Hapa ndipo alipojikwaa Mheshimiwa James Francis Mbatia (Mb)

Naona wote nyie hamuelewani, je kuna mfumo wowote wa uandishi unaotkiwa ufuatwe for the book to be adopted?
 
Kaka Huruma, aliyotamka Mbatia, yamekugusa wewe kama mwandishi na asssesor wa vitabu. mengi ya mambo aliyolalamikia mbatia ni kweli tupu. Hivi ni kweli wakazi wa mtaa wowote ule wameajiriwa na serikali?
 
viwe vimetajwa au havikutajwa..wewe ukiwa kama mwandishi na bado unang'ang'ania tafsiri ya wakazi wa mtaa wengi wameajiriwa,sasa nyie wote si walewale tu. huko vijijini hakuna mitaa na hao wameajiriwa au wamejiajiri.. kabla ya kuhukumu na kuandika tafiti kwanza vinginevyo unapotosha ikizingatiwa WEWE NI MWANDISHI MZOEFU. IWE ISIWE VITABU VINGI VINAPOTOSHA SASA NGOJA NKATAFUTE VITABU VYAKO NICHEKI PENGINE NAWE NI MMOJAWAO ILA HUKUTAJWA TU KUTOKANA NA VILE VILITUMIKA KAMA NI SAMPO TU.
 
.

Kaka naomba usome tena aya niliyaondika hapo juu (tatizo lako unapenda kusoma nusu sentensi) inasomeka hivi:

Si makosa kitabu kusomeka kuwa wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni. Kwa mfano, wakazi wengi wa mtaa wa Unga limited (Arusha) wameajiriwa katika makampuni (ujenzi, maduka, hotel n.k), viwanda (bia, uchapaji, nguo nk), ofisi za umma na wengine wamejiajiri wenyewe. Msisitizo wa mwandishi wa kitabu ni kuonyesha kuwa katika maeneo ya mjini hakuna shughuli za kilimo

sikusema wakazi wote wa mtaa wameajiriwa serikalini kama unavyosema wewe. Nakusihi soma tena kwa ukamilifu kaka
 
viwe vimetajwa au havikutajwa..wewe ukiwa kama mwandishi na bado unang'ang'ania tafsiri ya wakazi wa mtaa wengi wameajiriwa,sasa nyie wote si walewale tu. huko vijijini hakuna mitaa na hao wameajiriwa au wamejiajiri.. kabla ya kuhukumu na kuandika tafiti kwanza vinginevyo unapotosha ikizingatiwa WEWE NI MWANDISHI MZOEFU. IWE ISIWE VITABU VINGI VINAPOTOSHA SASA NGOJA NKATAFUTE VITABU VYAKO NICHEKI PENGINE NAWE NI MMOJAWAO ILA HUKUTAJWA TU KUTOKANA NA VILE VILITUMIKA KAMA NI SAMPO TU.

ufafanuzi.
soma mkala yangu kwa umakini. Nimesema wapo pia waliojiajiri (kama wewe hapo kariakoo). Vijijini kuna vitongoji hakuna mitaa na kwamba vijijini wanajishughulisha na shughuli gani haikuwa mada yangu. Nimeandika hivi:

Si makosa hata kitabu kusomeka kuwa wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni. Kwa mfano, wakazi wengi wa mtaa wa Unga limited (Arusha) wameajiriwa katika makampuni (ujenzi, maduka, hotel n.k), viwanda (bia, uchapaji, nguo nk), ofisi za umma na wengine wamejiajiri wenyewe. Msisitizo wa mwandishi wa kitabu ni kuonyesha kuwa katika maeneo ya mjini hakuna shughuli za kilimo

Tena naomba ukatafute vitabu vyangu haraka uvinunue ili upandishe mauzo. Asante.
 
Mpo sawa, nilidhani ni mm tuu ndio niligunduwa udhaifu aliouonyesha mh mbatia kumbe tulikuwa wengi tuliloliona hilo. Nakubaliana na wewe kuwa kuna chuki binafsi zaidi ya uchungu Elimu yetu. Ila tufanyie kazi changamoto alizozianisha tusimbeze sana.
Naomba kuuliza: je kosa dogo moja au mawili ya kiuandishi (typographic errors) yanaweza kui-discredit kazi nzima ya mwandishi? Hivi Mbatia ni technical editor au mhandisi?
 
ufafanuzi.
soma mkala yangu kwa umakini. Nimesema wapo pia waliojiajiri (kama wewe hapo kariakoo). Vijijini kuna vitongoji hakuna mitaa na kwamba vijijini wanajishughulisha na shughuli gani haikuwa mada yangu. Nimeandika hivi:
Si makosa hata kitabu kusomeka kuwa wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni. Kwa mfano, wakazi wengi wa mtaa wa Unga limited (Arusha) wameajiriwa katika makampuni (ujenzi, maduka, hotel n.k), viwanda (bia, uchapaji, nguo nk), ofisi za umma na wengine wamejiajiri wenyewe. Msisitizo wa mwandishi wa kitabu ni kuonyesha kuwa katika maeneo ya mjini hakuna shughuli za kilimo

