Hapa tutanufaika na madini au bado ni siasa?

Tasia I

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
1,223
193
Muswada madini wawabana wawekezaji wakubwa Send to a friend Thursday, 22 April 2010 23:30

dogongeleja.jpg
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja

Frederick Katulanda, Dodoma

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana aliwasilisha muswada wa sheria mpya ya madini ambao umeonyesha kufanyiwa mabadiliko makubwa yakiwemo ya kumtaka mwekezaji wa sekta hiyo kuwa na dola 100 milioni za Marekani sawa na zaidi ya Sh 137 bilioni ili aweze kuwekeza.

Kipindi kilichopita mwekezaji wa madini aliruhusiwa kuanza hata kwa mkopo jambo ambalo sasa halitakuwepo.

N geleja alisema marekebisho ya sheria hiyo hayana mana ya kuwatisha wawekezaji wakubwa ulimwenguni, bali kuinufaisha nchi na raslimali zake.

Muswada huu wa madini uliwasilisha bungeni jana baada ya kuitoa jasho serikali kiasi cha kukwama kuwasilishwa bungeni kwa siku ya pili bila maelezo kutokana na wadau kuutilia shaka wakidai kuwa haukuzingatia maslahi ya nchi.

Mbali na wadau mbalimbali kupinga muswada huo waziwazi, Waziri na Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige waliupinga muswada huo hadharani wakati wa semina ya Kamati ya Madini iliyofanyika mjini hapa wiki iliyopita.

Kitendo cha muswada huo kupingwa na viongozi wa dini na hata mawaziri kilionekana kuishtua serikali kiasi cha kusitisha kuwasilisha haraka hivyo kuamua kuutayarisha upya ili kukidhi mahitaji ya wengi.

Muswada huo uliwasilishwa Bungeni baada ya kujadiliwa kwa siku tano kuanzia Aprili 16, 18 hadi Aprili 21 mwaka huu na kufikia makubaliano ya kufanya marekebisho hayo ambayo aliyasoma Ngeleja na kuonyesha kukubaliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge wa kambi zote huku wakitoa marekebisho kadhaa ya kuzingatiwa ili ukidhi mahitaji.

Akiwasilisha muswada huo bungeni jana, Ngeleja alisema umefanyiwa marekebisho ya kutosha na wadau na hivyo umezingatia mfumo wa uingiaji mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni za uwekezaji.
Alisema katika kifungu cha 8 ndani ya muswada kimebainisha jinsi Watanzania wakavyonufaika katika uchimbaji wa madini ya vito kwa vile uwekezaji huo utahusu Watanzania tu na endapo kutahitajika wageni basi watachimba kwa ubia ambao haupaswi kupungua asilimia 50 za Mtanzania au Watanzania na serikali.

“Katika vifungu vya 10, 11 na 12 vya sehemu ya pili ya sheria hii vimegusia mikataba kati ya serikali na mwekezaji ambapo (Kifungu cha 10) kinahusu serikali kupata hisa zisizolipiwa katika kampuni kubwa za madini kwa kiwango kitakachopangwa na serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana na madini kwa mashauriano na mwekezaji” alieleza na kufafanua.

“Serikali pia kwa kupitia mashirika yake kama Stamico na NDC itaweza kununua hisa zaidi katika kampuni hizo kubwa itaona inafaa kwa manufaa ya Taifa jambo ambalo halipo katika mikataba iliyopita kuokana na sheria za zamani” alieleza.

Alisema kuwa mikataba itaingiwa iwapo uwekezaji utakuwa unafikia kiwango kisichopungua dola100 milioni za Marekeni atakazowekeza mwekezaji tofauti na sheria ya sasa.

Akielezea mambo muhimu alisema sheria hiyo, imezingatia ushiriki wa serikali katika shughuli za madini na ushiriki wa wananchi katika kuendeleza sekta hiyo na kumiliki kwa hisa za kampuni zinazochimba madini nchini.

“Serikali imeweka kipengele cha upitiaji mkataba kila baada ya kipindi cha miaka mitano na kuboresha kipengele kinachohusu uzuiaji wa mabadiliko ya kodi na ada mbalimbali kwa kiwango cha uwekezaji unaoruhusu kuwepo kwa mkataba” alieleza.

Mengine ambayo alieleza kuwa yamezingatiwa katika muswada huo ni kuanzishwa kwa makundi na kuruhusu utoaji wa leseni za uchimbaji mdogo na wa kati ndani ya leseni ya utafutaji mkubwa, kuzuia utoaji leseni ya biashara ya madini ya uranium na kutunga kanuni maalumu kusimamia shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya mionzi.

“Eneo lingine ambalo limezingatiwa na muswada huu ni kuzuia baadhi ya aina za leseni na kuanzisha leseni za aina nyingine, kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini kwa kubadili mamlaka za utoaji leseni ili kuhusisha maafisa madini wa kanda kwa utoaji leseni za uchimbaji mdogo na biashara za madini” alieleza Ngeleja.

