Kuna bloggers wasafi wanaopiga $2,000+ hapa bongo ?

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Nipo interested na mambo haya ila nilipotaka kufatilia nilikuwa nazungushwa sana, nikaja kugundua kwamba hii kazi ya blogging wanaotusua ni wale wanaotumia njia nyeusi na ndio mana hawapo open.

Bloggers wa mikato hawa wala haishangazi kuchapa hata dola 2,000+ kila mwezi japo huwa ni wasiri mno, mtu wa kawaida huwezi kujua hata kazi anayofanya, we utaona tu jamaa yupo ndani lakini ana usafiri, apartment ya laki 4, mtoto anasoma shule private, mke anapiga shopping za maana, n.k.

Binafsi napenda zaidi blogging safi ambazo hata siwezi kujitambulisha kwamba mimi ni blogger na naweza kumuelekeza mtu kila nachofanya bila hofu,

Tatizo linakuja kwamba hizi blogging safi unakuta mtu anaambulia dola 300, ila pengine labda utafiti wangu haukugusia maeneo ambayo siyajui ningependa tujadiliane.

Je, Tukiachana na bloggers maarufu kina millard Tza, hizi shughuli ukifanya kihalali bila njia nyeuse kuna uhakika wa kufika walau dola 1,000 ili kuifanya blogging iwe side hustle au hata ajira rasmi ?


Bloggers wa hapa bongo wanaopiga pesa wanafanya kazi kwa siri maana process ya kupata hio hela ni chafu.

1. Wanadukua account za fb, hapa huwa wanatengeneza website inayofanana na facebook sehemu ya kuingiza username na password, ukiingiza zinaenda kwao, wanatumia account yako. huwa wanatega hizi wensite feki kwenye magroup ya fb wanaposti picha kitu cha kuhamasisha mtu afatilie zaidi, wanadanganya ukitaka kuona zaidi minya sehem flani, ukiminya inatokea hio website feki, ukiingiza password zinanaswa.

2. account hii inaanza kutumiwa kushare picha kama hizi kwenye magroup

baka.PNG


Wanaongeza kitufe cha kucheza "play button"

baka.jpg


Hapo wanaanza kushare picha hii wanaambatanisha na link za blogs zao kwamba ukitaka ucheze hio video inabidi uingie blog yake utazame

Ukiingia hio blog hakuna chochote humo, umeshamuingizia shilingi 20, kwa kila watu elfu moja anapata elfu 20 kwa hapa bongo, kwa kenya elf 30, afrika kusini ndio wanakupenda zaidi maana kule watu elf 1 inaenda elf 50 hadi 80,

watu wamejifungia ndani humo kwenye apartment mtu anatandika laki 3 sio masikhara.
 
Blogging kwa bongo ni ushuzi mtupu bora ukalime asee

Why
1.Blog ili uingize mapato itabidi uwe na Traffic(watembeleaji,) wengi sasa watumiaji nao wanatofautiana

Mfano:Nchi kama USA,UK wanaCPA kubwa ukilinganisha na Nchi zinazojitafuta kama TZ yani hapa namaanisha CPA ni kiwango utacholipwa kwa watu 1000

Hivyo kwa watu 1000 wataotembelea blog yako wakiwa USA,UK utalipwa $1+ ila kwa watu 1000 wataotembelea blog yako wakiwa nchi zenye CPA ndogo utalipwa kama $0.5 tu kwahiyo utahitaji watembeleaji zaidi ya Millioni kwa siku ili upate walau $100 sasa kwa niche gani uliyonayo mpaka upate wasomaji Millioni??

Hata kwa blog kubwa kama za Millard ayo sidhani kama anatengeneza pesa ndefu kihivyo blog ni ngumu mnooo.mnoooo
 
Blogging kwa bongo ni ushuzi mtupu bora ukalime asee

Why
1.Blog ili uingize mapato itabidi uwe na Traffic(watembeleaji,) wengi sasa watumiaji nao wanatofautiana

Mfano:Nchi kama USA,UK wanaCPA kubwa ukilinganisha na Nchi zinazojitafuta kama TZ yani hapa namaanisha CPA ni kiwango utacholipwa kwa watu 1000

Hivyo kwa watu 1000 wataotembelea blog yako wakiwa USA,UK utalipwa $1+ ila kwa watu 1000 wataotembelea blog yako wakiwa nchi zenye CPA ndogo utalipwa kama $0.5 tu kwahiyo utahitaji watembeleaji zaidi ya Millioni kwa siku ili upate walau $100 sasa kwa niche gani uliyonayo mpaka upate wasomaji Millioni??

Hata kwa blog kubwa kama za Millard ayo sidhani kama anatengeneza pesa ndefu kihivyo blog ni ngumu mnooo.mnoooo
Kwenye blogging kuna ujanja wa kuongeza mapato

Matangazo tuliyoyazoea kuyaona kwenye blogs ni hizi banners yale mabango, aina hii ya matangazo inabidi uwe na traffic kubwa sana ili upige pesa, mfano ni blogs maarufu za muziki, blogs za ajira na hata hapa jamiiforums kuna muda yapo, hapa unakuta kwa siku watembeleaji ni laki 1 inaingia laki na 20.

Sasa kuna aina ya matangazo yanaitwa direct link, haya ndio matangazo yenye pesa zaidi kuliko banners / mabango yale ya kuweka kwenye blog, hizi direct link ndio zenye pesa zaidi, kuna tricks za kuitegesha mtu aminye, watu wlf 1 wakiminya kwa hapa bongo tu ni elf 20, sauzi elf 60 hivi, huko marekani inakimbiza hadi laki na nusu. kupata traffic ya matangazo haya ni ngumu, ni ujanja ujanja wa kuzitega hizo links, inabidi uwe karibu na hao bloggers ndio unazijua tricks za kisasa.
 
Na ndomaana mpaka leo cryptosystem haieleweki maana wasomi wetu wameshindwa kujenga hoja za kusonga kidigital
 
Huu ujinga wako ndo mana hupewi mbinu,eti blogger wachafu Utaishia kulaumu watu sijui wasiri.Kama unapenda usafi kwanini na wewe usipambane uwe kama Millard?
 
Nafikri Blog yako niche yake ikitarget audience wanaozungumza lugha ya English , itatisha zaidi.. na pia usitegemee Ads pekee.. , blogs nyingin hata za nje wanapiga hel pia kupitia affiliate marketing

Based on your niche!
Kwenye post zako zingatia affiliate marketing ili uweze kupata commission
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom