Hapa ndipo alipojikwaa Mheshimiwa James Francis Mbatia (Mb)


H

HURUMA JOSEPH

Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
69
Likes
0
Points
13
H

HURUMA JOSEPH

Member
Joined Sep 28, 2012
69 0 13
Hapa ndipo alipojikwaa Mheshimiwa James Francis Mbatia (Mb)

Na. Huruma K. Joseph
Alipokuwa akichangia hoja ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mbunge wa Kuteuliwa Mheshimiwa Mhandisi James Francis Mbatia (katika makala hii atafahamika kwa kifupi kama Mheshimiwa) aliweka wazi udhaifu katika wizara ya elimu ambayo kwa kupitia kitengo chake ya kuidhinisha machapisho na vifaa vya elimu, ilikuwa imepitisha vitabu vyenye makosa.

Mbatia alianika makosa mbalimbali kutoka kitabu kimoja baada ya kingine. Vitabu hivyo ni kile cha hisabati kinachoonyesha sifuri ukigawa kwa sifuri jibu ni sifuri, na uwepo wa hesabu za kukokotoa senti wakati katika uhalisi wa maisha ya kila siku hatuna tena mambo ya senti senti. Pia alionesha kitabu cha uraia kinachosomeka kuwa mtaa hundwa na vitongoji na kuwa wakazi wake wengi ni waajiriwa. Aidha Mheshimiwa pia alikosoa kitabu kuandikwa Jografia badala ya Jiografia. Binafsi nilimwona kupitia runinga nikiwa macho kodokodo huku Waziri na Naibu wake wakiwa wamenywea. Nampongeza kwa utafiti huo ambao kwa kiasi umedhihirisha kuwa kuna watu wanaocheza na elimu ya watoto wetu. Kabla sijaendelea naomba nitangaze msilahi katika jambo hili. Mimi ni mwandishi wa vitabu vya kiada vinavyofikia 12 vinavyotumika katika shule za Tanzania. Kitabu changu mashuhuri (si cha kiada) ni kile cha “40 Big Lies in Civics for Tanzania schools” ambacho tarehe 4/6/2013 kiliingia rasmi kwenye hansard kupitia hotuba ya msemaji wa upinzani.

Pamoja na juhudi hizo za Mheshimiwa ambazo si za kubeza, lakini bado tunahitaji tafakuri tunduizi (critical thinking) ili kujiridhisha kama alikuwa sahihi katika maeneo aliyoyagusa.

Kufundisha senti
Kwa mfano, Mheshimiwa, anasema watoto hawana haja kufundishwa mambo ya senti kwa vile hazitumiki tena siku hizi Je, ni kweli kuwa senti hazitumiki? Itakumbukwa kuwa siku hiyo hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba alitoa maelezo yafuatayo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CUF) Mh. Mhonga Said Ruhwanya “kupiga simu kutoka mtandao moja kwenda mwingine gharama imeshuka kutoka sh. 115 mwaka 2012 kwa dakika hadi kufikia sh. 34.92 Machi mwaka huu” sasa kudai kuwa senti hazitumiki unadhihirisha kuwa utafiti wa Mbatia katika swala hili ulikuwa kondefu. Je, Mbatia hafahamu kuwa katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki ulinganifu wa bei za bidhaa mbalimbali hufanywa kwa dola ya kimarekani ambazo huambatana na senti. Kwa mfano takwimu za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zinaonyesha bei ya reja reja ya Nyama ya ng’ombe kwa kilo katika nchi wanachama ni kama ifuatavyo: Tanzania dola 3.17, Burundi dola 4.14, Uganda dola 3.17, Kenya dola 3.21, Rwanda dola 2.49, wastani EAC, dola 3.24. Tukiacha hayo ya Afrika Mashariki ambayo kila siku wabunge wanasema tuwaandae watoto wetu kwenda kushindana, swali jingine muhimu ni kweli kuwa mheshimiwa hajawahi kwenda katika duka la kubadilisha fedha (Bureade Change) na kukokotoa (au kukokotolewa) hesabu yenye senti. Sasa inakuwaje aseme watoto wetu wasifundishwe mambo ya senti?


