Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Usiku ulikuwa mrefu, hatimaye kumekucha. Katua, kanaswa! Wanaye...
Tutarajie nini kitafuata?
========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (13:30hrs)
========
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa Mahakama ya Kisutu kujibu mashtaka 10 yanayomkabili
========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (9:30am)
========
Baada ya kumsaka kwa muda mrefu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.
Takukuru imemkamata Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hanspoppe alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.
Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.
“Na vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata. Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani kesho (leo).”
Pamoja na Hanspoppe, mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Franklin Lauwo ambaye naibu mkurugenzi huyo wa Takukuru alieleza kuwa amekwishawasiliana nao na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya kurejea nchini akitokea Pakistan.
Hanspoppe ataunganishwa katika kesi inayomkabili rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ya madai ya kughushi na utakatishaji fedha ambayo inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam