Hapa Kazi Tu

Kama walifanya pamoja,mbona unasema alifanya peke Yake.
Ndio maana nikakwambia wewe uko nje ya mada kwa sababu umevamia usichokielewa.

Huwezi kumtenganisha Magufuli na Samia katika miaka 6 ya awamu ya 5.

Sema tu nyie Waha wa ACT wazalendo ni wabishi wa kuzaliwa.

Samahani lakini!
 
Utaelewa tu.Unabadilisha gia angani.Mbona mwanzo,hukumjumuisha Mama Samia,katika hiyo miaka 6.
Zitto Kabwe ana kazi kubwa sana kuwaelimisheni aiseee!

Duh.......Chadema kuna mbwiga lakini ACT wazalendo sijui mawese yamewafanyeje!

Ligi na Waha siiwezi, ulale unono!
 
Kuanzia mwaka huu... tarehe 17.3 na kila mwaka ya tarehe hiyo, itakuwa SIKU MAALUMU YA KITAIFA...KUADHIMISHA na kumshukuru Mwenyez Mungu kwa maisha ya Kiongozi na Mzalendo John P. Magufuli.
 
Kila Rais amefanya yake,na matunda yanaonekana.Mwalimu Nyerere alipigania Uhuru,na akahakisha nchi zote za kiafrika na zisizo za kiafrika zinakuwa huru,kama vile Palestina na nyinezo.Na alifanikiwa.Akaja Mzee Mwinyi,Yeye alirudisha uwekezaji,biashara,mzunguko wa pesa,na akajenga alivyovijenga.Akaja Mkapa,akaleta heshima kwa waajiriwa ,akajenga alivyovijenga.Akaja Kikwete akapandisha mashahara,akajenga mabarabara,mashule,mahospital nk.Akaja Magufuli ndio hayo unayoyataja,Kaja mama na yeye tunayaona yake,mashule,mahospital,barabara,reli,nk anamalizia na kujenga mapya.Yote ni mambo ya CCM(Nambari One)
 
Badala uwapongeze WATANZANIA kwa moyo wao mzuri wa kulipa kodi.

Hiyo miradi yote ni jasho la watanzania wala siyo pesa ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…