Jiografia au Jografia
Jambo jingine la kujadili ni neno lipi ni sahihi kati ya Jiografia na Jografia. Kwa mujibu wa Mheshimiwa, Neno sahihi ni Jiografia. Hapa kuna sintofahamu. Wakati kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI inalitambua neno Jiografia, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) inalitambua neno Jografia. Aidha machapisho mbalimbali yanayotolewa na Taasisi ya Elimu (TIE) mojawapo ikiwa ni MUHTASARI WA MAFUNZO YA UALIMU WA ELIMU YA MSINGI NGAZI YA CHETI, pia inalitambua neno jografia. Ikumbukwe kuwa BAKITA ndiyo chombo ambacho ni “authoritative” (kwa sheria ya Bunge) katika lugha ya Kiswahili kikiwa juu ya TUKI. Ningekuwa naandika kitabu cha somo hilo, kamwe nisingelitumia neno Jiografia. Kufikia hapo naweza nikabashiri kwamba mhandisi huyu atataka kuona neno jiometri katika vitabu vya hisabati badala ya jometri, kitu ambacho si sahihi.

Wakazi wengi wa mtaa ni waajiriwa
Si makosa hata kitabu kusomeka kuwa wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni. Kwa mfano, wakazi wengi wa mtaa wa Unga limited (Arusha) wameajiriwa katika makampuni (ujenzi, maduka, hotel n.k), viwanda (bia, uchapaji, nguo nk), ofisi za umma na wengine wamejiajiri wenyewe. Msisitizo wa mwandishi wa kitabu ni kuonyesha kuwa katika maeneo ya mjini hakuna shughuli za kilimo.

Mitala kukuza watoto kijamii
Hainishangazi nisomapo kuwa Mtala wa elimu ya awali unamwezesha mwanafunzi kukua kiuchumi, kisiasa na kijammii. Achilia mbali mtala, mbona mtoto wangu aliyeko shule ya awali makuzi ninayompa nyumbani ni ya kumpa msingi/kumkuza katika nyanja mbalimbali za maisha. Maathalani ninapomwambia asichezee chakula ninamkuza kiuchumi. Shuleni hufunzwa human relation kwa kucheza na wenzake bila kgombana huku ni kumkuza kijamii.

Jina la mwandishi kuwa kampuni ya uchapishaji.
Katika mfumo wa uandhishi wa vitabu mwandishi yaweza kuwa taasisi au shirika, hivyo mahali pa jina litaonekana jina la taasisi/shirika hilo.

Maathalani kampuni ya uchapishaji pia inaweza kuwa author kwa maana ya kutumia rasilimali watu iliyonayo. Chuo kikuu cha Harvard kinafafanua vyema hili. When a book is authored by an organization rather than an individual, put an organization name. In APA styles, if the author and publisher are the same corporation/institution, list publisher as author .

Vitabu kukosa wasifu wa waandishi
Mheshimiwa alinukuliwa akisema, “hakuna hata kitabu kimoja chenye wasifu wa waandhishi, karibu vitabu vyote havina wahariri” Mheshimiwa angefanya utafiti mdogo tu angegundua kuwa hata vitabu vya shule za msingi vya nchi mbalimbali ikiwemo zile ziliozoendelea wasifu wa waandishi kwenye kitabu si kpaumbele, na isitoshe hata vitabu alivyokuwa akitumia mheshimiwa shule ya msingi, vile vya KIBANGA AMPIGA MKOLONI havikuwa na “majisifu” ya waandishi. Vitabu vya Yusuf Halimoja ambavyo ndivyo vilivyonipa hamu ya kuwa mwandishi havikuwa na wasifu wake hadi nilipokutana naye miaka ya karibuni na kunipa historia yake. Mwanafunzi hana haja na wasifu wa mwandishi. Kwa kawaida wasifu huhifadhiwa kwenye data base ya publisher. Kuhusu vitabu kutokuwa na wahariri, mimi sio msemaje wa wachapishaji wote, wao wenyewe waje waseme lakini katika makampuni niliyoandikia vitabu wahariri ( na wasaidizi wao) wapo na ninamawasiliano nao mara kwa mara katika ku -update facts. Hata hivyo utafiti uliofanywa na TAMNGSCO (2012) haukuonyesha kukosekana kwa wahariri bali ilipendekeza wahariri hao wasajiliwe na EMAC.

