Hamisa Mobetto akanusha madai ya kumkomoa X wake Diamond Platnumz

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Mwigizaji maarufu Bongo Hamisa Mobetto amepuuzilia mbali madai kwamba amekuwa akionekana sana na watu mashuhuri duniani kwa sababu anajaribu kumkomoa aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz.

Akiwa kwenye mahojiano na wanahabari, Mobetto aliweka wazi kwamba kwa kawaida yeye huwa hana matatizo yoyote na mpenzi wake yeyote wa zamani .

Mama huyo wa watoto wawili alisema huwa hafuatilii maisha ya wapenzi wake wa zamani wala kujali kuhusu wanawake watakaochumbia baada yake. Alisema huwa hana kinyongo chochote dhidi ya mpenzi wake yeyote wa zamani.

"Mimi ni mpenzi wa zamani asiye na matatizo. Mimi ni Ex ambaye siwezi kujali kuhusu kile unachofanya sasa hivi. Huwa najali cha kwangu kwa muda wangu. Ikitokea kwamba tumeachana, hayo yameisha. Siwezi kujali ukiwa na mwanamke mwingine na sidhani kama nimewahi kujali kwa Ex wangu yeyote akiwa na mwanamke mwingine. Naamini kwamba kila kitu kinatokea kwa sababu ni chema, kitu kikija kwako ni cha kwako. Kama sio cha kwako basi sio cha kwako. Pia naamini watu huchumbiana na kuachana, mkiachana inamaanisha riziki inaishia hapo ama Mwenyezi Mungu alitaka ufike hapo uendelee na safari. Mimi sijawahi wazia ex wangu yeyote yule vibaya. Sijawahi kufanya kitu kwa ajili ya yeyote yule. Huwa nafanya mambo yangu, na kufanya yale yanayonifurahisha" Alisema Mobetto.

unnamed (1).jpg
 
Back
Top Bottom