Hapa nihesabu niko nje tu

Hapa nihesabu niko nje tu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Habari za weekend wapendwa,

Huyu ni rafiki yangu rafiki rafiki, lakini yeye ni wa jinsia ya pili. Tunafanya vitu vingi pamoja, mwezi wa kumi na mbili aliniambia mama yake anakuja, kwakua sasa hivi hatukai mji mmoja, tulikubaliana mama akifika nitakwenda kumuona na kumsalimia. Mwezi ule mama alipata matatizo hivyo alishindwa kusafiri, rafiki yangu alishachukua likizo mwezi Januari akae na mama yake, kwakweli nilimhurumia, January ile alishinda nyumbani mwenyewe, ilibidi atafute vishughuli vidogo vidogo ili muda uende.

Hatuna mazoea ya kuongea kila siku, ni mpaka kuwe na jambo la kuongelea, nilikuwa na issue ya kuongea nae, ninapiga ananiambia aah nitakupigia baadae nipo kwa daktari nimemleta mama. Jamani kumbe mama amefika, ehh tangia mwezi wa pili. Mmhh niliona kabisa hili ni lisilokuhusu.

Alinipigia simu baadae tuliongea vizuri issue iniliyotaka kuongea, lakini sikuulizia tena mustakabali wa mama, wala siwezi kusema ninakuja kumuona. Hii ni dalili kabisha huko upande wa pili wa tunnel hakuna mwanga.
 
Sasa kama mama yake kaja Jana na alikuwa hayuko vizuri ki afya naumesema huwa amuwasiliani kira siku ulitegemea nini kwenda kumuona utaitwa tu uende ukamuone kwani lazima akwambie leo tulia mtoto wa kike kama yako yakwako tu una haraka ya nini tulia mtoto
 
Sasa kama mama yake kaja Jana na alikuwa hayuko vizuri ki afya naumesema huwa amuwasiliani kira siku ulitegemea nini kwenda kumuona utaitwa tu uende ukamuone una haraka ya nini
mtu wake wa karibu alipaswa tu amtaarifu mapema hakuna kitu kizuri kama kumthamini na kumjali mwenziwe

alipaswa ampe taarifa mapema
 
Kuna watu don't care. Asipoulizwa kitu hasemi. Sio waongeaji na kutoatoa taarifa. Na tunaendaga mbali zaidi kufanya mambo kivyetuvyetu.
Hapana mkuu kwa jinsi ninavyomfahamu mama yeke amefika angenitumia hata ujumbe wa whatsupp. Leo ananiambia amempeleka mama madukani, nimesikiliza tu lakini hakuna mwaliko.
 
Li bichwa langu bwana eti nimeshindwa kuelewa hayo maneno ya kiswahili je ingekua kingerenge
 
Kazana ujue sababu, mwambie unaenda kumtembelea na kumsalimu mama yae. Ila alipokuwa likizo kwanini hukumkaribisha kwako au?

Jionee mwisho wake kama unampenda jua pa kumvuta.
 
Back
Top Bottom