Ahsante shishi kwa hii thread, maana tunaweza kujifunza vizuri mambo ya financial, haswa jinsi ya kushare mnapokuwa kwenye ndoa.
Mie niko mbioni kuja huko ndoani, ila huyu mwenzangu hataki nichangie kitu chochote, ananiambia yeye atabeba majukumu yote kama mwanaume. Mie hadi woga unanishika, maana kama kipato cha kuchangia ninacho, ila yeye anataka kufanya kila kitu. Je yupo sawa hivi kweli? Maana baadhi ya rafiki zangu wanasema eti ndio mwanaume mzuri, maana nitakuwa huru na pesa zangu. Lakini mimi najiona kama vile kuna walakini.