Pamoja na Mheshimiwa na dhamira nzuri ya kuonyesha kuwa kuna udhaifu mkubwa katika sekta ya elimu hadi kufikia EMAC kufutwa, ukweli unonyesha kuwa hata yeye “amebugi” kwa asilimia kubwa. Mwendo kasi aliokuwa nao umemfanya ajikwae. Naomba kutoa hoja.
Huruma K. Joseph ni mwandishi mkongwe wa vitabu nchini ambaye kwa sasa anayeishi Jijini Arusha. Mwendelezo wa makala hii utakuwa katika lugha ya kiingereza katika gazeti la Arusha Times. josephhuruma@gmail.com
 
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Messages
1,809
Likes
4
Points
0
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2011
1,809 4 0
Nimekusoma vizuri na nimekuelewa, Hsasa hilo swala la jografia na jiografia.
Pia wasiwasi wangu mwingine, mheshiwa mbatiana si tu anataka kukosoa elimu yetu ili aisaidie kiwango kiongezeke bali anaonesha pia kama anachuki zaidi ya kukosoa...
 
K

Kibambaza

Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
16
Likes
0
Points
0
K

Kibambaza

Member
Joined Jun 5, 2013
16 0 0
Du mheshimiwa kweli umechambua.nakupa heko sana.
 
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,013
Likes
81
Points
145
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,013 81 145
Mpo sawa, nilidhani ni mm tuu ndio niligunduwa udhaifu aliouonyesha mh mbatia kumbe tulikuwa wengi tuliloliona hilo. Nakubaliana na wewe kuwa kuna chuki binafsi zaidi ya uchungu Elimu yetu. Ila tufanyie kazi changamoto alizozianisha tusimbeze sana.
 
Philip Dominick

Philip Dominick

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Messages
1,022
Likes
4
Points
135
Philip Dominick

Philip Dominick

JF-Expert Member
Joined May 26, 2013
1,022 4 135
duh,ila ni siasa 2 zilezile
 
M

MTK

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Messages
7,881
Likes
3,801
Points
280
M

MTK

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2012
7,881 3,801 280
Well balanced rebuttal; Wanasiasa wetu wafanye utafiti wa kina kabla ya kwenda public; short of that; they open themselves to sucker punches!!

Mh. James Mbatia Upo hapo?!
 
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Messages
16,228
Likes
4,625
Points
280
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2009
16,228 4,625 280
Mkuu umeongea kweli, mi mwenyewe nilimshangaa nikajipanga kuleta thredi humu, bahati mbaya nikapata jukumu jingine.
Yani alitamka kabisa bila kupepesa macho eti sent hazitumiki wakati ulaya na amerika na kwengineko wanazitumia licha ya technologia yao.
 
L

lukanima

Member
Joined
Apr 6, 2013
Messages
52
Likes
0
Points
0
L

lukanima

Member
Joined Apr 6, 2013
52 0 0
Very good clarification with facts! Natamani Mbatia angekuomba ushauri kabla hajatoa hoja yake.
 
scramble

scramble

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Messages
1,593
Likes
0
Points
0
scramble

scramble

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2012
1,593 0 0
Tatizo la mbatia ni kwamba ANALISHWA MANENO. huyapokea hivyo hivyo bila kuchanganya na akili au utafiti wake. nakupongeza kwa kuandika vitabu na kukosoa pale unapoona pana makosa. mimi ni mwalimu ktk shule ya msingi (English medium) hapa dar. nafundisha sayansi pamoja na social studies. nimewahi kutumia vitabu vyako vya civics na hist bk 7. licha ya wewe kuandika kitabu kinachokosoa vitabu vya wengine ktk somo la civics, na wewe vya kwako vina mapungufu. baadhi ya hayo mapungufu ni yafuatayo;

1- kitabu chako cha hist 7 kinaanza na kiraka kwenye roman I. kiraka hicho kinaonesha marekebisho ya kosa lililopo kwenye ukurasa wa 36. nimeshangaa! kumbe na wewe unakosea!?

2. vitabu vyako vya cvcs na hist 7 havina page 1! kwa nini? havina roman numbers kabla ya pg 1.

3. ktk vitabu vyako chapter one zinaanza page 2! hivi vitabu vinachapwa uchochoroni? umesema una wahariri. wamekwenda shule!?

4. sheria ya mpangiliyo wa kitabu inasema kuwa chapter ya kitabu lazima ikae kulia. vitabu vyote ulivyoviandika, chapters zinaanza kushoto. unaupotosha umma wa watanzania. watakao andika baadaye hudhani kuwa wakiiga mpangiliyo wako taifa litakua linaangamia!?

