Hanspope atua katika ‘Mikono salama’; Mahakama ya Kisutu yamwachia kwa dhamana...


Invisible

Invisible

Admin
Joined
Feb 11, 2006
Messages
9,104
Likes
602
Points
280
Invisible

Invisible

Admin
Joined Feb 11, 2006
9,104 602 280
Usiku ulikuwa mrefu, hatimaye kumekucha. Katua, kanaswa! Wanaye...

Tutarajie nini kitafuata?

========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (13:30hrs)
========
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa Mahakama ya Kisutu kujibu mashtaka 10 yanayomkabili

========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (9:30am)
========

Baada ya kumsaka kwa muda mrefu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Takukuru imemkamata Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hanspoppe alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.

Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.

“Na vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata. Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani kesho (leo).”

Pamoja na Hanspoppe, mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Franklin Lauwo ambaye naibu mkurugenzi huyo wa Takukuru alieleza kuwa amekwishawasiliana nao na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya kurejea nchini akitokea Pakistan.

Hanspoppe ataunganishwa katika kesi inayomkabili rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ya madai ya kughushi na utakatishaji fedha ambayo inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
 
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
6,582
Likes
11,568
Points
280
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
6,582 11,568 280
Ukishakuwa mbongo ni mbongo tu. Mtu kawatoroka vizuri kapanda mpaka basi la abiria kupitia Nairobi sasa karudi tena? Yan kwa jiwe atakaa mahabusu miaka 7. Amejinyea mwenyewe
 
kalemauji

kalemauji

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2014
Messages
592
Likes
367
Points
80
Age
36
kalemauji

kalemauji

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2014
592 367 80
pengine alidhani yameisha na akaamuwa kurudi nyumbani au pengine kuna mtu kamchomesha...........................
 
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
6,582
Likes
11,568
Points
280
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
6,582 11,568 280
Atakuwa alishaandaa majeshi na yakamhakikisia kwamba mambo yapo kwa upande wa vielelezo na mambo mengine
Tatizo ni jiwe mkuu. Kwani kina Ruge na Harbinder si wanashikiliwa kimabavu tuu? Huyu atapotelea mahabusu nakuhakikishia.
 
MSAGA SUMU

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Messages
4,526
Likes
11,435
Points
280
MSAGA SUMU

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined May 25, 2015
4,526 11,435 280
Tanzania imeonesha imekuwa kwenye diplomasia yake, Mahiga alifanya mazungumzo na nchi aliyokimbilia, wakakubali extradition ya mdau. Mazungumzo yanaendelea vizuri US na Finland, kuna fugitives wawili soon watatua Dar kulipa madeni yao kwa jamii
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,270
Likes
30,613
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,270 30,613 280
Ukishakuwa mbongo ni mbongo tu. Mtu kawatoroka vizuri kapanda mpaka basi la abiria kupitia Nairobi sasa karudi tena? Yan kwa jiwe atakaa mahabusu miaka 7. Amejinyea mwenyewe
Nyie mnaona jambo la kawaida hili. Mie Napata mashaka kidogo kuwa usije kuwa mwanzo wa jambo linguine tusilotarajia. Kumbukeni yeye alikuwa nani hapo awali! na kuna usemi wa Kikwere unasema hivi Once a soldier always a soldier nimemkumbuka sana Jerry Rawlings alicheza game mara mbili.
Tukumbuke kuwa huwa wapo watu kazi yao kusubiri wa kulianzisha tuu, kasha wanalicheza!
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
13,582
Likes
11,415
Points
280
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
13,582 11,415 280
HUYU MAKOFIA BANA HATIMAYE AMEJILETA MWENYEWE.MI NILIJUA MUDA HUU ATAKUWA JAMAICA AU KOREA KASKAZINI
Maadam amerudi mwenyewe atajua kwa nini watoto wanaita maji MMA
Sakasaka ya MO kwenye apartments huenda ndio imemfichua!
 

Forum statistics

Threads 1,236,491
Members 475,174
Posts 29,259,708