Hapa kwa 99% Magufuli amechemka

Forgo

Member
Apr 7, 2016
27
60
Mwanzo ilisikika JPM hashauriki ikaishia hewani ila leo amejidhihirisha wazi kwa watanzania wote kuwa yeye "Hashauriki" nanukuu "Mpaka watu wengine wanaingilia Uhuru wangu, Mimi huyu uniingilie?, Ukiniingilia ndiyo umeshapoteza kabisa, Mimi huwa sipangiwi mambo.... Hakuna mtu wakuniambia fanya hivi na Mimi nikafanya.... "Hata fomu ya kugombea niliifata mwenyewe, hakuna aliyenishauri kwamba fata fomu" - JPM.
Hii ni wazi kwamba bwana mkubwa hashauriki na mara zote mtu asiyeshaurika huwa mwepesi sana kurubunika, nawapeni mifano hai ya kurubunika kwake JPM mingine mtafuatilia watu wa aina hii kwenye jamii zenu.
*Kwanza* Aliwai kukusanya pesa za kutosha huku TRA wakivuka lengo la makusanyo kila mwezi ghafula akaja Rais wa Rwanda Paul Kagame akamrubuni kununua ndege (Bombardier pia unaweza ziita Panga Boy) na pesa zote akazimwaga kwenye manunuzi ya ndege na ujenzi wa kiwanja cha ndege nyumbani kwao Chato. Matokeo yake pesa imekosekana serikalini, pesa imekuwa ngumu mitaani, uvukaji lengo TRA ukapotelea kusikojulikana, Boss wa TRA aliyekuwa akiongoza makusanyo ya kuvuka lengo akafukuzwa kazi na juzi tu mmemsikia CAG akilia ukata.
*Pili* Aliwai rubuniwa kwamba Tanzania inaweza kujitegemea sababu tuna Bahari,Maziwa,Mlima,Mbuga za wanyama,Madini,Gesi,Mafuta na sisi wenyewe kwani kitu gani!!?, akajifaragua kutoa maneno ya kejeri kwa nchi wahisani nanukuu "Ni heri kushindia mihogo kuliko mkate wa masimango, kwanza Tanzania ni nchi tajiri sana, serikali yangu haiwezi kukopa kopa". Ghafula hali ikabadilika na Matokeo yake akageuka ombaomba asiye na staha yani ombaomba anayeomba hata "mate"... Si mnamkumbuka mfalme wa Morocco? Aliombwa mpaka nayeye akaamua aombe kuongeza siku za kuwepo hapa Tanzania na sijui kama ameshaanza kutujengea Uwanja na Msikiti, sijui!.... Kuaibika kwa kuomba alirejea "Mikoponi" na hata leo mumemsikia akifurahia mkopo toka Bank ya dunia.

***************************

Jambo jingine ni kwamba Tanzania hatuna Kiongozi wa nchi, huyu aliyepo ni Mtawala (Mtemi).

Tuelewane.....
Kiongozi huwaongoza watu wake kwa kila jambo na hawezi kuwa msaliti pale mambo yakienda kombo... Ni dhahiri mtemi JPM alianzisha vita ya usafishaji aliyoibatiza kwa jina "Tumbua Majipu" na kuwafuta kazi watumishi wote wa serikali waliobainika kugushi vyeti au kudanganya kwa namna moja ama nyingine katika taaluma zao na hata waliokuwa wanafanya udanganyifu wa aina yoyote kwenye ajira zao... Walikuwepo walioshauri na kudai zoezi halifuati taratibu za utumishi wa umma lakini wapi!!,,,, ilifika mahali wateule wa Mtemi (Ma-RC na Ma-DC) nao walijawa ujinga na kugeuza kauli zao kuwa sheria ya kuwafukuza kazi waajiriwa wa serikali bila kufuata taratibu, lakini kama nilivyoeleza awali huyu bwana mkubwa hashauriki na hivo hakusikia kitu... Vita hii ilifika ukingo pale alipoibuka Mtanzania mmoja kwa jina la Benard Focus Saanane aliyeanza kuhoji uhalali wa PhD ya mtawala Rais na kutaka naye ahakikiwe elimu yake... Ajabu kuanzia hapo haikusikika tena takwimu ya walioitwa wafanyakazi hewa (Ghost workers) iliyokuwa ikitolewa na Mtemi kila mwisho wa mwezi..... Kilichosikika ni kutoweka kwa Mtanzania huyu aliyeanzisha kampeni ya kuhoji uhalali wa elimu ya Mtawala... Hatuwezi jua kwa undani swala la kupotea kwa Mtanzania mwenzetu ila inatia shaka kwa namna ambavyo utawala wa mtemi ulivyolibeba jambo hili.
Na hadi kwa wakati huu kuna RC aliye na tuhuma za kughushi vyeti lakini huyu ninayemuita mtawala(mtemi) haoni kibanzi kwa jicho lake... Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,,, masikini waliofukuzwa kazi kwa kughushi vyeti bila kupewa hata nafasi ya kujieleza kwa taratibu za kiutumishi nao ni Binadamu, nao ni watanzania wanaohitaji haki. U-RC usiwe kigezo.

Kingine......
Mfano hai wa mtawala, ni juzi tu amesikika mtawala Rais akipiga simu kupongeza Clouds TV Kituo cha television na kudai amefurahishwa na kipindi cha Umbea maarufu kama SHILAWADU, Yeye kama kiongozi akawa njia ya sisi watanzania kuifuata.... What next?
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyeghubikwa na kashfa lukuki ikiwemo kughushi vyeti,kupokea rushwa(hongo) na matumizi mabaya ya office alionekana kuandaa saga ya kumdhalilisha mtu kupitia kipindi hicho cha wambea kinachofuatiliwa na watanzania wakiongozwa na Mtawala Rais... Saga hiyo ilikataliwa kurushwa hewani na uongozi wa Clouds TV kwa madai ipo kinyume na maadili ya wanahabari. Ndipo RC huyo akaamua kutumia nguvu ya dola kuvamia kwa mitutu ya bunduki ili kutimiza azima yake ya kuwafurahisha wafuatiliaji wa umbea ndipo akachukua nakala ya video kwa nguvu na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kwasababu haikurushwa na kituo hicho cha television.
Baada uvamizi huo wa kutumia silaha Taifa lilisimama kungojea uamuzi wa Rais kama kiongozi wa nchi juu ya huyu RC...

Lakini kabla napenda kuweka mambo sawa.... aliwai sema Tundu A. Lissu Rais wa TLS, nukuu "Sijapata kuona Rais wa ajabu kama huyu JPM, narudia, hajawai tokea Rais wa ajabu kama huyu tuliyenaye".

Leo amesika Mtawala Rais akisema "Watanzania tumejikita sana kwenye maswala ya umbea ambayo hayatupunguzii njaa, hayatupunguzii umasikini wala hayatupunguzii matatizo ya elimu. Mnajisumbua na vipost vyenu kana kwamba mnanipangia mimi nini cha kufanya".... Aaaaaaah!!!!

Mtawala Rais, wewe hukuwa wa kwanza kuushangilia umbea!?, Hadi kupiga simu za pongezi kwenye kipindi cha umbea?... Kwanini leo unawasaliti watanzania baada tu ya kuona RC wako kipenzi amekiuka maadili ya utumishi kwa kuvamia kituo cha television akiwa na askari wenye silaha za moto?.

Wewe siyo Kiongozi, wewe ni Mtawala....

Sichoki kuandika naomba kuangusha kalamu....

Forgo #JF
 
1051c77327de28728c8e58bf7739cb6e.jpg
 
Fanyeni kitu haya mabandiko hayatabadili kitu
 
Back
Top Bottom