema Znz tutapambana mpaka Damu ya Mwisho. Hatutaki Vita Jakaya na Lowassa jueni hivyo.
 
tuuumechokaa tumechokudanganywa na cmm.......................zimebaki siku chache sana ccm msome number!
 
Umeniharibia jion yangu ilikuwa powa yaani JF haieleweki sikui mara chungu mara tam
 
Mbona Lowassa na Sumaye wanalindwa na usalama wa taifa?hata wewe ukitishiwa amani utalindwa na usalama wa taifa na hata polisi.

Ipotofauti Kati ya Silaa na hao wengine,Lowassa na Sumaye wanalindwa na usalama wa Taifa kwa kuwa ni mawaziri wastaafu,Slaa ana lindwa na usalama wa Taifa kwa kuwa ni msukule wa CCM.
 
Mimi ni Mtanzania nasema basi inatosha ghiriba za UKAWA kutaka kuingia Ikulu kwa gharama zozote zile. Maneno yaliyotokewa leo na "Mchungaji Gwajima" na yale ya "padri" Dr Slaa, wote wana CHADEMA, si ya kupuuza kwa jinsi yanavyogusa usalama wa Taifa hili. Chonde chonde tuyafakari kwa kina, kwani siyo tu kwamba wanajibizana tu hawa wawili bali yaenda mbali zaidi na kugusa hata imani zetu.

Ha ha ha.
Kuingia Lowasaa Chadema kuna mshindo.
Waache wenyewe wanyukane pamoja na wake zao. We tulia uone shoo tu.
 
Back
Top Bottom