Tena naomba ukatafute vitabu vyangu haraka uvinunue ili upandishe mauzo. Asante.
RED=hujakosea ila unaonyesha uvivu wa kufikiri halafu bado utuandikie vitabu!!?? GREEN=mnapotosha watoto wadogo BLUE=siwezi kupoteza pesa yangu kununua vitabu vya wapotoshaji..ntaenda kusoma maktabaaaa!!!! HEKO mbatiA KWA KUANIKA UMBULULA WA WAANDISHI NA EVIDENCE ZINAZIDI KUJITOKEZ HAPA.
 
Last edited by a moderator:

Ukisema maeneo ya mjini hakuna kilimo si sahihi sana. Hii ni generalization ambayo siyo applicable kwa miji mingi ya Tanzania. Kwenye mitaa na miji yetu mingi tuna watu wanapata kipato chao kwa kufuga kuku, ngombe, bata, nguruwe, kwa kulima mchicha,mahindi,ndizi, mikunde etc .........Wataalamu wa kilimo wanaiita hii kitu: urban agriculture!
 
kwa taarifa yako hivyo vitabu vimelenga kusomwa na wanafunzi wa shule zote na sio wa mijini peke yao,,sawa MWANDISHI MWANDAMIZI!!??
 
Mie kwenye hili nakwazwa na Nyangwine ambaye hana mfumo maalum unaoeleweka kiasi cha kuchanganya mada kuu/ndogo
 
Vitabu vingi vina madudu mfano URAIA drs la iii na iv swali moja majibu tofauti wakati mwandishi ni yuleyule.
 
Atleast ukweli umejulikana kuliko mngekaa kimya,lakini bado kuna vitabu kadhaa vinapotosha.

Ukisoma kitabu changu cha 40 BIG LIES IN CIVICS FOR TANZANIA SCHOOLS utaviona hiyo vitabu vinavyo potosha. Usimlaumu mtu yeyote bali wewe mwenyewe uliyemnunulia mwanao wakati vipo visivyopotosha.
 
Ukisema maeneo ya mjini hakuna kilimo si sahihi sana. Hii ni generalization ambayo siyo applicable kwa miji mingi ya Tanzania. Kwenye mitaa na miji yetu mingi tuna watu wanapata kipato chao kwa kufuga kuku, ngombe, bata, nguruwe, kwa kulima mchicha,mahindi,ndizi, mikunde etc .........Wataalamu wa kilimo wanaiita hii kitu: urban agriculture!

Hata mwandishi ambaye Mbatia anamchallenge haku -generalize, ndiyo maana ameandika wakazi wengi (sio wote) wa mtaa ni....... Kwa mtazamo wako shughuli kuu za kiuchumi hapo kariakoo ni kufuga nguruwe? hebu funguka. Halfu mbona umeng'an'gania hiyo hoja wakti nimejadili vipengele vingi?
 
Siwezi kusema kama Mbatia kajikwaa au la, ila amenga'ng'ania manyoya. Yako mambo makubwa zaidi ambayo angeweza kushughulika nayo. Haya mambo ya jometri na jografia nadhani ndiyo matamshi sahihi kutokana na BAKITA. Ila ni kweli vitabu vingi vina factua errors here and there kiasi kwamba hawa waandishi wengine wanalalamika kuwa ilikuwaje vitabu hivyo vikaingia kwenye school sytem. Kama kitabu kina factual arror kinatakiwa kiwe na sahihisho au kiondolewe kwenye system. Mbatia angekomalia hapa. Viko vingi kuliko hata hivyo alivyovisema Mbatia. Ukitaka kufuatilia hili tafuta vitabu vya sayanasi nadhani DRS la nne -sita. Hapa ndipo utagundua kuwa tatizo lilikuwa ni EMAC kukwepa majukumu yao na kuyaacha kwenye EMAC Secretariat peke yake.

Kimsingi kulikwepo na mkanganyiko mkubwa sana kwenye EMAC na secretariat yake. Kutokana na ufinyu wa bajeti wataalamu waliokuwa wakipitia manuscripts au vitabu hawakuwa makini kwa kuwa hawakuwa na muda wa kupitia manuscript au kitabu chote. Walikuwaa waki-sample pages jambo ambalo ni kosa kubwa. Inatakiwa kitabu chote kipitiwe. Lakini pia inawezekana hata wataalamu hao hawakuwa na ujuzi wa font ipi itumike kwenye level ipi ya elimu. Hata kama hiyo EMAC imevunjwa, kama watu hawatakuwa waadilifu, bado cheap quality books vitaingia kwenye school system. Lakini kama walimu wa elimu ya msingi watafundishwa kitabu kizuri kikoje bila shaka mengi ya matatatizo haya yataondoka. Unaweza kushangaa walimu wakuu kununua vitabu ambavyo siyo original kwa kukosa tu ufahamu sahihi. Labda sasa kwa kuwa kutokana na change ya rada vitabu vimenunuliwa centrally, pengine itasaidia. EMAC was a problem nakubaliana na Mbatia. lakini pia hata siasa ilichangia kwa sehemu. In addition, kukosekana kwa uadilifu kwa baadhi ya wajumbe wa secretariat ya EMAC kulichangia vilevile huo uozo. How many titles will be removed from the school system? God knows.
 