Akisitiza kuwepo kwa mabadiliko, Ngeleja alisema kuwa muswada huo umebadilisha mfumo wa ukokotoaji wa mrahaba na kuongeza viwango kwa aina tofauti za madini ikiwa ni pamoja na kufuta bodi ya vito na kuimarisha kazi za kamati za ushauri ya madini kwa kuanzisha bodi ya ushauri.

Mara baada ya kusoma hotuba ya kuwasilisha muswada huo waziri Ngeleja alisema kwa ujumla anaitangazia dunia kuwa sheria hiyo haina maana ya kuwatisha wawekezaji huku akipongezwa na spika Samwel Sitta kuwa wasilisho la muswada huo limeweka historia nchini katika bunge hilo.

“Naomba kuutangazia ulimwengu, sheria hii haikusudii kuwatisha wachimbaji (Wakubwa) ulimwenguni bali imeandalia kutokana na kujifunza, tunayo imani dunia itatuelewa” alisema wakati akihitimisha kuwasilisha muswada huo.

Mara baada ya waziri huyo ilifuata zamu ya mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ya bunge ambayo inaongozwa na William Shelukindo ambaye alisema kamati yake imeridhika na marekebisho makubwa ambayo yamefanyika licha ya muswada huo kuwasilisha kwa hati ya dharula ingawa imetoa mapendekezo ya maeneo kadhaa kufanyiwa marekebisho.

Akielelezea Shelukindo alisema kwamba katika kamati yake wamekubaliana na kuudwa kwa bodi ya ushauri ya madini, lakini itumike kwa muda wakati serikali ikijiandaa kuunda mamlaka ya madini kama ilivyopendekezwa kwenye taarifa Jaji Mark Bomani.

Naye mbunge wa kuteuliwa na Rais Ismail Jussa Ladu (CUF) akitoa tamko la kambi ya upinzani kwa niaba ya msemaji wa kambi hiyo Mohamed Habib Mnyaa alisema bado muswada huo una mapungufu makubwa ambayo yanapaswa kurekebishwa ingawa kwa kiasi umeanza kutoa mwelekeo wa matumaini.

Alisema serikali inapaswa kuweka sheria itakayo wabana wawekezaji hao kutumia umeme wa Tanesco ama kuingia mkataba nao kuzalisha umeme wanaohitaji tofauti na ambapo wamekuwa wakizalisha nishati yao na hivyo kulikoseha mapato shirika letu.

“Jambo lingine ambalo kambi ya upinzani inaona ni muhimu ni kuhakikisha kunakuwepo kwa sheria itakazozibana kampuni kununua bidhaa za hapa nchini. Mfano ng’ombe wapo Geita je, kuna sababu gani wao kununua nyama Kenya” alieleza Jusa.

Alisema sekta hiyo ya madini ikisimamiwa vyema itasaidia kukua kwa uchumi tofauti na sasa ambapo umekuwa ukikua hewani, lakini haufikii wala kunufaisha wananchi wengi na ukiangalia sekita hiyo ya madini yenye uwezo mkubwa wa kuchangia imekuwa ikichangia asilimia 3.8 ya pato la taifa.

“Sekta ya madini inachangia asilimia 3.8 katika pato la taifa wakati katika mauzo ya nje madini haya yanachangia asiliamia 40 ya mauzo ya nje na imekuwa ikikuwa kwa wastani wa asilimia 10 kutoka mwaka 2000,” alisema msemaji huyo wa upinzani.

Hata hivyo aliikosoa serikali na kusema iwapo muswada huo utapitishwa kama ulivyo itakuwa imeshiriki kutunga sheria ya kumuimarisha mtu ambaye alimtaja kuwa ni kamishina na waziri wa madini kwa kumpatia nguvu.

“Serikali hapa inaweza kuturudisha nyuma kama ilivyokuwa kwa mamlaka aliyokuwa amepewa mkurugenzi wa wanayamapori wakati ule. Bunge linakumbuka tulipokuwa tunatunga sheria ya wanayamapori ya mwaka 2009 tuliweza kuondoa tabia hii ya kurundika mamlaka kwa mtu mmoja” alieleza.

Baada ya wasemaji hao ndipo ulifika wakati wa wachangiaji ambapo wa kwanza alikuwa ni mbunge Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye alisema amefurahisha na muswada huo na kuonya marekebisho yazingatiwe ili usije kuleta bungeni humo kwa hati ya dharula tena kama ule wa gharama za uchaguzi.

Mchangiaji mwingie alikuwa Chrisant Mzindakaya( Kwera CCM) ambaye alisema amekuwa akikerwa na kauli za kuwaogopa wawekezaji kuwa iwapo watadai raslimali zaidi watanyimwa misaada na kusema jambo hilo linapaswa kukomesha na kuondolewa kwa vile wao ndiyo wenye shinda ya kuchuma raslimali zetu.

Hatma ya muswada huo kupitishwa itajulikana leo asubuhi baada ya wachangiaji wengine kukamilisha michango yao na bunge kuwahoji wabunge iwapo wanauunga mkono.



SOURCE :Mwananchi 23-04-2010
 
Another scam
maana ukiingia kiundani zaidi tutakuja kugundua kuwa kuna sentensi zimepindishwa kuwafavor haop wakubwa wawekezaji.
 
Back
Top Bottom