Hapa natapeliwa au?

Hapa natapeliwa au?

Superboy

Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
45
Reaction score
6
Kuna mdada wa senegal alikimbia vita liberia yupo senegal kwenye camp ya wakimbizi sasa kuna pesa ziliachwa na wazazi wake bank ya scotland na kwenye urithi aliandikwa yeye. Siku akatuma maombi ya kuzitaka hizo pesa bank wakamwambia atafute mtanzania ili pesa zi hamishiwe kwa huyo mtanzania. Halafu atafute mwanasheria aliye sajiliwa wa senegal akaingia fb akaniona akanitumia email tukawasiliana fresh akanipa anwani za hiyo bank nilipowasiliana nao wakasema nitafute hati ya kiapo kwa mwanasheria wa senegal nikamwambia yule mdada akaniunganisha na huyo mwanasheria sasa anataka$700 ili aniandikie ampe huyo mdada asaini hiyo hati yenye details zangu ikiwemo akaunt yangu ya bank na apeleke kule bank na benk wanasema wakiipata tu hiyo hati na vyeti vya kifo cha huyo baba yake mdada wananitumia hiyo hela hapohapo halafu yule mdada aje aichukulie kwangu na kuna asilimia ananiachia. Kila kitu kimekamilika bado hiyo hati tu na kuipata inatakiwa nimtumie mwanasheria $700. Kinachonitia wasiwasi mbona kila kukicha wanaoniomba niwasaidie inshu kama hii wanaongezeka kila kukicha.
 
Hahahaha! Ncheke miye!! Huyo binti anaitwa nani?anaanzia na M???
 
hongera!!

kuna wenzio zaidi ya mia moja wako kwenye systemkama hiyo hiyo!

hebu jiulize, hivi senegal nzima hakuna watu wa kucheza function kama yako?

kaka huyo ni dude wa Dakar!

mwambie akutumie kwanza wewe dola 100 ucheki upepo!
 
Hao ni matapeli wanatuma msg fb ila wanataka muwasiliane kupitia emal, kimbia haraka sana.
 
Mwenyewe ukaona zali la mentaliiii? We hujiulizi yeye ana ndugu wangapi asiwape wao akupe wewe ambaye hata hamjuani......ha ha ha!!! Changa la macho hilo
 
Jamani mkuu upo dunia ipi haujawai pata hizo barua au e-mail? Ukituma hiyo pesa ndo basi na ukitoa acc yako ya bank iliyo active usijeenda kuuliza bank pesa yako imekwenda wapi.
Kuna siku utakuja kupata ujumbe kuwa rafiki yako au ndugu yako wa karibu yuko nchi fulani na amepata tatizo anahitaji pesa ni utapeli mwingine usiulize wanajuaje e-maili yako na wamepataje fahamu uhusiano wako na huyo mtu.
Ni matapeli mimi ilishatokea wametuma kuwa baba angu anahitaji msaada yupo uingereza pia kua rafiki yangu anahitaji msaa baada ya kuvamiwa huko uingereza.
Kuwa makini.
 
Ni utapeli wa kitoto sana. Kama ukinasa kwenye mtego kama huo basi tena kila aina ya utapeli utakuwa unakunasa bila ya wasi wasi.
 
mwenzenu keshampa bank details zake longgggg
 
utakuwa ndo umejiunga na facebuk nini?hawa matapeli wapo wanabahatisha kumpata atakayeingia kingi,watch out!😀
 
Back
Top Bottom