Hivi nauliza CCM wamebadilisha utaratibu. Anayesikika ni Makonda tu

frog black

Member
Oct 22, 2023
5
4
Chama cha Mapinduzi (CCM) tangia kilipoanzishwa,Kilikuwa na utaratibu mzuri tu.Kila aliyeteuliwa alikuwa akiheshimu madaraka ya mwenzie na pia kulikuwa na ustaarabu wa kutokimbilia ovyo kwa wananchi na kuwasema au kuwahoji viongozi wenzio wakiwemo mawaziri.walikuwa wanaitana kwenye vikao baina yao kisiri na kutoka na jibu litakalowaridhisha wananchi.

Cha ajabu ninachoshuhudia ni kuwa Mheshimiwa Makonda kwa cheo chake kwa ufupi ni katibu Mwenezi tutake, tusitake. Ni kama wenezi wa Simba au Yanga.Sasa amewafunika viongozi wote wa juu wa chama,na hili ni HATARI KWA MUSTAKBALI WA CCM.

Kuna Katibu Mkuu, Manaibu wawili bara na dola ya Zanzibar, pia Manaibu Wenyeviti 2. Nchi yetu pamoja na wenzetu wa dola ya Zanzibar sisi wananchi tuna maisha magumu lakini haimaanishi utaratibu wa chama ukiukwe. CCM nawashauri mumyamazishe huyu mheshimiwa mtukufu makonda vingenevyo chama kitapasuka, sasa hivi kina ufa mkubwa. Kwa sisi watu wazima tunajua huu ndio mwanzo wa mwisho wa chama kilichotulea, kutupa elimu hadi tulipo fika hapa.

Kamwe sitasahau CCM ilivyoweka amani na utulivu hadi sasa ingawa hawa akina makonda wanataka rabsha na ukosefu wa nidhamu. Yeye akitaka basi apewe cheo kinachomruhusu kufanya.

Anayoyafanya, lakini hiki cha mwenezi hakiwezi kumpa uwezo huu. Sisi wa dola ya zanzibar na ndugu zetu wa dola ya bara tuna shida kubwa kimaisha lakini tunapenda ustaarabu na heshima kwa mwenzio.

Kidumu Chama cha Mapinduzi, zidumu fikra za mwalimu nyerere na mwenzie wa dola ya Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.
 
CCM walichotofautiana na chadema ni kwenye kupeana nafasi ….
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) tangia kilipoanzishwa,Kilikuwa na utaratibu mzuri tu.Kila aliyeteuliwa alikuwa akiheshimu madaraka ya mwenzie na pia kulikuwa na ustaarabu wa kutokimbilia ovyo kwa wananchi na kuwasema au kuwahoji viongozi wenzio wakiwemo mawaziri.walikuwa wanaitana kwenye vikao baina yao kisiri na kutoka na jibu litakalowaridhisha wananchi.

Cha ajabu ninachoshuhudia ni kuwa Mheshimiwa Makonda kwa cheo chake kwa ufupi ni katibu Mwenezi tutake ,tusitake.Ni kama wenezi wa Simba au Yanga.Sasa amewafunika viongozi wote wa juu wa chama,na hili ni HATARI KWA MUSTAKBALI WA CCM.

Kuna Katibu Mkuu, Manaibu wawili bara na dola ya Zanzibar, pia Manaibu Wenyeviti 2. Nchi yetu pamoja na wenzetu wa dola ya Zanzibar sisi wananchi tuna maisha magumu lakini haimaanishi utaratibu wa chama ukiukwe. CCM nawashauri mumyamazishe huyu mheshimiwa mtukufu makonda vingenevyo chama kitapasuka, sasa hivi kina ufa mkubwa. Kwa sisi watu wazima tunajua huu ndio mwanzo wa mwisho wa chama kilichotulea, kutupa elimu hadi tulipo fika hapa.

Kamwe sitasahau CCM ilivyoweka amani na utulivu hadi sasa ingawa hawa akina makonda wanataka rabsha na ukosefu wa nidhamu.Yeye akitaka basi apewe cheo kinachomruhusu kufanya.

Anayoyafanya, lakini hiki cha mwenezi hakiwezi kumpa uwezo huu.Sisi wa dola ya zanzibar na ndugu zetu wa dola ya bara tuna shida kubwa kimaisha lakini tunapenda ustaarabu na heshima kwa mwenzio.

Kidumu Chama cha Mapinduzi, zidumu fikra za mwalimu nyerere na mwenzie wa dola ya Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.
Umekosa cha kuandika au wewe ni chagadema
 
Back
Top Bottom