Hapa ndipo CCM ya leo inayopumulia mashine ilipofika

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Naweza sema CCM ya leo inaangamia kutokana na watu wake ama kukosa maarifa,au kutokana na wao kukataa tamaa na sasa wanaamua waende tu hivyo hivyo ili mradi tu bado wana dola mkononi.

Kwa maneno mengine,kipimo cha namna gani mambo yao yanaenda vizuru sio tena ni namna gani wanakubalika kwa wananchi, bali ni wao kuendelea kubaki madarakani bila kujali wana political legitimacy au laa kutoka kwa wananchi.

Wakipata political legitimacy, it is well and good,ila wakiikosa,kwao sio isssue sana as long as wanachopoteza ni polical legitimacy tu na sio dola.

Matokeo ya hali hii ni CCM kufanya mambo yanayowagharimu kisiasa bila kujali matokeo yake kwani teyari inaonekana wamejikatia tamaa na sasa wanaamua kama ni kusema, basi semeni au andikeni ila wao hawajali mradi tu dola wanayo.

Ukitaka kujua ukweli huu,fanya jambo linalotishia wao kuendelea kubaki madrakani, uone utavyoshugulikiwa(mfano ni yale maandamano ya mwanadada yule wa ughaibuni ya mwaka 2018).

Hivyo,mnaposikia mtu anasimama majukwaani kipindi hiki cha kampeni na kuwaambia wananchi wataendelea kutopata maendeleo iwapo watawachagua wapinzani,huo ni ushahidi tosha kuwa wenzetu hawa hawajali tena wananchi watasema nini au watawachukuliaje, cha msingi kwao ni kuhakikisha tu dola iko mikononi mwao.

Vile vile mnapoona watu waliopitishwa kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali wanajitoa ili CCM ipite bila kupingwa licha ya siasa za hamahama na hujuma zingine dhidi ya upinzani kutoisadia CCM mpaka sasa,basi huitaji shahada kutambua kuwa kuwa sasa wamekata tamaa na hivyo wanaendeleza mbinu zile zile hata kama haziwasaidii mbele ya wananchi as long as bado wana dola.

Halikadhalka,mnaposikia viongozi waandamizi wa chama hiki wakinukuliwa kusema hadharani tena bila hofu wala aibu kuwa watatumia dola kubaki madarakani,mjue tu watu hawa wameshagundua ukweli kuwa wamepoteza political legitimacy na njia pekee waliobaki nayo ni kutumia dola kulinda dola waliyonayo na si vinginevyo.

Kwa lugha nyepesi ni kuwa, wanachofanya sasa ni kuonyesha kuwa kwakua nyinyi ndio mnajidai kuwa mnapendwa na wananchi kuliko sisi,sasa wacha tutawaonyesha hata kama wanachi hawa watazidi kutuchukia mradi tu sisi tuna dola.

Hapa ndipo CCM ya leo inayopumulia mashine ilipofika!!!
 
endelea kulamba miguu lakini mwisho wenu ni 28 octoba , mtake msitake
Sasa miguu ya mlevi wa Konyagi ndio unaona bora? Nitakukumbusha hili wala usiwe na shaka. JFYI nipo hapa JF for the last 3 elections wakati hata JF haijazaliwa. Then huyo mlevi wa Konyagi akaja na hadithi ya kutumia majina kumbe yeye ndio mwoga wa kwanza.
 
Sasa miguu ya mlevi wa Konyagi ndio unaona bora? Nitakukumbusha hili wala usiwe na shaka. JFYI nipo hapa JF for the last 3 elections wakati hata JF haijazaliwa. Then huyo mlevi wa Konyagi akaja na hadithi ya kutumia majina kumbe yeye ndio mwoga wa kwanza.
So what ?
 
Back
Top Bottom