5. kwenye uk wa 10 hist 7, kuna ramani ambayo kuna mchoro rangi ya kijani ukionesha maeneo alikotawala abushiri. mchoro huo umewekwa upande wa znz licha ya kuwa abushiri hakutawala znz. huku ni kuwapotosha watoto. mchoro huo ubadilishwe.

6. ramani iliyopo kwenye uk wa 4 imeitambua Somaliland lkn ile ya 45 Somaliland haionekani. naomba ufafanuzi! kuna sehemu niliandika makosa yaliyomo kwenye hist bk

7. lkn kwa sasa hivi sioni notebook yangu. vile umeweka e mail yako nikishaipata, nitakuandikia kwa kirefu.

UPANDE WA CIVICS 7 nako kuna mapungufu yafuatayo;
1. mpangiliyo wa mwanzo wa kitabu nao umekosewa.
2. ramani ya mikoa iliyopo ukurasa wa 2 imepitwa na wakati.
3. lugha iliyotumika ktk kitabu kizima ni ngumu sana kwa wanafunzi wa drs la 7.
4. structure ya utawala wa jamhuri ya muungano iliyopo uk wa 14 siyo sahihi. haioneshi viongozi kutoka znz. makamu wa rais umemuweka upande ambao siyo wa kwake.
5. chapter two inayohusu katiba, umeiandika kwa kifupi sana on pg 22-25 licha ya kupewa vipindi 10. inaelekea unapoandika huwa huangalii upande wa periods allocated. upande huoo humsaidia mwandishi ktk kutathmini upana au ufinyu wa topic. lengo la serikali ni kwamba watoto waelewe angalau kwa wastani katiba yao. wewe umeainisha vifungu tu bila hata kuvielezea kwa kifupi. hebu angalia waandishi wenzako wa vitabu vya kiingereza na uraia kwa Kiswahili walivyo andika kwa kirefu!
6. umeandika kwenye uk wa 26 kuwa tuna aina mbili za uraia hapa nchini. hilo ni kosa. unawalisha watoto mambo ambayo siyo sahihi. tafiti kuhusu hili.
7. upande wa mihimili ya nchi, hakuna sehemu hata moja ambayo umeuliza watoto rais wa tz, spika, jaji mkuu nk...... ni nani? huoni kuwa hujalocalise topic ili watoto waelewe vizuri!?
8. matumizi ya picha ktk topics za civics ni muhimu sana! ukirevise weka picha za kutosha.
9. kuhusu jumuiya za kimataifa ambazo TZ ni mwanachama, ulipaswa kuuliza majina ya angalau makatibu wakuu wa hizo jumuiya pamoja na wenyeviti.

Maswali kama haya yanamlazimisha mwalimu na mwanafunzi kutafiti kujua kwa sasa kujua viongozi wa jumuiya hizo ni akina nani. usipoweka maswali hayo unaifanya civics iwe kama history. naomba ukirevise ufanye hivyo. wenzako unaowaponda kuwa hawajui kuandika, wameweka maswali kama hayo. angalia vitabu vya civics na uraia vya darasa la 7 uone walivyochambua vizuri.

NAAHIDI NIKIPATA NOTEBOOK YANGU NITAKUANDIKIA KWA KIREFU.
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Bongo bwana kila mtu ana lake all in all elimu yetu mbovu sana mbali ya kuwa mbatia ana mapungufu kwenye hoja zake
 
K

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
146
Likes
4
Points
0
K

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Joined Aug 19, 2012
146 4 0
Mkuu hesabu hii ndo inatumika siku hizi na wafanyakazi wengi wa serikalini kwa mwezi mshahara 200,000. ila matumizi yake kwa mwezi 1,000,000. na hana mradi wowote wa kuingiza kipato cha ziada sasa hapo ni hesabu ipi inayofaa kufundishwa?
 
Papaa Kinyani

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Messages
1,458
Likes
624
Points
280
Papaa Kinyani

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2013
1,458 624 280
Mh kweli wewe ni mwandishi, jinsi ulivyoelimisha hapo, ila Mbatia pamoja na dhamira yake ya kukosoa mfumo dhaifu wa elimu ya Tz, bado anawakilisha kwa jazba sana kama vile kuna rushwa hakupewa na wahusika fulani au amepewa taarifa ambayo si sahihi na mtu ili awaumbue watu fulani. Anyway umejitahidi James.
 
M

Mipale Steve

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
387
Likes
2
Points
0
M

Mipale Steve

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
387 2 0
Hujanishawish ki2 hapo ndugu zaid ya blaa blaa 2!
 