kwa taarifa yako hivyo vitabu vimelenga kusomwa na wanafunzi wa shule zote na sio wa mijini peke yao,,sawa MWANDISHI MWANDAMIZI!!??

ufafanuzi
Hiyo aya ilikuwa inaelezea mambo ya mjini, ipo pia iliyokuwa inaelezea maswala ya vijijini. Katika uandishi huwa hatuchanganyi mambo kaka. Halafu mbona hujadili hoja nyingine nilizowasilisha? hii inaonyesha umeunga mkono asante.
 
Vitabu vingi vina madudu mfano URAIA drs la iii na iv swali moja majibu tofauti wakati mwandishi ni yuleyule.

ufafanuzi

Ni kweli si swali moja ni mengi sana. Tafuta kitabu changu cha 40 BIG LIES IN CIVICS FOR TANZANIA SCHOOLS nimeainisha makosa hayo. Tatizo lenu walimu hamtafuti vitabu bookshop mnasubiri mletewe shuleni na kushawishiwa kuvinunua bila kujua kibaya chajitembeza halafu mnakuja kalalamika.
 
scramble

Mkuu tupo pamoja, nakuunga mkono kwa 100%

Kama huyu ndo anasahihisha wenzake halafu ni kilaza hivyo ndo maana zero zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Ninachofahamu ni kwamba Wizara ya Elimu imeundwa kwa ajili ya kuendeleza elimu nchini lakini kama wanatumia vitu vyenye makosa namna hiyo wanatakiwa kulaaniwa na kila mpenda maendeleo katika nchi hii maana wanalipwa kodi zetu ili wawe makini lakini wanafikilia vidosho hao.

Kuhusu BAKITA mimi naona kama kijiwe fulani maana sidhani kama kazi waliyoitiwa kwa maana ya malengo ya kuanzishwa kwake ni hiki wanachokifanya lasivyio tunahitaji mamlaka nyingine ya kuendeleza lugha hii. Hili baraza limeshindwa kabisa kuendeleza lugha hii ndiyo maana mjadala uliopo kwa sasa ni lugha ipi itumike katika kufundishia ambapo walio wengi wanaonekana wanaunga mkono Kiingereza kutokana na kushindwa kwa baraza kukiendeleza Kiswahili.

Naona ni heri kutumia nondo za TUKI angalau wanafanya utafiti kuliko hawa jamaa bongo lala. Mbatia siyo mwalimu na wala siyo Waziri wa Elimu alichofanya ni kuifungua Wizara na jamii kwa ujumla ili wajue madudu yanayoweza kuchangia mdororo wa elimu nchini. Huyu jamaa katika analysis yake kaegemea upande wa vitabu mboana hasemi mengine? au na yeye alipata 'O' akaunga unga kwa msaada wa Kawambwa?
 
Last edited by a moderator:
RED=hujakosea ila unaonyesha uvivu wa kufikiri halafu bado utuandikie vitabu!!?? GREEN=mnapotosha watoto wadogo BLUE=siwezi kupoteza pesa yangu kununua vitabu vya wapotoshaji..ntaenda kusoma maktabaaaa!!!! HEKO mbatiA KWA KUANIKA UMBULULA WA WAANDISHI NA EVIDENCE ZINAZIDI KUJITOKEZ HAPA.

Acha jazba. Ninakubaliana na hoja ya Mbatia ndiyo maana nimewahi kuandika kitabu kinachoelezea makosa mbalimbali katika somo la uraia ambacho hata msemaji w aupinzani alikinukuu. (Waziri na Naibu wake wanacho hicho kitabu) Tatizo ni kwamba hujasoma makala yangu yote kwa sababu ya uvivu wako wa kusoma. Huko maktaba utakutana na vitabu vyangu hata uende uingereza (longman) utanikuta. Futa hilo povu kaka.
 
Vitabu vingi vina madudu mfano URAIA drs la iii na iv swali moja majibu tofauti wakati mwandishi ni yuleyule.

si swali moja tu yapo mengi. Tafuta kitabu changu cha 40 big lies in civics for Tanzania schools utayaona mengi. Tatizo nyie walimu hamtafuti vitabu bora mnasubiri vya kuletewa hapo shuleni na kushawishiwa badala ya kwenda bookshop.
 
Back
Top Bottom