Hamisi Kigwangalla: Hatujui Dkt. Bashiru alirudisha lini kadi ya CUF. Hatujui namba ya kadi yake ya CCM

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Hatujui kadi yake ya Chama Cha Mapinduzi aliichukuwa lini, hatujui hata kadi yake ya CUF aliirudisha lini?

Tulishangaa tu ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, lakini tuliheshimu mamlaka iliyomteua, sasa tulitegemea awe na Shukrani"

Aliyoandika Kigwangalla kwenye account ya Twitter

Mkiendelea kubisha, kesho ntaenda Serena Press conference nikiwa na nakala ya kadi ya CUF ya Bashiru! Nasisitiza, mlio karibu naye mwambieni aombe radhi na kisha ajiuzulu! Amepuyanga mno kumsema Rais na mfumo mzima kwa hoja za kichochezi zisizo na ushahidi. No one does that.

----
"Hapo nyuma wakulima walilima tu bila kuangalia ubora wa mbegu na ardhi ila Mhe.Rais ametambua umuhimu wa huduma ya afisa ugani ndio maana ameweza kuongeza bajeti kutoka millioni 603 hadi bilioni 15 hii ni kutambua umuhimu wa ugani katika kuongeza au kulipa faida zao shambani "

"Rais samia anafanya mengi sana Mnyonge Mnyongeni ila haki yake mpeni, kuna watu wengi sana ambao wanatumia mwanya huu kupotosha sana Watanzania kwa nia zao mbovu wanazozijua wao "

"Watu wengi sana nyumbani kwa kina Dkt. Bashiru walikuwa wanatorosha kahawa kwenda Uganda ila Mhe.Rais ameboresha utawala bora na kuifungua nchi ndio maana Leo hii mazao yetu yanapata soko zuri ndani na nje ya nchi nakufanya wakulima kunufaika nayo "

" Dkt.Bashiru kwasababu sio mkulima ndio maana hajui kwamba mbolea na pembejeo hapo nyuma zilikuwa bei kubwa ila kwasasa zimeshuka sana, msimu uliopita tulinunua mbolea kiroba kimoja 150,000/= ila mwaka huu kutokana na Ruzuku tunanunua 70,000/= hili bashiru hawezijua kwasababu sio mkulima "

" Kutokana na maelezo aliyotoa Dkt. Bashiru kwa wakulima wadogo wadogo inaonesha dhahili kwa Bashiru hana uelewa na sekta ya kilimo hivyo kabla hajaongea chochote awaulize wakulima na wataalam wa sekta ya kilimo kabla hajaropoka mbele ya umati wa watu "

" Nashangaa sana kuona Dkt.Bashiru kuongea maneno yale ya uwongo kuhusu watawala wakati na yeye alishakuwa mtawala na kupewa nyadhifa mbalimbali serikalini unawezaje sema watawala wake na yeye ni sehem moja ya watawala "

" Dkt.Bashiru alishawahi kuwa mwanachama wa CUF hapo nyuma na alivyokuja CCM hatukuona akirudisha kadi yake wala kuichoma na kwasababu aliteuliwa na kiongozi wetu mkuu kuwa katibu tuliheshimu mamlaka , sasa kama anahisi sio mwenzetu aseme tujua tunamweka kundi lipi na sio kutuchanganya kwa maneno ya uwongo "

" Dkt.Bashiru kipindi cha nyuma akiwa katibu mkuu alishawahi kumshambulia Waziri mkuu mbele ya kikao cha wabunge kitu ambacho sio sawa sisi tulishangaa sana ila tuliheshimu Mamlaka aliyopewa, sasa yeye kama hawezi kuheshimu Mamlaka iliyopo sasa tutamfundisha namna ya kuheshimu na kumkumbusha aliyofanya yeye kipindi cha nyuma"

" Tunashangaa sana kumwona Dkt.Bashiru akikasirika sisi kumsifia Rais wakati anafanya mambo mazuri wakati yeye ndiye aliyetufundisha kumsifia Rais akifanya mazuri, sasa kama yeye anaumia wakati huu ni bora akae kimya tu na sio kutoka hadharani kuongea maneno ya uchochezi "

"Kama Dkt.Bashiru atakuwa anajitambua basi ajitadhimini, aombe radhi kwa Watanzania pia aandike barua ya kuachia nafasi ya ubunge wapewe watu wengine wanaostahiri na yeye aendelee kufanya harakati huko nje "
 
Hizi sarakasi zinazoendelea ngoja tuandae popcorn , Dr Bashiru atapigwa pressure hadi ajiuzuru!

Screenshot_20221121-120417_Twitter.jpg
 
Mh. Bushiru katoa hoja kama watanzania wengine, kinachotakiwa ni kumjibu kwa hoja - sasa mnapokuja kwa maneno ya kejeli na kumtisha sidhani kama inasaidia, hoja ipo mezani ijibiwe tushuhudie.

Hapa mnanikumbusha msemo wa yule mzee wa Shule ya siasa kwamba - Koleza moshi wahuni lazima wataibuka tu... :D
 
Hatujui kadi yake ya Chama Cha Mapinduzi aliichukuwa lini, hatujui hata kadi yake ya CUF aliirudisha lini?

Tulishangaa tu ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, lakini tuliheshimu mamlaka iliyomteua, sasa tulitegemea awe na Shukrani"
HUYU KINGWALANGWALA MSHAMBA MSHAMBA TU, KILA KILA KITU YEYE NI MPENDA KIKI TU, AKAFATILIE BODABODA ZA MSAADA KULE KWA MO
 
Hatujui kadi yake ya Chama Cha Mapinduzi aliichukuwa lini, hatujui hata kadi yake ya CUF aliirudisha lini?

Tulishangaa tu ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, lakini tuliheshimu mamlaka iliyomteua, sasa tulitegemea awe na Shukrani"

You dont listen to politicians ambao wanatetea matumbo yao...unasikiliza wale wanaorisk maisha yao na nafasi zao kwenye siasa kusema ukweli....

Huyu ndugu yetu niwakuupuzwa tu...
 
Bashiru amaeona kinachoendelea labda ni ujingauninga tu,kawa karibu na JPM,kashika nyadhifa nzito,anafanya comparison ya JPM na SHS,anaona machawa wanazingua sana.,ndiyomaana kasema hivyo alivyosema.Hawamuwezi kwa lolote,atarudi kufundisha Kama kawaida,yeye siyo kama ambao siasa kwao ni kila kitu.
 
Hatujui kadi yake ya Chama Cha Mapinduzi aliichukuwa lini, hatujui hata kadi yake ya CUF aliirudisha lini?

Tulishangaa tu ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, lakini tuliheshimu mamlaka iliyomteua, sasa tulitegemea awe na Shukrani"
Akili za Watanzania tunajua a wenyewe tu...
Imagine, Kigwa anajiona ni Prez material na anaota kuna siku atatuongoza kwenda kwenye nchi ya asali na maziwa..... God forbid.
 
Back
Top Bottom