Hans Pope: Ni nchi nne tu zenye smelting duniani,tanuri moja tu linaweza kula nusu ya umeme wetu

Hebu wengine endeleeni kuleta nondo za hizo smelting plants,maana mdau mmoja hapo juu kasema Zambia wanayo,na kama ni maswala ya umeme nikitafakari,kwa gesi tulionayo ina maana soon haitakuwa issue kwetu,sasa kwanini tuogope!
Mchanga wenywewe unao!!! Umeme tu, domestic use umetushinda leo unaobgelea gas, mna gas nyie au?
 
ndo inabidi tuthubutu.
Wewe huko ni mbali sana, kama mikopo tu ya wanafunzi inatutoa jasho, ndio mtajenga huo mtambo!! Yangu macho, lakini kama ndio mnataka mpigie dili humo la hela ya uchaguzi, baada ya watu kufungua kesi mimi nipo.
 
usituzuge kama umeshakula chochote. sisi tumeambiwa mchanga unaopelekwa wala haujapita kwenye smelter yoyote. kwenye migodi yetu wanayeyusha ule wa juu na ule wa deep down ya migodi wanapeleka nje. siku zote tumekua tunaambiwa ni mchanga kumbe ni kitu tofauti. sasa nyie mnaonasema tuache business as usual wakati rais anataka sote tujue ni thamani kubwa inabebwa sio mchanga ili tupewe haki yetu tuwaeleweje.
Haki ya 3% ya mrahaba una balaha wewe. Nendeni Gabs utaoba mrahaba wanaochukua ni hatareeee
 
....regardless methodologies inayotumika... Namuunga mkono Rais kwa hili la Mchanga ... Tuachane na Umangungo kwenye zama hizi za technologia ... Mbona SGS wanavipimo vinanavyoonesha % ya Gold kwenye Kifusi? Mbona tunajua kuwa kuna madini Zaidi ya Gold kwenye Kifusi? Logically huo mchanga/kifusi itakuwa na thamani kubwa Zaidi ... Wabongo Tuungane kwenye Mambo ya Msingi , tukosoane kwenye ujinga wa wazi wa kipuuzi ....
 
Mtoa post umekaa ukawaza hoja itakayokutoa leo ukaamua ulete hii, sawa tumekusikia ila Mchanga hauendi tena nje au huelewi Kiswahili?
Huyu mkuu achelewi kugeuka na kuacha watetezi kwenye mataa. Wewe bila shaka una uwezo wa fikra binafsi, tu convince kwanini una support? Mimi kwa hili niko zero fa fa fa kabisa zaidi ya kusikia siku za nyuma uongozi wa kijiji Fulani waliuza mchanga kwa dola laki tatu. Kama mna data tuleteeni ili tuelewe ili na sisi tuweze kuchangia.
 
you are cynical. ...have no public trust. JPM is right. he is a visionary leader. the smelting plant is not core in gold mining but gold itself. Tanzania has long lost patriotic leaders thanks God, we now have JPM. If you don't comply with current policy environment, options are open - flee the country or commit suicide.

Ur right visionary reader, vision ni ndoto kwa kiswahili tatizo ndoto zake tu ndio anataka ziwe kweli. Hata watanzania wanazo vision kiongozi anayetakiwa ni wa kuunganisha ndoto za watu wengi ili tupate ndoto ya Taifa sio za raisi.
Vision zake lazima ziendane na za watanzania wengi, watu wanalalamika sababu tunawaza tofauti na ndoto zetu huyu bwana akizifuata tunatusua kwa rahisi sana yeye anatumia nguvu kubwa na anaumiza wengi.
Wewe na yeye mnatakiwa kuchange approach za kutimiza ndoto zenu, hatuhitaji kulimia meno zama hizi wakati kuna machines na technologies.
 
hao wanatuibia Zimbabwe,Zambia,Botswana wana smelting hizo ni Africa tuu mbona mnatudanganya mambo yaliyo wazi kabisa...
 
Hans Pope acha mbwembwe, Zambia na DRC wana smelting plant, je wao wana umeme gani wa ajabu au teknologia gani ?
Kama Acacia wanaona sio economically viable kuweka smelting plant Tz, waache tu mchanga tutauchenjua tukiwa na uwezo, madini hayaozi.

Mkuu unaweza kutupa links ili tuthibitishe na kufahamu undani wa hili?
 
Mtukufu alikuwa na maono kwa hili. Ngoja tusubiri kile alikuwa anakifikiria.
 

