Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Uko vzr mkuu mawe yapo nyumban ya kutosha inaonekana
Aah, wapi ndugu yangu.Wote watoto wa kusomeshwa na Nyerere kwani tunachekana basi?

Kama tumepishana wote tumegawana umasikini tu.

Ndiyo maana nikaamua kukimbilia kwenye ligi kuu kwa kina Elon Musk, Jeff Bezos na Bill Gates huku.

Nikikaa Bongo sichelewi kubweteka kujiona mtoto wa Oysterbay, nikija huku natia akili kumkichwa watu hawaijui hata Tanzania iko wapi katika ramani, sembuse Oysterbay ya Bongo.
 
Kaka sisi wengn madream yet ni kufika ht US tunajikuta tunaishi buza kwa mpalange au kariako tukijitahid san bhas et zanzibar
 
Kaka sisi wengn madream yet ni kufika ht US tunajikuta tunaishi buza kwa mpalange au kariako tukijitahid san bhas et zanzibar
Huyo Bakhressa aliitoa hapo hapo Bongo hata US kama kufika kafika baada ya ubilionea.

Very humble man.

Maisha popote kaka.

Tena Bongo inawezekana ndiyo kukawa na uwanja mpana wa kupiga mingo vizuri hakuna wajanja wengi, huku kuna wajanja wa kila kona ya dunia wamejazana.

Kuitoa ile kimasomaso lazima upige hesabu za ziada.
 
bongo changamoto ni nyingi sana mkuu yaani hata hizo hand to mouth hazipatikani na sisi tunaotamani US tunataka kidogo tu ambacho kibongo bongo hakipatikani
 
bongo changamoto ni nyingi sana mkuu yaani hata hizo hand to mouth hazipatikani na sisi tunaotamani US tunataka kidogo tu ambacho kibongo bongo hakipatikani
Nakuelewa mwana.Shuta shuta mwendo wa ngiri pelaso la bongo nuksi nalijua.

Yani kuna wakati mtu huchelewi kuunga mkono Azimio town mpaka Sinza kwa sababu nauli imeflet apeche alolo.

Lakini mtoto wa kiume unakomaa mpaka one day yes.
 
Siku hizi wanakata kata viwanja.

Hiyo nyumba ya Bakhressa pale zamani lilikuwa shamba la mchicha la Shule ya Msingi Oysterbay.

Oysterbay siku hizi imekuwa ovyo sana wameweka mpaka gereji za magari, last time nilipofika nikashangaa barabara zilikuwa mbovu sana, pale shuleni.

Sijui kama sasa hivi wametengeneza.

Baada ya moratorium ya Mkapa ya kuuza nyumba kupita it will get even worse.
Hapo ni kwa mtoto wake.
 
Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.

Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.

Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.

Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.

Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.

Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.

Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.

Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.

Watoto wake wakakasirika sana.

Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?

Baba yao akasema ameshaamua.

Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.

Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.

Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.

Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.

Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.

Ukikipata unapata balaa.
Well said. Ingawa ni bora uishi sehemu nzuri kwa muda mfupi kuliko kuishi miaka mingi sehemu ya kichoko.
 
Back
Top Bottom