Hamkani si shwari tena

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
Mipango ilikuwa ni kumuua mlengwa na ikibidi na dereva pia.... Intelijensia iliyotumika haikupangwa na watalaam na pengine kitengo cha usalama mkuu hakikujulishwa ama la kama kikijulishwa zilikuwa habari nusunusu

Kujiamini kulikopitiliza bila kujua kuwa dereva anawachora walianza kulifuatilia gari la mlengwa tangu mbali... Hili lilimpa dereva muda wa kutosha kuisoma na kuikariri number ya usajili (kosa lingine kubwa)
Dereva alilipeleka gari la mlengwa mpaka kwenye maegesho pembeni ya gari nyingine karibu kabisa

DEREVA ALIOKOKAJE NA RISASI ZOTE ZILE?
Umakini, kujipanga, maamuzi sahihi na kudra za mwenyezi Mungu vilisaidia...
Kufika kwenye maegesho wakapaki gari lakini hawakushuka.... Watu wale wasiojulikana wakiwa kwenye gari jeupe wakasogea karibu kabisa na gari la mlengwa lenye vioo vya giza (pengine na la kwao pia lilikuwa na vioo vya Giza)

Assumptions za kukurupuka zikawatuma kuwa mlengwa bado yuko kwenye seat yake ya mbele kushoto na amejawa na woga tele... Hivyo wamshtukize kwa mziki wa risasi... Kazi ikaanza PA!PA! PA! PA! 1 mpaka 30 kishapo jumlisha 8 idadi yake 38

Wanaume wakijua kwa mziki ule washamaliza kazi wakaondoka kwa kujiamini kabisa (kosa la tatu kubwa). Ili uweze kufyatua risasi inabidi ufungue vioo vya gari yako hivyo sura yako kuonekana ni lazima kapelo na miwani mweusi...!

V8 liko juu, Nissan patrol old model iko chini kidogo, nikiwa upande wa dereva wa V8 na wewe uko kwenye Nissan, nikifungua mlango huwezi kuniona....
Dereva alishatoka na kuingia uvungu wa gari ya pili pembeni yake (assumption) mlengwa alishachumpa seat ya dereva japo kwa kuchelewa kidogo na inawezekana naye alichumpa nje (bila kujulikana/kuonekana)

Risasi 38, 30 SMG, 8 PISTOL zikachakaza urembo wa ndani wa V8, bila kuleta madhara kusudiwa.... Ukiwa makini baada ya tendo lazima ukague mazingira (hilo halikufanyika na ni kosa la NNE)

Hamkani si shwari tena, yatokanayo yanaaza kujifunua, dereva hayupo tena, yuko mbali na mkono muovu... Ila alikariri number T 932 AKN kapelo na miwani. Ukiona mtu hatulii kwenye kiti... Ujue halmashauri ya oblongata yake iko busy kupanga na kupangua

Jr[emoji769]
 

Shati alilovaa kabla hajaondoka bungeni ni la bluu ,alilopigwa nalo risasi jeupe
Hii movie imekosewa kidogo tu lakini wangerekebisha kidogo Hollywood ingeingia
Stering mpenda kiki hormorapa
Baada ya lowassa kuingia chadema sects ya maigizo imezidi kushika chat

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni kinachoshabihiana na shati jeupe hapo lakini

Jr[emoji769]
 
Wewe aliekwambia hilo shati aliloshika ndo alikuwa amelivaa ni nani?haiwezi kuwa vest labda au hapo kwenye pic ushaikunjua hiyo nguo kwa hisia kwamba ni shati na kwasababu akili zako zinaamini hivyo unataka na sisi tuamini!je kama ni moja ya nguo zake walizozichukuwa dry cleaner wakatumia kuzuia damu isiendelee kumvuja utajuaje.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…