Attachments

  • VID-20170326-WA0028.mp4
    3.7 MB · Views: 14
....regardless methodologies inayotumika... Namuunga mkono Rais kwa hili la Mchanga ... Tuachane na Umangungo kwenye zama hizi za technologia ... Mbona SGS wanavipimo vinanavyoonesha % ya Gold kwenye Kifusi? Mbona tunajua kuwa kuna madini Zaidi ya Gold kwenye Kifusi? Logically huo mchanga/kifusi itakuwa na thamani kubwa Zaidi ... Wabongo Tuungane kwenye Mambo ya Msingi , tukosoane kwenye ujinga wa wazi wa kipuuzi ....
Acha ubishi kwa upande wa technology bado hatuwezi kuchenjua madini kwenye mchanga.kama toothpick tunaagiza China pamoja na vijiko smelting plant tunaweza?
 
Mkuu;
Tafuta lugha nyingine ya ku present hii idea. Ni nzuri ila lugha yako haitampendeza mkulu. Najua anayo nafasi kusoma jf na huwa threads kama hizi anazipitiaga mwenyewe.
Sasa basi, hepa Zacharia, lete hapa wazo kuwa, mkulu afanye nini ili awafanye hao wawekezaji wajenge hayo matanuru hapa kwetu??
Elewa, hizo nchi zenye hayo matanuru hazina tena dhahabu ila sasa wanatumia hayo matanuru kwa vitisho kuwa hakuna mwenye uwezo kuyajenga. Sisi tuna dhahabu ya kuchimbwa muda mrefu hivyo waje wawekeze japa.
Uwezo wa umeme wawekeze huko huko pia. Ni mawazo yangu lakini. Simpingi Zacharia bali nimemwomba aangalie hili tatizo kivingine tu
 
Wazee wetu enzi za ukoloni waliambiwa hali ya hewa Afrika haifai kuweka Viwanda, loo! Kumbe huo ujinga hadi leo una mashabiki ! hakuna mashine isiyetengenezwa kulingana na uhitaji wa mteja na tz hatujakose umeme kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini.
 
ANAANDIKA ZACHARIAH HANS POPE
1f449.png
1f449.png
1f449.png
1f449.png
..

Hili suala la mchanga wa dhahabu litaishia kulitia hasara kubwa taifa na hii tabia ya rais kukurupuka na amri kila kukicha kwenye mambo yenye mikataba si sahihi na mwisho wake ni serikali kulipishwa pesa nyingi za walipa kodi bila sababu za maana zaidi ya kujitafutia sifa kirahisi.

Kwenye mikataba ya uchimbaji wa dhahabu inaeleweka kuwa baada ya dhahabu kutolewa kwenye huo mchanga pale mgodini uliobaki unakuwa bado una kama 20% ya dhahabu iliyobaki na kuutupa ni hasara hivyo unapelekwa kwenye smelting plants ambazo ni kama nne tu duniani. Hatuna uwezo wa kujenga matanuri hayo hapa nchini na tanuri moja tu linaweza kula nusu ya umeme tunaozalisha.

Tunakataa nini mchanga huo usiende huko wakati sisi tunapata mrahaba wake. Haya mambo ya kufanya biashara halali iwe haramu overnight ni bad governance na inawafanya wafanya biashara kuwa na wasiwasi wa biashara zao. Viroba ilikuwa halali na watu wakaweka pesa zao leo ni haramu hiyo hasara waliyopata hao wenye biashara nani atawalipa.

Sasa mchanga sasa hili ni la kimataifa na kitachofuatia ni wao kushtaki na tayari washasema wanaingia hasara ya usd 1m kwa siku mwishoe ni kulipishwa. Nakumbuka rais alivyoteuliwa uwaziri kwa mara ya kwanza alianza kwa kuvunja petrol station moja kule mwanza na kilichotokea baada ya hapo ni huyo mwenye hiyo petrol station kutajirikia hapo kwa kulipwa mabilioni na serikali.

Hivi huko ccm hajatokea mtoto wa kumuuliza baba mbona mfalme yuko uchi?
Hans Pope ni muhaini,kauli zake ni za kupuuzwa tu hata zikiwa na maana hawezi kuaminika tena
 
Kwa wadau wa maddini na wataalam u wa mahhesabu je mtambo wa kuchuja na kuchakata mchanga wa madini haswa haswa copper concentrate inayodaiwa kuwemo kwenye makontena yaliyokmatwa ni shilingi ngapi za kitanzania?mtambo huu unatumia umeme kv ngapi kwa siku au kwa kilo ya mchanga?mods tafadhali sana hii nu hoja inayosimama yenyewe.
 
Back
Top Bottom