MITOCHONDRIA

MITOCHONDRIA

Senior Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
144
Likes
17
Points
35
MITOCHONDRIA

MITOCHONDRIA

Senior Member
Joined Feb 21, 2013
144 17 35
Acha hizo brother hata ww hivyo vitabu vyako tutavifuatilia, inawezekana na ww ndio walewale
 
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Messages
4,129
Likes
51
Points
0
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined May 27, 2009
4,129 51 0
Mbatia kajitahidi kuonesha Overview ya hali halisi japo inawezekana kakosea kuonesha mifano halisi ila tatizo lipo na hata mleta mada akiwa mkweli atakubali, hata hivyo nimependa analysis uliyofanya imekaa ki Great thinker sana inanikumbusha enzi za Jambo forum!,
 
M

majid musisi

Senior Member
Joined
Apr 14, 2013
Messages
185
Likes
1
Points
0
M

majid musisi

Senior Member
Joined Apr 14, 2013
185 1 0
Atleast ukweli umejulikana kuliko mngekaa kimya,lakini bado kuna vitabu kadhaa vinapotosha.
 
N

neyro

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2011
Messages
231
Likes
37
Points
45
N

neyro

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2011
231 37 45
kwa vile wewe ni mwandishi wa baadhi ya vitabu tajwa napita kimya hapa... maslahi kuzingatiwa!
 
Last edited by a moderator:
H

HURUMA JOSEPH

Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
69
Likes
0
Points
13
H

HURUMA JOSEPH

Member
Joined Sep 28, 2012
69 0 13
scramble

Ufafanuzi.

1. Kuulizana majina ya viongozi ilikuwa enzi za zidumu (wakati wa siasa za kutukuzana) siku hizi kaka kinacho matter ni duties and responsibilities za portifolio na sio jina la mtu, kwanza hao hubadilika kila wakati. Inaelekea bado una athari ya kutu ya kale. badilika.

2. Aina za uraia ni nne ambazo zinawekwa katika mafungu makubwa mawili (fanya utafiti) kumwambia mtoto kuna aina mbili ni sawa kufuatana na ngazi ya elimu aliyopo. (waandishi wengine husema tatu)

3. Kijani haijawekwa hadi Zanzibar angalia- wewe una makengeza.

4. Kitabu ulichonacho kiliandkwa mwaka 2010 wakati serikali haijatoa ramani mpya, baada ya serikali kutoa ramani mpya hatuwezi (na haiwezekani) kuja kuvikusanya vitabu vyote huko mashuleni ili tuweke ramani mpya. hebu tafuta kitabu hicho hicho toleo la 2013.

5. Chaper 2 inayohusu katiba imekidhi objectives za syllabus. Tatizo lako ulitaka nii-copy na ku-paste katiba nzima kama ulivyofanya wewe katika kile kitabu chako ambacho ni black and white. Syllabus inaelekeza kueleza muundo wa katiba ya JMT hicho ndicho nilichofanya. hao waandishi wenzako na wewe mmeelezea muundo au mmekopi katiba na kuiweka kitabuni?

6. Katika structure ya utawala wa jamhuri ya muungano iliyopo uk wa 14 ulitakaa nimweke makamu wa rais chini ya Waziri Mkuu, unahitaji msaada.

7. Katika mfumo wa uandishi kuna kitu kinaitwa "errata". hiyo ni taarifa ya mwandishi kumjulisha msomaji marekebisho ya uchaapaji yaliyofanya ndani ya kitabu. Hii ndiyo best practice inayoonyesha perfection na inakubalika duniani pote. kuliko kumwachia msomaji agundue.

8.Katika mfumo wa uandishi wa vitabu duniani hakuna utaratibu unaomlazimisha mwandishi aonyeshe roman number. Hivi umeshindwa kuona kuwa ukurasa wa kwanza ni YALIYOMO.

9. chapter za kitabu kukaa kushoto au kullia hapo hujaeleweka . Lakini inatosha kukuambia kuwa kuna vitabu vya india ambavyo chapter imewekwa chini ya kitabu.

Kwa taarifa yako kwa mujibu wa walimu wenzako hicho kitabu hakiwezi kushindana na chochote cha uraia drs la saba maana kimesheheni utafiti katika mambo ambayo nyie mmepotosha mf. mambo ya bunge hususani uchaguzi wa spika na muundo wa sekretarieti ya mkoa.
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,274,693
Members 490,736
Posts 30,521,144